Gamba la nyoka
![]() |
Gamba la nyoka |
📚 Gamba la Nyoka ni riwaya inayosawiri mapambano kati ya dola na wananchi wa hali ya chini waliogomea tekelezaji wa mifumo ya uzalishaji mali iliyowalazimisha kuondoka katika maisha na maeneo waliyoyafahamu baada ya ukombozi.
✍️Mwandishi anaangazia namna dola ilivyotumia mabavu kupambana na wakulima wa kawaida ambao hawakukubaliana na uamuzi wa kuwahamisha kutoka katika makazi yao ya jadi na kuwapeleka katika vijiji “vilivyopangwa.”
✍️Ni riwaya inayoangazia pupa za kisiasa katika kufanya uamuzi, na athari zake kwa watu wa kawaida. Unjozi wa mawanio ya kujenga mfumo mpya vijijini unaoneshwa, na hali kadhalika vikoa vya upinzani, baadhi vikiwa ndani ya makanisa na baadhi ndani ya serikali yenyewe.
✍️ Mbali na uhalisia huo, riwaya inaeleza pia falsafa ya mwandishi kuhusu maisha na ubaho, kuhusu dini, imani na Mungu, na kuhusu mabadiliko na mageuzi duniani.
𝗦𝗼𝗺𝗮 𝗿𝗶𝘄𝗮𝘆𝗮 𝗵𝗶𝗶 𝗻𝗮 𝗻𝘆𝗶𝗻𝗴𝗶𝗻𝗲 𝗻𝘆𝗶𝗻𝗴𝗶 𝘁𝗮𝗻𝗱𝗮𝗼𝗻𝗶 𝗸𝘂𝗽𝗶𝘁𝗶𝗮 𝘄𝘄𝘄.𝗹𝗮𝗻𝘁𝗲𝗿𝗻.𝗰𝗼.𝘁𝘇
(www.lantern.co.tz)🔗
Comments
Post a Comment