Jinsi ya kujibu swali la “wewe ni nani” katika usaili wa kazi
Epuka kuelezea wasifu wako kwani tayari wameshausoma. Elezea mafanikio yako na jinsi unaweza kuwa na mchango utakapoajiriwa. Usisahau kuongelea shauku yako juu ya kazi hiyo. Dar es Salaam. Kama ni mtafuta ajira ambaye umewahi kupata bahati ya kuitwa kwenye usaili, bila shaka swali hili sio geni. Ni swali la “wewe ni nani” ambalo mwajiri anauliza ili kufahamu taaluma, ujuzi na uzoefu wako. Amini ninapokuambia kuwa, wala hahitaji kujua kabila na mkoa uliozaliwa. Anahitaji madini ya kung’amuliwa mchango ambao unaweza kuwa nao kwenye kazi unayoomba. Hivi ndivyo vitu unavyotakiwa kujibu swali hilo: Ongelea ujuzi na mafanikio yanayoendana na kazi unayoomba Ni wazi kuwa hauwezi kufika kwenye swali hili ukiwa haujataja jina lako lakini kama ndiyo swali ulilolipata mara baada ya kuingia mlangoni, ni muhimu ukaanza na utambulisho ambao ni majina yako na elimu yako au cheo. Tovuti ya masuala ya ajira, Resume Now imeeleza kuwa, ni muhimu kueleza historia yako kikazi na mam...