Fursa mpya wazalishaji video fupi YouTube


Dar es SalaamIkiwa wewe ni miongoni mwa watu wanaotengeneza video fupi na kuziweka YouTube, mwaka ujao unaweza kuwa wa kipekee katika maisha yako.
Mtandao huo umeandaa mpango maalum wa kuwazaja pesa mifukoni wazalishaji wa maudhui ya video yanayojulikana kama “shots” yanayowekwa katika mtandao huo.
Kwa mujibu wa blogu ya Youtube watazamaji wa kila mwezi wapatao bilioni 1.5 hutazama zaidi ya video fupi bilioni 30 kila siku, hali hii inaleta ubunifu wa hali ya juu katika kila mada kutoka maeneo yote duniani.
“Kuanzia mwanzoni mwa 2023, watayarishaji wa sasa na wa siku zijazo wa Mpango wa Washirika wa YouTube (YPP) watastahiki ugavi wa mapato ya video fupi ili kupata pesa kutokana na maudhui yao,” amesema Amjad Hanif, Makamu wa Rais wa Bidhaa za Watayarishi, Youtube.
Malipo yatatokana na majumuisho ya mapato ya kila mwezi kutokana na matangazo ambayo huonyeshwa kati ya video fupi  na kusaidia kulipia gharama za leseni ya muziki unaotumiwa kutayarisha video hizo.
Watayarishaji watapata asilimia 45 ya gawio la mapato kulingana na idadi ya watazamaji wa video zao. Mgao wa mapato utabaki sawa, haijalishi kama watatumia muziki au la katika uandaaji.
“Tunatarajia wengi wa wapokeaji wetu wa mapato ya video fupi wapate pesa zaidi chini ya muundo huu mpya, ambao uliundwa kwa uendelevu wa muda mrefu…Ugavi wa mapato kwenye matangazo ya video fupi ni njia nyingine ya watayarishi kuchuma pesa,” amesema Hanif.    

Maboresho ya matumizi ya muziki
Kutokana na watayarishaji wa video kukosa mapato wanapotumia nyimbo zenye hati miliki, Youtube imepanga kujenga daraja kati ya tasnia ya muziki na watayarishi kuboresha jinsi muziki unavyoweza kuingaziwa katika video za watayarishi.
“Tunakuletea Muziki wa Watayarishi, mahali papya katika Studio ya YouTube ambayo huwapa watayarishaji wa YouTube ufikiaji rahisi wa orodha inayoongezeka ya muziki ili kuitumia katika video zao za fomu ndefu.”
“Watayarishaji sasa wanaweza kununua leseni za muziki za ubora wa juu zinazoweza kumudu bei nafuu na zinazowapa uwezo kamili wa kupata mapato, watakuwa na mgao sawa wa mapato ambao kwa kawaida wangefanya kwenye video bila muziki wowote,” imeeleza blogu hiyo.
Watayarishaji ambao hawatataka kununua leseni ya muziki, wataweza kutumia nyimbo na kugawana mapato na msanii wa wimbo wenye haki husika.

Kipengele cha Muziki wa Watayarishaji kinamaanisha ushirikiano mkubwa zaidi wa wasanii na watayarishi, nyimbo mpya zaidi katika orodha za kucheza za watazamaji, na fursa zaidi za wasanii kupitia ushirikishwaji, huku mtandao huo ukiendelea kuweka pesa kwenye mifuko ya watayarishaji.

Comments

Popular posts from this blog

HIZI HAPA SMS TAMU ZA KUMTAKIA USIKU MWEMA MPENZI WAKO

SMS na MESEJI 900+ za mapenzi

MIAKA 22 SASA TANGU KUZAMA KWA MELI KUBWA YA MV BUKOBA, TANZANI TUMEJIFUNZA NINI?