FONIMU INAVYO WEZA KUVUKA MPAKA WA FONIMU NA KUINGIA KAYIKA FONIMU NYINGINE
FONIMU INAVYOWEZA KUVUKA MPAKA WA FONIMU NA KUINGIA KATIKA FONIMU NYINGINE. Dhana ya fonimu ni dhana ambayo imejadiliwa na wataalamu mbalimbali wakitumia mitazamo tofauti tofauti. Wataalamu wafuatao wameeleza maana ya fonimu:- Massamba, (2004) anasema fonimu ni kipande kidogo kabisa katika mfumo wa sauti za lugha ambacho kina sifa pambanuzi kuweza kukitofautisha na vipande vingine vya aina yake. Sauti pambanuzi katika mfumo wa lugha. Massamba na wenzake, (2004) wanasema fonimu ni kitamkwa kilicho bainifu katika lugha fulani maalumu. Mgullu, akimnukuu Jones, (1975) anaeleza kuwa Fonimu ni kundi la sauti katika lugha fulani, lenye sauti muhimu (phonemes) pamoja na sauti zinazohusiana na ambazo hutumiwa mahali peke katika muktadha maalumu. Tunaweza kusema kuwa wataalamu hawa wametofautiana katika kuelezea dhana nzima ya fonimu, wakati Massamba (2004), anasema fonimu ni kipande kidogo kabisa katika mfumo wa sauti za lugha, Jones (1975) akinukuliwa na Mgullu anasema kuwa fonimu ...