Makarani watakaovujisha Siri za sensa kutupwa jela
MAKARANI na wasimamizi wa maudhui na Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (Tehama) 205,000 watakaovujisha taarifa za sensa ya watu na makazi watafungwa miaka miwili jela au kulipa faini ya Sh milioni mbili au vyote kwa pamoja.
-
Makarani watakaofuzu mitihani watatakiwa kufika kwenye maeneo ya kaya Agosti 21 na 22 kujifunza maeneo ya kaya ili kuelewa mipaka na kuhoji dodoso la jamii. Mtakwimu Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu, Dk Albina Chuwa jana alitoa majukumu saba kwa watendaji wa kata Tanzania Bara na masheha wa Zanzibar ambao watapata mafunzo kwa siku mbili; Julai 31 na Agosti Mosi.
-
Dk Chuwa alitaja miongoni mwa majukumu hayo kuwa ni kuhamasisha na kuelimisha umma kupitia redio, ngoma na mikutano wakishirikiana na sekta binafsi. Alisema watafanya kazi kwa kushirikiana na watendaji wa vijiji, mitaa na vitongoji katika kutoa ushirikino kwa makarani na kuwatambulisha katika kaya.
-
Dk Chuwa alisema suala la sensa ni la kikatiba hivyo watakaoliharibu watakumbana na mkono wa sheria.
Comments
Post a Comment