MWIGULU AKUTANA NA YULE KIUNGO ALIYE SAINI YANGA

 Waziri wa Mambo ya Ndani, Mwigulu Nchemba ambaye ni shabiki wa Yanga wa ‘kugalagala’, amekutana na kiungo mpya wa Yanga, Justice Zulu. Zulu raia wa Zambia, yuko nchini tayari kumalizana na Yanga. Mwigulu ambaye ni straika tegemeo wa Yanga katika timu ya Wabunge ameonekana akiwa picha na Zulu, nje ya hoteli aliyofikia. Zulu anatarajia kumalizana na Yanga, leo au kesho na mara moja ataanza kazi katika harakati za kocha mpya, George Lwandamina kuandaa kikosi chake.

Comments

Popular posts from this blog

HIZI HAPA SMS TAMU ZA KUMTAKIA USIKU MWEMA MPENZI WAKO

SMS na MESEJI 900+ za mapenzi

MIAKA 22 SASA TANGU KUZAMA KWA MELI KUBWA YA MV BUKOBA, TANZANI TUMEJIFUNZA NINI?