Maajabu VIDEO Ng'ombe waliotobolewa Tumbo lakini wanaishi

MAAJABU? Ng’ombe katobolewa tumbo lakini bado anatembea (+Video)

Kadri siku zinavyoendelea kuhesabika ndio wengine pia tunaendelea kushuhudia vitu vipya au kusikia vitu kwa mara ya kwanza na hii inatokea Morogoro Tanzania ambapo baada ya hivi karibuni kusambaa clip ikionesha ng’ombe waliotobolewa tumbo na bado wanaishi.
Video hii ambayo ilizua gumzo huku watu wengi wakiwa wanajiuliza ng’ombe hao wanawezaje kuishi wakiwa na tundu kwenye matumbo?
masshele Blog  na millardayo.com zimetembelea Chuo Kikuu ch Kilimo Sokoine SUAambako ng’ombe hao wanapatikana na kuzungumza na Siriakusi Faustineambaye ni Mtafiti na kufafanua zaidi juu ya kilichopelekea kufanya hivyo kwa ng’ombe hao.
Siriakusi Faustine anaanza kwa kusema:>>>”Hawa wanyama ni kwa ajili ya utafiti unaohusiana na vyakula mbalimbali vinavyotumika kwa ajili ya kulisha wanyama aina ya Ng’ombe, Mbuzi na Kondoo.
“Hiki ni kitendo kimojawapo kinachofanyika kutoboa tumbo la mnyama aina ya ng’ombe. Hawa ni ng’ombe dume na wametobolewa upande wa kushoto ambako ndiko kuna tumbo kubwa ambalo linachukuwa sehemu kubwa ya chakula.
“Haya matundu yanatusaidia kuona ndani ya tumbo la mnyama, majani ambayo amekula asubuhi na vyakula vingine alivyokula. Hii ni kwa ajili ya kutafiti kutaka kujua vyakula wanavyokula wanyama vinaweza kusagiga kwa ubora na kumpatia lishe ya kutosha kabla hatujapeleka matokea kwa wafugaji.” – Siriakusi Faustine.
Kwenye VIDEO hii hapa chini kuna kila kitu kuhusiana na Ng’ombe hao na unaweza kuitazama kwa kubonyezaPLAY!!
Share mtu wangu nifollow Instagram kwa kuandika massheleblog

Comments

Popular posts from this blog

HIZI HAPA SMS TAMU ZA KUMTAKIA USIKU MWEMA MPENZI WAKO

SMS na MESEJI 900+ za mapenzi

MIAKA 22 SASA TANGU KUZAMA KWA MELI KUBWA YA MV BUKOBA, TANZANI TUMEJIFUNZA NINI?