KIPA MPYA ATUA SIMBA

Baada aya hadithi siku kadhaa, hatimaye kipa wa Medeama, Daniel Agyei ametua nchini tayari kumalizana na Simba. Kipa huyo, atasajiliwa na Simba baada ya kocha mkuu wa timu hiyo Mcameroon, Joseph Omog kutoa mapendekezo hayo kwenye ripoti yake aliyoikabidhi hivi karibuni. Agyei ametua jijini Dar es Salaam leo akitokea Ghana kupitia Abu Dhabi.  BAada ya kutua na ndege ya Etihad, Agyei alipokelewa na mratibu wa Simba, Abbas Ally maarufu kama Dizzo. Kuhusiana na kipa huyo, awali Msemaji wa Simba, Haji manara alisema hivi: "Tumeona maswali yamekuwa mengi, hivyo basi nichukue nafasi hii kutangaza kuwa, kesho (leo) Simba tunashusha kipa mpya kutoka Medeama ambaye ni Agyei raia wa Ghana. "Kipa huyo, atakuja kusaini mkataba wa kuichezea Simba, hiyo yote ni katika kuifanyia kazi ripoti ya kocha wetu aliyoitoa kwa uongozi katika usajili huu wa dirisha dogo,"alisema Manara. Kutua kwa kipa huyo, kutafanya idadi ya makipa kuongeza na kuwa wanne ambao ni Manyika Peter Jr, Denis Richard, Angban na Agyei mwenyewe.

Comments

Popular posts from this blog

HIZI HAPA SMS TAMU ZA KUMTAKIA USIKU MWEMA MPENZI WAKO

SMS na MESEJI 900+ za mapenzi

MIAKA 22 SASA TANGU KUZAMA KWA MELI KUBWA YA MV BUKOBA, TANZANI TUMEJIFUNZA NINI?