KUONDOKA KWA NGOMA KWAMBAKISHA BUSUNGU YANGA
NA WINFRIDA MTOI
BAADA ya straika Donald Ngoma kuwa mbioni kutimkia Simba, uongozi wa klabu Yanga umeanza mazungumzo na Malimi Busungu, ili kuangalia uwezekano wa kumbakisha kwenye kikosi chao.
Busungu ni miongoni mwa wachezaji wanaomaliza mikataba na Yanga.
Mshambuliaji huyo alikuwa kwenye wakati mgumu msimu uliopita, kutokana na kutokuwa chaguo la kocha George Lwandamina, ambaye amekuwa akiwaamini wapachika mabao wake wa kigeni, Obrey Chirwa na Donald Ngoma.
Taarifa zilizoifikia masshele Blog zinadai klabu hiyo huenda ikaachana na mpango wake wa kuwatema baadhi ya wachezaji wake, akiwamo Busungu, baada ya kuwapo kwa taarifa ya Ngoma kutaka kutimkia Simba.
“Ujue kwa hali iliyopo Yanga kwa sasa si rahisi kuwaruhusu wachezaji kama Busungu kuondoka na ndiyo maana umeona hata Deusi Kaseke anaongezewa mkataba,” kilisema chanzo hicho.
Kwa upande wake Busungu, aliliambia kila kitu ataweka wazi baada ya mkataba wake kufikia ukingoni Juni 30, kwa kuwa anazo ofa kadhaa za timu zinazomhitaji.
Comments
Post a Comment