Skip to main content

Papa Francis : Ninaweza kustaafu - lakini muda mwafaka haujafika



Papa Francis akihutubia wanahabari kwenye ndege ya Papa
Maelezo ya picha,

Papa Francis akihutubia wanahabari

Kiongozi wa Kanisa Ktoliki Duniani Papa Francis amesema anaweza kustaafu hivi karibuni - na atafanya hivyo ikiwa atahisi kuwa afya yake haitamruhusu kuhudumu ipasavyo.

Alitoa  kauli hiyo mwishoni mwa ziara yake nchini  Canada- ambako aliomba msamaha kwa watu wa kiasili – katika safari ambayo ilihusisha shughuli nyingi na siku ndefu.

Papa mwenye umri wa miaka 85 alisisitiza kuwa kwa sasa ana nia ya kuendelea na majukumu yake - na ataongozwa na Mungu ni lini ataondoka madarakani.

"Sio ajabu kumbadilisha Papa, sio mwiko," aliwaambia waandishi wa habari kutoka kwa kiti cha magurudumu kwenye ndege kutoka eneo la Arctic la Kanada hadi Roma.

"Mlango [wa kustaafu] uko wazi - ni jambo la kawaida. Lakini mpaka leo sijagonga mlango huo. Sijaona haja ya kufikiria juu ya uwezekano huu - sio kumaanisha kwamba katika muda wa siku mbili nisianze kufikiria juu ya hilo."

Katika miezi ya hivi karibuni Papa Francis amepata matatizo ya goti ambayo yameathiri uwezo wake wa kutembea.

Alitumia muda mwingi wa ziara yake nchini Canada akiwa kwenye kiti cha magurudumu. Lakini hapo awali alitupilia mbali uvumi kwamba anaugia magonjwa hatari zaidi, yanayotishia maisha.


"Safari hii imekuwa na shughuli nyingi," alisema. "Sidhani kama naweza kuendelea kusafiri jinsi nilivyokwa nikisafiri katika umri wangu huu na ugumu wa goti hili.

"Ama nahitaji kujiokoa kidogo ili kuendelea kutumikia Kanisa, au ninahitaji kufikiria uwezekano wa kujiondoa."

Papa - ambaye mtangulizi wake Benedict XVI alistaafu kutokana na afya mbaya mwaka 2013 - alisema kwamba alikuwa na nia ya kuzuru Ukraine hivi karibuni, lakini itabidi atafute ushauri wa madaktari wake kwanza.

Katika ziara yake nchini Canada, lengo kuu lilikuwa kuomba radhi watu wa kiasili wa eneo hilo kwa makosa waliyofanyiwa na wale wa Kanisa Katoliki.

Papa alionekana kujishughulisha zaidi na mwingiliano wake na watu wa eneo hilo - haswa waathirika wa unyanyasaji katika shule za Kikatoliki.

Lakini kuna nyakati hasa wakati wa baadhi ya taratibu rasmi na wanasiasa ambapo uchovu wake ulionekana dhahiri.

Chanzo: BBC

Comments

Popular posts from this blog

HIZI HAPA SMS TAMU ZA KUMTAKIA USIKU MWEMA MPENZI WAKO

SMS na MESEJI 900+ za mapenzi

MIAKA 22 SASA TANGU KUZAMA KWA MELI KUBWA YA MV BUKOBA, TANZANI TUMEJIFUNZA NINI?