Posts

NACTE : TAARIFA KWA UMMA KUHUSU WAHITIMU WA STASHAHADA KATIKA PROGRAMU MBALIMBALI WANAOKUSUDIA KUOMBA KUJIENDELEZA KATIKA NGAZI YA SHAHADA KATIKA VYUO VYA ELIMU YA JUU KWA MWAKA WA MASOMO

Image
+255766605392 TAARIFA KWA UMMA KUHUSU WAHITIMU WA STASHAHADA KATIKA PROGRAMU MBALIMBALI WANAOKUSUDIA KUOMBA KUJIENDELEZA KATIKA NGAZI YA SHAHADA KATIKA VYUO VYA ELIMU YA JUU KWA MWAKA WA MASOMO 2017/2018 Date Posted:  28th June 2017 20:19:27  Posted By: NACTE   BARAZA LA TAIFA LA ELIMU YA UFUNDI (NACTE) TAARIFA KWA UMMA KUHUSU WAHITIMU WA STASHAHADA KATIKA PROGRAMU MBALIMBALI WANAOKUSUDIA KUOMBA KUJIENDELEZA KATIKA NGAZI YA SHAHADA KATIKA VYUO VYA ELIMU YA JUU KWA MWAKA WA MASOMO 2017/2018 Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE) ni chombo kilichoanzishwa kwa Sheria ya Bunge, Sura 129, ili kusimamia na kuratibu utoaji wa mafunzo ya elimu ya ufundi nchini. Jukumu kubwa la Baraza ni kuendeleza na kuinua ubora wa elimu na mafunzo ya ufundi nchini kwa kusimamia kikamilifu shughuli za usajili na ithibati, mitaala na upimaji ili tuzo zitolewazo na vyuo/taasisi ziwe na ubora unaokubalika kitaifa na kimataifa. Kifungu cha 5 (1) (e) na (f) ...

Kibiti: Wawili wauawa kwa kupigwa risasi

Image
Kibiti: Wawili wauawa kwa kupigwa risasi   Kibiti. Watu wawili wameuawa kwa kupigwa risasi katika kijiji cha Mangwi kilichopo Kata ya Mchukwi wilayani Kibiti usiku wa kuamkia leo (Jumatano). Waliouawa wametajwa kuwa ni Mtendaji wa kijiji hicho, Shamte Makawa na mwenyekiti wa Kitongoji cha Mangwi, Maiko Nicholaus. Habari za awali zinaeleza maiti ya mwenyekiti huyo wa kitongoji bado haijaonekana na nyumba zao zimechomwa moto. Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani, Onesmo Lyanga amekiri kutokea kwa mauaji hayo. Amesema polisi wameenda eneo la tukio kwa ajili ya ufuatiliaji na ukaguzi.

TETESI ZA SOKA ULAYA JUMATANO

Image
    TETESI ZA SOKA ULAYA JUMATANO 28.06.2017 Mchakato wa Manchester United kumsajili mshambuliaji wa Real Madrid Alvaro Morata, 24, unasuasua baada ya Real kupandisha dau la mchezaji huyo hadi karibu pauni milioni 80 (Mirror). Morata ambaye ameoa hivi karibuni, amelazimika kuondoka kwenye fungate yake ili kuharakisha uhamisho wake kwenda Old Trafford (AS). Wasiwasi kuhusu hatma ya Cristiano Ronaldo unasababisha kuchelewa kutangazwa kwa uhamisho wa Alvaro Morata kutoka Real Madrid kwenda Manchester United (Diario Gol). Tottenham wapo tayari kumpa mkataba mpya beki wake Toby Alderweireld, 28, ambaye ananyatiwa na Inter Milan (Daily Mirror). Mshambuliaji wa Sunderland Jermain Defoe, 34, amekwama kwa sababu Bournemouth na West Ham zinachelea kumchukua kutokana na gharama kubwa za mchezaji huyo (Daily Star). Mshambuliaji wa Burnley Andre Gray, 26, anataka mkataba mpya wenye mshahara wa pauni 100,000 kwa wiki, lakini klabu hiyo inasema haina u...

PENGO LA NIYONZIMA YANGA LAZIBWA

Image
NA EZEKIEL TENDWA KIUNGO Zimiseleni Moyo anayefukuziwa na Yanga, amemchana Haruna Niyonzima akisema Mnyarwanda huyo asidhani kama ameacha pengo Jangwani kwani anao uwezo wa kufanya mambo makubwa na mashabiki wa timu hiyo kumsahau kabisa fundi wao huyo anayeelezwa kutua Msimbazi. Mido huyo wa Zanaco ya Zambia, yupo mbioni kutua kwa mabingwa hao wa Ligi Kuu Tanzania Bara kwamba mambo yakienda vizuri akamalizana na uongozi, msimu ujao atakuwa katika uzi wa rangi ya kijani na njano. Yanga wapo kwenye mawindo makubwa kwa kiungo huyo ili kuziba pengo la Niyonzima, ambaye amesaini Simba baada ya kushindwana na Wanajangwani hao baada ya kudaiwa kutaka fungu kubwa. Masshele blog ilizungumza na kiungo huyo ambapo alisema mpaka timu hiyo inaamua kumfukuzia, inamaanisha kwamba wameona anao uwezo mkubwa, hivyo kama watafanikiwa kumalizana, wenyewe watafurahi namna atakavyowaburuza wapinzani wake. “Mimi ni mchezaji na popote naweza kucheza, sasa kama ikitokea Yanga wakanisajili na...

KUONDOKA KWA NGOMA KWAMBAKISHA BUSUNGU YANGA

Image
NA WINFRIDA MTOI BAADA ya straika Donald Ngoma kuwa mbioni kutimkia Simba, uongozi wa klabu Yanga umeanza mazungumzo na Malimi Busungu, ili kuangalia uwezekano wa kumbakisha kwenye kikosi chao. Busungu ni miongoni mwa wachezaji wanaomaliza mikataba na Yanga. Mshambuliaji huyo alikuwa kwenye wakati mgumu msimu uliopita, kutokana na kutokuwa chaguo la kocha George Lwandamina, ambaye amekuwa akiwaamini wapachika mabao wake wa kigeni, Obrey Chirwa na Donald Ngoma. Taarifa zilizoifikia masshele Blog  zinadai klabu hiyo huenda ikaachana na mpango wake wa kuwatema baadhi ya wachezaji wake, akiwamo Busungu, baada ya kuwapo kwa taarifa ya Ngoma kutaka kutimkia Simba. “Ujue kwa hali iliyopo Yanga kwa sasa si rahisi kuwaruhusu wachezaji kama Busungu kuondoka na ndiyo maana umeona hata Deusi Kaseke anaongezewa mkataba,” kilisema chanzo hicho. Kwa upande wake Busungu, aliliambia  kila kitu ataweka wazi baada ya mkataba wake kufikia ukingoni Juni 30, kwa kuwa an...

HIKI NI KIKOSI CHA KARNE SIMBA SC

Image
GLORY MLAY NA SELEMANI MAJEMA (DSJ) KIKOSI cha Simba cha msimu ujao kinaweza kuwa cha karne iwapo Wekundu wa Msimbazi hao watafanikiwa kumalizana na nyota kadhaa wanaodaiwa kusainishwa mikataba na timu hiyo. Miongoni mwa nyota hao, yupo kipa mahiri aliyekuwa Azam, Aishi Manula, beki wa kulia, Shomari Kapombe (Azam), kiungo mshambuliaji, Haruna Niyonzima (Yanga), washambuliaji Emmanuel Okwi (SC Villa ya Uganda), John Bocco (Azam) na Donald Ngoma (Yanga). Hakuna asiyefahamu ubora wa nyota hao kutokana na viwango walivyovionyesha misimu kadhaa iliyopita wakiwa na timu zao ambao wakiungana na wale waliopo kikosini Msimbazi, ni wazi timu hiyo itakuwa ni moto wa kuotea mbali. Nyota wa Simba wanaoweza kuungana na wageni na kukifanya kikosi chao kuwa hatari msimu ujao, ni beki wa kushoto, Mohammed Hussein ‘Tshabalala’, mabeki wa kati, Abdi Banda na Jjuuko Murshid, viungo wakabaji, Jonas Mkude na James Kotei, winga Shiza Kichuya na mshambuliaji wa kati, Laudit Mavugo. W...

Maajabu VIDEO Ng'ombe waliotobolewa Tumbo lakini wanaishi

Image
MAAJABU? Ng’ombe katobolewa tumbo lakini bado anatembea (+Video) Kadri siku zinavyoendelea kuhesabika ndio wengine pia tunaendelea kushuhudia vitu vipya au kusikia vitu kwa mara ya kwanza na hii inatokea Morogoro Tanzania ambapo baada ya hivi karibuni kusambaa clip ikionesha ng’ombe waliotobolewa tumbo na bado wanaishi. Video hii ambayo ilizua gumzo huku watu wengi wakiwa wanajiuliza ng’ombe hao wanawezaje kuishi wakiwa na tundu kwenye matumbo? masshele Blog   na  millardayo.com   zimetembelea Chuo Kikuu ch Kilimo Sokoine  SUA ambako ng’ombe hao wanapatikana na kuzungumza na  Siriakusi Faustine ambaye ni Mtafiti na kufafanua zaidi juu ya kilichopelekea kufanya hivyo kwa ng’ombe hao. Siriakusi Faustine  anaanza kwa kusema: >>>”Hawa wanyama ni kwa ajili ya utafiti unaohusiana na vyakula mbalimbali vinavyotumika kwa ajili ya kulisha wanyama aina ya Ng’ombe, Mbuzi na Kondoo. “Hiki ni kitendo kimojawapo kinachofanyika k...