Mwalimu wa sensa akutwa amefariki Gesti
Kamanda wa Polisi mkoa wa Tabora, Richard Abwao
Bahati
Msengi ambaye ni mkufunzi wa sensa amekutwa amefariki dunia katika
nyumba ya kulala wageni, Kata ya Kanyenye mkoani Tabora.
Mkufunzi
huyo ambaye pia alikuwa afisa elimu kata ya Milambo, wilayani Kaliua
mkoani humo, alihudhuria mafunzo ya siku 21 yaliyomalizika juzi Jumanne
na kufungwa na mkuu wa mkoa wa Tabora, Dk Batilda Burian, katika Chuo
Cha Ualimu Tabora.
Kamanda
wa Polisi mkoa wa Tabora, Richard Abwao amesema tukio hilo ni kifo cha
kawaida kama vifo vingine vinavyotokea hospitalini.
Via Mwananchi
Comments
Post a Comment