AKUTWA AMEFARIKI GESTI BAADA YA KURUSHANA ROHO NA MREMBO
Polisi
huko Migori wanachunguza kisa ambacho kinaripotiwa kuwa mwanaume mwenye
umri wa miaka 52 anadaiwa kuzimia na kufariki katika nyumba ya kulala
wageni (Guest House) asubuhi ya jana ijumaa nchini Kenya.
Kwa
mujibu wa Kurugenzi ya Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI), marehemu;
Naftali Nyandera, na mpenzi wake wa miaka 24 walikuwa kwenye nyakati
nzuri kwenye nyumba ya kulala wageni kabla ya kifo chake.
"Katika
kisa hicho ambacho kiliwashangaza wakazi wa Kanyarwanda, mwili wa
Naftali Nyandera uligunduliwa ukiwa umetulia bila ya kutikisika kwenye
kitanda katika nyumba ya kulala wageni ya Lavanda, baada ya shughuli
nyingi zilizofanyika jioni na msichana huyo," ilisema taarifa ya DCI.
Uchunguzi wa awali wa DCI ulibaini kuwa mwanaume huyo alianguka saa chache baada ya kuingia chumbani na mwanamke huyo.
"Maafisa
wa polisi wa kituo cha polisi cha Macalder waliitwa katika eneo la
tukio na kubaini kuwa mzee huyo mwenye umri wa miaka 52 aliingia ndani
ya chumba hicho akiwa ameongozana na msichana mwenye nusu ya umri wake,
na kuzimia saa kadhaa baadaye kufuatia tukio la jioni," DCI alisema.
Mwili
wa marehemu ulihamishwa kupelekwa katika chumba cha kuhifadhi maiti cha
Migori level IV ukisubiri uchunguzi wa maiti kufanyika.
Comments
Post a Comment