Posts

Showing posts from July, 2022

Jinsi ya kujua Deni la maegesho

Image
  Deni la maegesho Tarura Parking fees Tanzania kwa sasa imeamua kuama mfumo wa kizamani wa kulipia cash wakati wa parking na kuamia kulipisha kidigitali kwa njia ya simu. Hii yote imeletwa kutokana na changamoto kubwa iliokua ikisababisha pesa nyingi ya serikali kutofika serikalini. TARURA ni Taasisi ya serikali ambayo inahusika na ukusanyaji wa hizi fedha za parking barabarani. Nakala hii itakuelekeza jinsi ya kuangalia chombo chako cha usafiri kinadaiwa bei gani na namna ya kulipa deni hili ili kuepukana na faini. Jinsi ya kuangalia deni la parking Bonyeza *152*00# Chagua namba 4 (Nishati, madini na usafiri) Baada ya hapo chagua namba 2 (Tarura) Kisha chagua namba 2 (Termis/angalia deni) Ingiza namba ya usajiri wa chombo cha usafiri mf. T544 AZZ Utapokea ujumbe mfupi wenye deni lako na kumbukumbu namba ya malipo. Jinsi ya kulipia car parking Bonyeza *152*00# Chagua namba 4 (Nishati, madini na usafiri) Baada ya hapo chagua namba 2 (Tarura) Kisha chagua namba 1(Lipia Maegesho

Jinsi ya kuangalia Deni la gari

 Je unataka kujua unadaiwa kiasi gani Kama faini ya gari yako? Je umemwazimisha mtu gari lako na ungependa kujua iwapo alitenda kosa BARABARANI na kuandikiwa faini? Hii hapa jinsi ya kuangalia Deni la gari lako kutokana na faini zitokanazo na makosa ya gari lako. Vitu vya kuandaa, andaa namba ya gari lako, Kisha ingiza msimbo wa gari lako baada ya kubofya >>HAPA>> Iwapo unekuta Deni hii hapa jinsi ya kulipa Deni la gari lako  Zifuatazo ni njia za kulipia deni la traffic:  Kupitia matawi ya benki:  NBC  NMB  CRDB  Kupitia mitandao ya simu Lipa kwa kutumia namba ya kampuni  001001  kisha weka kumbukumbu namba yako iliyopo kwenye TMS au receipt uliyopatiwa

SHABAN KAONEKA VS MANDONGA

Image
 Mpambano Kati ya Shabani KAONEKA na MANDONGA MTU KAZI umemalizika ambapo bondia MANDONGA ameambulia kichapo TKO raundi ya nne ya mpambano.

Papa Francis : Ninaweza kustaafu - lakini muda mwafaka haujafika

Image
Maelezo ya picha, Papa Francis akihutubia wanahabari Dakika 15 zilizopita Kiongozi wa Kanisa Ktoliki Duniani Papa Francis amesema anaweza kustaafu hivi karibuni - na atafanya hivyo ikiwa atahisi kuwa afya yake haitamruhusu kuhudumu ipasavyo. Alitoa  kauli hiyo mwishoni mwa ziara yake nchini  Canada- ambako aliomba msamaha kwa watu wa kiasili – katika safari ambayo ilihusisha shughuli nyingi na siku ndefu. Papa mwenye umri wa miaka 85 alisisitiza kuwa kwa sasa ana nia ya kuendelea na majukumu yake - na ataongozwa na Mungu ni lini ataondoka madarakani. "Sio ajabu kumbadilisha Papa, sio mwiko," aliwaambia waandishi wa habari kutoka kwa kiti cha magurudumu kwenye ndege kutoka eneo la Arctic la Kanada hadi Roma. "Mlango [wa kustaafu] uko wazi - ni jambo la kawaida. Lakini mpaka leo sijagonga mlango huo. Sijaona haja ya kufikiria juu ya uwezekano huu - sio kumaanisha kwamba katika muda wa siku mbili nisianze kufikiria juu ya hilo." Katika miezi ya hivi kari...

AKUTWA AMEFARIKI GESTI BAADA YA KURUSHANA ROHO NA MREMBO

Image
  Polisi huko Migori wanachunguza kisa ambacho kinaripotiwa kuwa mwanaume mwenye umri wa miaka 52 anadaiwa kuzimia na kufariki katika nyumba ya kulala wageni (Guest House) asubuhi ya jana ijumaa nchini Kenya. Kwa mujibu wa Kurugenzi ya Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI), marehemu; Naftali Nyandera, na mpenzi wake wa miaka 24 walikuwa kwenye nyakati nzuri kwenye nyumba ya kulala wageni kabla ya kifo chake. "Katika kisa hicho ambacho kiliwashangaza wakazi wa Kanyarwanda, mwili wa Naftali Nyandera uligunduliwa ukiwa umetulia bila ya kutikisika kwenye kitanda katika nyumba ya kulala wageni ya Lavanda, baada ya shughuli nyingi zilizofanyika jioni na msichana huyo," ilisema taarifa ya DCI. Uchunguzi wa awali wa DCI ulibaini kuwa mwanaume huyo alianguka saa chache baada ya kuingia chumbani na mwanamke huyo. "Maafisa wa polisi wa kituo cha polisi cha Macalder waliitwa katika eneo la tukio na kubaini kuwa mzee huyo mwenye umri wa miaka 52 aliingia ndani ya chumba hic...

Matabibu waripoti kupona kwa mgonjwa wa nne wa VVU

Image
  Chanzo cha picha, Getty Images Mwanaume ambaye ameishi na virusi vya Ukimwi tangu miaka ya 1980 amepona, madaktari wake wamesema. Ili kutibu saratani ya damu , mgonjwa alipokea upandikizaji wa uboho kutoka kwa wafadhili ambaye kwa asili alikuwa sugu kwa virusi hivyo. Mzee ambaye hapendi kutambulika aliacha kutumia dawa za kupunguza makali ya VVU. Hiki ni kisa cha nne kuripotiwa na wanasayansi. Mgonjwa alisema "  anashukuru sana ” kwamba virusi haviko tena mwilini mwake. Mwanaume huyo alipokea huduma ya matibabu katika Kituo cha Tiba ya Saratani ya Jiji la Hope huko Duarte, California. Marafiki zake wengi walikufa kutokana na HIV kabla ya dawa za kurefusha maisha kuwapa wagonjwa muda wa kawaida wa kuishi. "Sina VVU tena" VVU huharibu mfumo wa kinga. Hii inaweza kusababisha ugonjwa wa upungufu wa kinga mwilini (UKIMWI) kwani mwili una wakati mgumu kupambana na maambukizi. Chanzo cha picha, Getty Images "Nilipogundulika kuwa na VVU mwaka 1988, kama w...

SABAYA AFANYIWA UPASUAJI KESI YAAHIRISHWA

Image
  Mawakili wa upande wa utetezi kesi namba mbili ya mwaka 2022, inayomkabili aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai, Lengai Ole Sabaya na wenzake wanne wameieleza mahakama ya Hakimu Mkazi Moshi kuwa hali ya Sabaya ni mbaya baada ya kufanyiwa upasuaji mkubwa wa kichwa Julai 27 mwaka huu. Sabaya na wenzake wanne wanakabiliwa na mashtaka saba likiwamo la uhujumu uchumi na matumizi mabaya ya ofisi wakati akiwa Mkuu wa wilaya hiyo. Juni Mosi mwaka huu, Sabaya na wenzake wanne walipandishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Moshi na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) na kusomewa mashtaka yanayowakabili mbele ya hakimu mkazi Mfawidhi, Salome Mshasha. Washitakiwa wengine katika kesi hiyo ni Sylvester Nyegu, John Aweyo, Nathan Msuya na Antero Assey. Hata hivyo Sabaya ambaye ni mshtakiwa namba moja katika kesi hiyo alifikishwa mahakamani hapo leo kichwa chake kikiwa kimeviringishwa bandeji huku mkononi akiwa na kifaa cha kuchomekea dripu. Awali wakili wa Sabaya, Fridoli...

Makarani watakaovujisha Siri za sensa kutupwa jela

Image
  MAKARANI na wasimamizi wa maudhui na Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (Tehama) 205,000 watakaovujisha taarifa za sensa ya watu na makazi watafungwa miaka miwili jela au kulipa faini ya Sh milioni mbili au vyote kwa pamoja.  - Makarani watakaofuzu mitihani watatakiwa kufika kwenye maeneo ya kaya Agosti 21 na 22 kujifunza maeneo ya kaya ili kuelewa mipaka na kuhoji dodoso la jamii. Mtakwimu Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu, Dk Albina Chuwa jana alitoa majukumu saba kwa watendaji wa kata Tanzania Bara na masheha wa Zanzibar ambao watapata mafunzo kwa siku mbili; Julai 31 na Agosti Mosi. - Dk Chuwa alitaja miongoni mwa majukumu hayo kuwa ni kuhamasisha na kuelimisha umma kupitia redio, ngoma na mikutano wakishirikiana na sekta binafsi. Alisema watafanya kazi kwa kushirikiana na watendaji wa vijiji, mitaa na vitongoji katika kutoa ushirikino kwa makarani na kuwatambulisha katika kaya. - Dk Chuwa alisema suala la sensa ni la kikatiba hivyo watakaoliharibu watakumbana na mkono ...

NAFASI MPYA ZA KAZI SERIKALINI LEO

Image
  Hizi hapa nafasi mbalimbali za kazi zilizo tangazwa leo. Advertisement  TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI HALMASHAURI YA WILAYA YA WANGING'OMBE 28-07-2022  TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI HALMASHAURI YA MANISPAA YA MTWARA - MIKINDANI 28-07-2022

HAYA HAPA MAJINA YA WALIOITWA KWENYE USAILI HALMASHAURI MBALIMBALI

Image
  -Walioitwa kwenye Usaili Kahama -Handeni Ifakara Buchosa Chato Mbozi Uvinza Call For Interview  TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI MANISPAA YA KAHAMA 28-07-2022  TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI HALMASHAURI YA WILAYA YA HANDENI 28-07-2022  TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI HALMASHAURI YA MJI IFAKARA 28-07-2022  TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI BUCHOSA DC 27-07-2022  TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI CHATO DC 26-07-2022  TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI HALMASHAURI YA WILAYA YA MBOZI 26-07-2022  TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI HALMASHAURI YA WILAYA YA BUNDA 26-07-2022  TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI HALMASHAURI YA WILAYA YA UVINZA 26-07-2022

Mwalimu wa sensa akutwa amefariki Gesti

Image
  Kamanda wa Polisi mkoa wa Tabora, Richard Abwao Bahati Msengi ambaye ni mkufunzi wa sensa amekutwa amefariki dunia katika nyumba ya kulala wageni, Kata ya Kanyenye mkoani Tabora. Mkufunzi huyo ambaye pia alikuwa afisa elimu kata ya Milambo, wilayani Kaliua mkoani humo, alihudhuria mafunzo ya siku 21 yaliyomalizika juzi Jumanne na kufungwa na mkuu wa mkoa wa Tabora, Dk Batilda Burian, katika Chuo Cha Ualimu Tabora. Kamanda wa Polisi mkoa wa Tabora, Richard Abwao amesema tukio hilo ni kifo cha kawaida kama vifo vingine vinavyotokea hospitalini. Soma zaidi <<HAPA>> Via Mwananchi

TAARIFA MUHIMU KUTOKA OFISI YA TAIFA YA TAKWIMU (NBS) KUHUSU MAANDALIZI YA SENSA YA WATU NA MAKAZI YA MWAKA 2022

Image
  Download taarifa kamili PDF >>HAPA>>

MAJINA YA WALIOPITA USAILI SENSA YA WATU NA MAKAZI 2022

Image
  Wengi waliofanya usaili wa sensa ya watu na makazi wamekuwa wakijuiliza je majina ya waliochaguliwa kufanya zoezi au AJIRA za sensa 2022 yatatolewa lini? Contents - Maandalizi ya Sensa ya watu na makazi ya mwaka 2022 - Ratiba ya mchakato wa kupata majina ya watakaofanya zoezi la Sensa - MAJINA AJIRA ZA SENSA 2022 . -Majina ya waliochaguliwa Sensa pdf - Jinsi ya ya kuangalia majina ya waliochaguliwa ajira za Sensa 2022. Maandalizi ya Sensa ya watu na makazi ya mwaka 2022 Utangulizi Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imepanga kufanya Sensa ya Watu na Makazi ifikapo mwezi Agosti 2022. Wizara ya Fedha na Mipango kupitia Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) kwa kushirikiana na Ofisi ya Mtakwimu Mkuu wa Serikali Zanzibar (OCGS), ipo kwenye maandalizi ya kufanya Sensa hiyo. Sensa ya Watu na Makazi ni zoezi la kitaifa linalofanyika kila baada ya miaka 10 ambapo Sensa ya mwisho kufanyika nchini ni ile ya mwaka 2012. Hivyo Sensa ya mwaka 2022 itakuwa ni sensa ya Sita kufanyika nchini b...

HAYA HAPA MAJINA YA WALIOFAULU NA KUPITA USAILI AJIRA ZA SENSA 2022

Image
  Ulifanya usaili wa Sensa ya watu na makazi? Haya hapa matokeo ya usaili. Moshi  is a municipality and the capital of  Kilimanjaro region  in the north eastern Tanzania. As of 2017, the municipality has an estimated population of 201,150 and a population density of 3,409 persons per km 2  . [2]  In the last official census of 2012, the municipality had a population of 184,292. The municipality is situated on the lower slopes of  Mount Kilimanjaro , a dormant volcano that is the highest mountain in Africa. The name  Moshi  has been reported to refer to the smoke that emanates from the nearby mountain.The municipality covers about 59 square kilometres (23 sq mi) and is the smallest municipality in Tanzania by area. Bofya >>HAPA kupakua pdf Source: moshimc.go.tz

Nchi 10 tajiri zaidi barani Afrika

Image
  Chanzo cha picha, WORLD BANK Bara la Afrika linatajwa kuwa maskini zaidi duniani, huku umaskini wa bara hilo ukichangiwa na hali ya uchumi kuyumba, ukosefu wa usalama, ufisadi, vita vya wenyewe kwa wenyewe na vitendo vya kigaidi katika bara hilo. Shirika la Fedha Duniani IMF na Benki ya Dunia, katika ripoti ya pamoja iliyochapishwa mwishoni mwa 2021, zimetangaza nchi 10 tajiri zaidi barani Afrika. 1. Misri Misri imekuwa nchi ya kwanza barani Afrika kuwa na ukuaji wa juu wa uchumi (GDP) kulingana na ripoti hiyo. Mapato ya kila mwaka ya Misri ni $1.38 trilioni. Misri ina jumla ya watu milioni 102, na nchi hiyo inategemea kilimo, uchimbaji madini na utalii. 2. Nigeria Nigeria, ambayo ni ya pili tajiri zaidi barani Afrika, ina pato la taifa la dola trilioni 1.14. Nigeria ina jumla ya watu milioni 206.1, ikiifanya kuwa nchi yenye watu wengi zaidi duniani. Uchumi wa Nigeria unategemea mafuta na kilimo. 3. Afrika Kusini Afrika Kusini, ambayo ni nchi tajiri zaidi barani A...