Posts

Showing posts from January, 2018

UNHCR Yadai wakimbizi 1,200 wakimbilia Tz kutoka Congo

Image
  Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia wakimbizi la UNHCR, limedai kuwa jumla ya wakimbizi 1200,raia wa jamhuri ya Demokrasia ya Congo,wameyakimbia mapigano yanayoendelea Mashariki mwa nchi hiyo na kuingia Tanzania. Aidha shirika hilo limedai Maelfu ya watoto, wanawake na wanaume, wameacha makazi yao kukimbia mapigano dhidi ya makundi yenye silaha ya Mai Mai yanayoendelea Kusini mwa Jimbo la Kivu. Aidha shirika hilo la umoja wa mataifa limedai mbali na Tanzania,wakimbizi wengine wamekimbilia nchi za Burundi, na Uganda. Wakati huo huo, inaamika kwamba, kuna wimbi kubwa zaidi la wakimbizi ambao wapo Kivu Kusini wakiwa katika hali mbaya ya kukosa chakula na makazi.

SIMBA NDIYE BINGWA MPYA VPL 2017/2018 SABABU HIZI HAPA

Image
Na Masshele Emanuel SIMBA imefanikiwa kushinda mechi nne mfululizo kwa idadi kubwa ya mabao ambayo yanaifanya kuwa timu hatari zaidi katika kipindi hiki unapozungumzia Ligi Kuu Bara. Katika mechi nne, Simba imekusanya pointi 12, maana yake imeshinda bila ya kupotea hata moja, jambo ambalo linaonyesha mwendo wao ni mzuri zaidi. Lakini utaona katika mechi zote nne, Simba imeshinda mabao 2-0 katika mechi mbili na 4-0 katika mechi mbili. Hawajaruhusu hata bao moja kutinga katika nyavu zao. Katika ligi kama ya sasa ambayo ugumu wake unajulikana, timu kucheza mechi nne na kufunga mabao 12, si jambo dogo. Lakini timu kucheza mechi nne bila ya kuruhusu hata bao moja, maana yake ni kiwango bora kabisa cha utendaji kwa maana ya ulinzi na ushambulizi. Mechi tatu za mwanzo, Simba iliifunga Ndanda FC kwa mabao 2-0 ikiwa ugenini, ikaitwanga Singida United 4-0 jijini Dar es Salaam na kusafiri kwenda Bukoba ambako waliivurumisha Kagera Sugar 2-0. Hapa kikosi kilikuwa chini ya ...

Umri wa Kustaafu Kwa Madaktari Bingwa, Wahadhiri Waandamizi na Maprofesa Sasa miaka 65.

Image
Frank Mvungi- Maelezo, Dodoma. Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania limepitisha muswaada wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria mbalimbali ikiwemo sheria ya Utumishi wa Umma, Sura ya 298  (The Public Service Act) itakayowezesha muda wa kustaafu kwa  Wahadhiri waandamizi, Maprofesa na Madaktari Bingwa kuwa miaka 60 kwa hiari na lazima miaka 65. Akizungumza wakati akiwasilisha muswaada huo  Mwanasheria  Mkuu wa Serikali Mhe. George Masaju amesema kuwa marekebisho katika jedwali yanapendekeza kuongezwa kwa kifungu kipya cha 25A ambacho kinaainisha kuhusu umri wa kustaafu ambapo kwa sasa sheria ilivyo  haina masharti hayo isipokuwa umri wa kustaafu umetajwa katika sheria zinazoanzisha mifuko ya hifadhi za jamii. Aliongeza kuwa, uzoefu umeonyesha kuwamba Maprofesa na Wahadhiri waandamizi wa vyuo  Vikuu  vya Umma pamoja na madaktari Bingwa wa Binadamu wa Hospitali za Umma wamekuwa wakihitajika kuendelea kutoa huduma, utaalamu na ...

Ultimate transfer scramble: Giroud, Aubameyang, Batshuayi

Image
The January transfer window has already seen a successful swap of players, with Mkhitaryan joining Arsenal from Manchester United and Sanchez going the other way. According to  The Mirror , Arsenal’s signing of BvB’s Aubameyang depends on Chelsea landing Giroud and loaning out Batshuayi to Borussia Dortmund. It is turning out to be a complicated chain of sale, as no club seems to accept losing their striker without securing a replacement. Arsenal is said to have paid £55 million for the Gabon striker and is willing to accept £15m plus add-ons for French man Giroud. The scramble Once a deal for Giroud is in place, Chelsea will allow Batshuayi to sign for Dortmund on loan, subsequently triggering Aubameyang’s release to London. Auba recently had problems with the Dortmund hierarchy and was even booed by fans during his recent appearance in the Bundesliga. If signed by Arsenal, he will become the best-paid player in the club’s history on a three-and-a-half-year contract ...

Manchester United handed tricky FA fixture

Image
Manchester United will take on Huddersfield or Birmingham following the FA Cup fifth round draw conducted on Monday 29th January 2018.   Jose Mourinho‘s men beat Yeovil 4-0 last Friday to book their spot in the draw and they await a replay to find out who they take on in February. Elsewhere, Chelsea were drawn against Hull after comprehensively beating Newcastle 3-0 at Stamford Bridge on Sunday while Manchester City will take on Wigan. Fourth round replays including Tottenham vs Newport  are set to take place on February 6/7. The fifth round is scheduled to take place on the weekend of February 17-18

Serikali imezima matangazo ya Television Kenya

Image
  Wakati wafuasi wa Muungano wa upinzani nchini Kenya (NASA) wanaendelea na shughuli ya kuapishwa kwa Raila Odinga kuwa ‘Rais’ serikali nchini humo imepiga marufuku TV za Kenya kurusha LIVE matangazo hayo kutoka katika uwanja wa Uhuru Park TV hizo ni Citizen, KTN na NTV. Wafuasi wa Upinzani tayari wamekwisha fika katika uwanja wa Uhuru Park kushuhudia tukio hilo Inaelezwa kuwa serikali nchini Kenya ilikuwa imekwisha tahadharisha kuhusu vyombo vya habari nchini humo kurusha live matangazo hayo ya Odinga kuapishwa ambapo ni kinyumme cha sheria. Hata hivyo vyombo vya habari vya kimataifa havijafungiwa na vinaendelea kurusha matangazo hayo kama kawaida.

Shule 10 BORA na Shule 10 za Mwisho Matokeo ya Kidato cha Nne 2017

Image
Baraza la mitihani Tanzania (NECTA) limetangaza matokeo ya kidato cha nne kwenye mtihani ambao ulifanyika October 2017 ambapo Shule  iliyoshika namba moja inatoka Mbeya. TOP 10 YA SHULE BORA. 1. St. Francis Girls ya Mbeya 2. Feza Boys ya Dar es salaam 3. Kemebos ya Kagera   4. Bethel Sabs Girls ya Iringa   5. Anwarite Girls ya Kilimanjaro   6. Marian Girls Pwani   7. Canossa ya Dar es salaam   8. Feza Girls ya Dar es salaam   9. Marian Boys ya Pwani   10. Shamsiye Boys ya Dar es salaam   TOP 10 YA SHULE ZA MWISHO KITAIFA 10. Mtule ya Kusini Unguja 9. Nyeburu ya Dar es salaam 8. Chokocho ya Kusini Pemba 7. Kabugaro ya Kagera 6. Mbesa ya Ruvuma 5. Furaha ya Dar es salaam 4. Langoni ya Mjini Magharibi 3. Mwenge S.M.Z ya Mjini Magharibi 2. Pwani Mchangani ya Kaskazini Unguja 1. Kusini ya Kusini Unguja

BREAKING: Raila Odinga Ajiapisha Kuwa ‘Rais wa Wananchi wa Kenya’

Image
Kiongozi  wa upinzani Raila Odinga (NASA) ameapishwa kuwa ‘Rais wa Wananchi’ wa Kenya licha ya kugomea uchaguzi mkuu wa marudio nchini humo. Raila Odinga amefika  leo katika Uwanja wa Uhuru Park pamoja na viongozi wengine wakuu wa NASA akiwemo Moses Wetangula na Musalia Mudavadi na kujiapisha akishika Biblia. Aidha, mgombea mwenza wake Kalonzo Musyoka wa Chama Cha Wiper hakuwepo wakati wa kuapishwa kutokana na kuhofia kukamatwa, ambapo Odinga amesema ataapishwa baadaye. “Odinga amesema leo ni siku ya kihistoria kwa Kenya, hatua ya leo ni kuelekea kutoa udikteta na kuleta demokrasia Kenya, maelekezo mengine mtayapata baadae,” alisema Odinga baada ya kuapishwa. Awali Raila Odinga aliiambia kituo cha habari cha KTN kwamba shughuli hio ‘ si mapinduzi ya serikali’ Raila aligomea uchaguzi huo kwa sababu za kusema kuwa tume ya Uchaguzi nchini humo si ya Uhuru na haki. Uchaguzi huo wa marudio ulikuja baada ya Mahakama ikiongozwa na Jaji Maraga kutengua Uchaguz...

HII NDIO HOTUBA YA MWISHO YA HAYATI MUAMMAR GADDAFI

Image
QADAFFI ANAANZA HIVI: "Kwa jina la Mwenyezi Mungu (Allah), Mungu mpaji, na mwenye rehema.... Kwa miaka takribani 40 ama ilikuwa zaidi sikumbuki. Nachokumbuka ni kuwa nilifanya kila nilichoweza kuwapa watu wangu nyumba, hospitali na shule. Na kila walipohisi njaa niliwapa chakula. Niliifanya Benghazi kutoka jangwa kuwa ardhi nzuri ya kilimo. Nilisimama imara dhidi ya Ronald Regan (Rais wa zamani wa Marekani), alipomuua binti yangu niliyemuasili. Alikua anajaribu kuniua mimi lakini akamuua yule binti yatima masikini. Niliwasaidia kaka na dada zangu waafrika fedha kupitia AU. Nilifanya kila nililoweza kuwafanya watu wangu waelewe maana halisi ya demokrasia; ambapo watu wa tabaka la chini niliwapa madaraka. Lakini hawakuridhika. Hata aliyekuwa na nyumba ya vyumba kumi, nguo mpya, na fanicha nzuri, hakuridhika. Alihitaji zaidi. Kwa jinsi walivyokuwa wabinafsi walihitaji zaidi. Hivyo wakawaambia Marekani kuwa wanataka "demokrasia" na "uhuru". Hawakuj...

Morata urges Chelsea to sign United target

Image
Chelsea striker Alvaro Morata is reportedly pushing for his club to seal the transfer of Real Madrid winger Marco Asensio, who has also been linked with Manchester United. The Spain international moved from the Bernabeu to Stamford Bridge last summer but has not yet had the best of times since switching to English football. Still, Morata could have some exciting influence in the transfer market if all goes to plan, as he looks for Chelsea to raid his old club Real Madrid for the signing of Asensio, according to Diario Gol.  Manchester United was also in for Asensio, having even tabled a staggering £177 million bid for the Spaniard.  The 22-year-old is regarded as one of the most exciting young players in Europe at the moment but hasn’t enjoyed as much playing time for  Los Blancos  this season.

United hope to complete £50 million deal before deadline day

Image
Manchester United is still hopeful of signing Shakhtar Donetsk midfielder Fred before the end of the January transfer window. The 24-year-old, who joined the Ukrainian side from Internacional in 2013, has been... Money and performance City manager Pep Guardiola recently admitted the Sky Blues can’t compete financially with United, but they are still in the running for Fred. The Brazilian international has made 142 appearances for Shakhtar in the last five years, and the  Daily Star  says he could set clubs back around £50m. The midfielder has been a regular in the Shakhtar side, making 24 appearances in all competitions this season, and would bring a lot to United’s engine room. Fred’s a combative player, as well as boasting fantastic box-to-box abilities, and will also provide an assured head in the middle of the park. He won’t come cheap, but the Red Devils are in need of midfield reinforcement. Michael Carrick will retire at the end of the season, while Marouane ...

Bayern Munich agree to sell Man United and Chelsea midfield target

Image
Bayern Munich has promised Arturo Vidal he will be allowed to leave the club in the summer amid major interest from Manchester United and Chelsea. The Bundesliga champions have wrapped up a deal to sign  Leon Goretzka  on a free transfer from Schalke in June, at which point Vidal is expected to fall down the midfield pecking order at the Allianz Arena. Conscious of Vidal’s desire for first-team football and his big salary, Bild report that Bayern have granted the Chilean permission to begin looking for a summer move.Vidal’s contract expires in 2019 and he will be available for a reasonable price come summer, when he will be entering the final year of his deal. The 30-year-old is already attracting a lot of interest, with some reports claiming that Alexis Sanchez is trying to lure his compatriot to Old Trafford.

Manula aweka rekodi ya kutofungwa Simba

Image
Golikipa wa vinara wa ligi kuu soka Tanzania Bara Simba SC Aishi Manula amefanikiwa kujiwekea rekodi ya pekee tangu ajiunge na klabu hiyo mwezi Juni 2017 akitokea Azam FC. Manula ameichezea Simba mechi 20 ambapo kati ya hizo mechi 14 hajaruhusu lango lake kufungwa hata bao moja hivyo kuwa msaada mkubwa kwa kikosi hicho kinachoongoza ligi kwa alama 35. Katika rekodi hiyo ya Manula  mechi za kukumbukwa zaidi ni mechi yake ya kwanza ndani ya Simba ambayo ilikuwa siku ya Simba Day dhidi ya Rayol Sports ya Rwanda. Simba iliibuka na ushindi wa bao 1-0. Mechi nyingine ni ile dhidi ya Yanga kwenye mchezo wa Ngao ya Hisani ambayo ilikuwa ni mechi yake pili kwake na timu hizo zilitoka sare ya 0-0 katika dakika 90. Mechi ya kwanza ya ligi kwa Manula akiwa na Simba ilikuwa ni ushindi wa 7-0 dhidi ya Ruvu Shooting. Mechi nyingine ambazo zimebaki kama alama ya uwezo wa Manula ndani ya Simba ni mechi tatu za mwisho kwenye mzunguko wa kwanza wa ligi, Simba ikishinda 4-0 dhidi ya Singid...

WAZIRI JAFO, MADARASA YA TEMBE, UDONGO, NYASI, YASITUMIKE KATIKA SHULE YEYOTE NCHINI

Image
Nteghenjwa Hosseah, OR-TAMISEMI. Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Selemani Jafo amewaagiza Wakuu wa Wilaya na Wakurugenzi ambao kwenye maeneo yao bado kuna wanafunzi wanasomea katika madarasa ya Tembe ama yalioezekwa Nyasi au kujengwa kwa Udongo kuhakikisha wanaacha mara moja kutumia madarsa hayo na kujenga madarasa bora. Waziri Jafo ameyasema hayo wakati akifungua mafunzo ya nne ya Uongozi wa Wakuu wa Wilaya na Wakurugenzi yanayotolewa kupitia ofisi ya Rais Tamisemi kwa kushirikiana na Taasisi ya Uongozi yenye lengo la kujenga uwezo wa viongozi kuweza kutawala kwa ufanisi. “Viongozi wangu nataka Mkakusanye mapato ya ndani kwa nguvu zote na Fedha hizo mzitumie kwenye miradi ya maendeleo na kwa wale ambao mpaka leo wanafunzi wanasomea kwenye mazingira duni hawana madarasa bora watoto wanasomea kwenye madarsa ya Tembe, mengine yameezekwa kwa Nyasi nahitaji muelekeze Nguvu katika ujenzi wa madarasa bora na hayo ya Tembe yotoweke kabisa; M...

HAKI MILIKI NA SHIRIKI NCHI TANZANIA

Image
KATIKA mambo yanayowasumbua watu wengi duniani (Tanzania ikiwemo) ni suala la hakimiliki na hakishiriki kwa wasanii na wabunifu wa sanaa.Hapa nchini, baada ya sheria ya hakimiliki ya mwaka 1966 kuthibitika kwamba ina mapungufu mengi, ndipo mwaka 1999 Bunge la Jamhuri ya Muungano lilipotunga sheria mpya ya hakimiliki na hakishiriki, namba 7 ya mwaka 1999, yenye sura ya 218 ya sheria za Tanzania (kama zilivyorekebishwa mwaka 2002). Kwa mujibu wa utangulizi wa sheria hii, imeletwa kutengeneza na kutoa manufaa zaidi na ulinzi zaidi wa kazi za wasanii wa kazi zinazolindwa na haki miliki na hakishiriki na zingine zote zinazoendana na hizo.Chini ya kifungu cha 2(c) cha sheria hii, ambacho kimsingi kinazungumzia madhumuni ya kutungwa kwa sheria hii ya muhimu kwa maendeleo ya wasanii na watunzi na wabunifu wote katika nyanja za nyimbo, maigizo na tasnia nyingine zinazoendana na hizo.Sheria hii ina madhumuni ya kuinua kazi za fasihi na za kisanii pamoja na nyinginezo zinazofanana na hizo...

ATHARI ZA MAGONJWA YA ZINAA KWA WAJAWAZITO

Image
Magonjwa ya zinaa ni maambukizi yaenezwayo kutoka mtu mmoja hadi mwingine kwa kufanya ngono na mtu mwenye vimelea vya ugonjwa. Aina ya vimelea vinavyohusika kusababisha magonjwa haya ni kama bakteria, virusi na aina nyinginezo za vimelea vya magonjwa. Kuna aina nyingi za magonjwa ya zinaa yanayojulikana, lakini baadhi ya hayo ni kama kisonono,  malengelenge, HIV/AIDS,Pangusa,Chlamydia, HPV ( Human Papilloma Virus ) ,Kaswende,  Trichomuniasis  na mengineyo mengi. Wanawake walio wajawazito waweza kuambukizwa magonjwa ya zinaa sawa na wanawake wasio wajawazito. Magonjwa haya ya zinaa mengi huwa hayaonyeshi dalili mtu anapoambukizwa, kwa hiyo ni vigumu wakati mwingine kwa kina mama wenye mimba kugundua kama wameambukizwa magonjwa haya.Kina mama walio wajawazito ni vyema kuhudhuria kliniki ili wafanyiwe uchunguzi wa magonjwa ya zinaa ikiwepo HIV ambayo husababisha Udhaifu wa Kinga Mwilini.Ni vyema kina mama wajawazito kufahamu madhara ya magonjwa haya kwa...