Posts

Showing posts from January, 2020

Chinese Government Scholarship at Shaanxi Normal University in China 2020

Image
c ebook Twitter Pinterest WhatsApp Shaanxi Normal University invites applications for the Chinese Government Scholarship for the 2020/2021 academic year. Chinese Government Scholarship is a full scholarship established by the Ministry of Education in China to support Chinese universities in specific provinces or autonomous regions to enrol outstanding international students for graduate studies in China. Shaanxi Normal University is one of the universities receiving international students under this program. Worth of Award This scholarship is fully funded and it covers the following: Registration fee waiver Tuition waiver Free accommodation on campus Stipend:Master RMB 3000yuan per month; PhD RMB 3500yuan per month Medical insurance:Designated Insurance Company shall undertake the following insurance liabilities during the period of insurance, Death insurance, accidental disability insurance, Medical Insurance for Accidental Inju...

Sababu za kwanini waajiri hawakujibu ukikosa kazi uliyoomba

Image
Sababu kubwa ni kukwepa gharama za kuwajibu watu kwani maombi huwa mengi. Pamoja na hayo, waajiri hufanya hivyo kuwapunguzia waombaji msongo wa mawazo. Baadhi wa wadau washauri walau kutoa mrejesho kwa wale ambao wana makosa madogo ili wajirekebishe wanapoomba sehemu zingine. Dar es Salaam.  Hapana! Siyo kwamba una bahati mbaya ya unasahaulika mara zote unaposhindwa kupata majibu baada ya kutuma maombi ya kazi kama hujafanikiwa kuchaguliwa katika kazi husika. Huenda hali hiyo imekuacha na maswali mengi yasiyokuwa na majibu na wakati mwingine umefikia hatua ya kuona ni jambo la kawaida kutokupewa sababu za kutochaguliwa katika kazi husika uliyoomba kutoka waajiri.   Zipo sababu mbalimbali ambazo zinawasukuma waajiri wengi kutokutoa mrejesho kwa kila mwombaji wa kazi ambaye hajafanikiwa kuitwa katika interview ili kuwasaidia kujirekebisha katika maeneo waliyofanya makosa.  Mtandao huu umefanikiwa kuzungumza na wadau mbalimbali wa ajira nchini ambao wameel...

UCHAPISHAJI NA UCHAPAJI BINAFSI , SELF PUBLISHING

JINSI YA KUFANYA UCHAPISHAJI BINAFSI (SELF PULBISHING) UTANGULIZI Ni ndoto ya watu wengi sana kuchapisha vitabu vyao na kuwafikia hadhira husika. Ila tafiti zinaonesha kuwa ndoto hizi hufutwa na changamoto mbali mbali zinazo wakumba waandishi, ikiwemo ya gharama za uchapishaji pamoja na urasimu uliopo katika makampuni ya uchapishaji. Yaani mchapishaji anafaidi sana kuliko msaani aliyeumiza kichwa chake na kuandika kazi husika. Kama huamini hilo waulize waandishi wengi wakongwe ambao vitabu vyao tumevitumia hadi mashuleni na vingine bado vinaendelea kutumika. Wengi wamekuwa na majina makubwa na wanafahamika sana sana ila hawajafaidi jasho lao. Mfano unakuta publisher analipwa Milioni 200 ila mwandishi anapata milioni mbili. Au laki saba hivi. Kwa kulitambua hilo makampuni mengi yakaleta njia sahihi kwa kila mwandishi (Haijalishi ni mkubwa au mdogo) ili aweze kuchapisha kitabu chake pasipo kutumia GHARAMA yeyote, na kujiingizia kipato kikubwa sana mara kumi zaidi ya kupeleka kwa Publish...

MAENDELEO YA TEHAMA NI AHUENI KWA WAANDISHI KATIKA KARNE YA 21

Image
Teknolojia ya habari na mawasiliano (TEHAMA) Imechangia pakubwa katika kukua kwa sekta nyinginezo duniani.  Nyenzo kuu ya TEHAMA ni kompyuta ambayo huwezesha kuchakata, kukusanya, kuchambua na kutoa taarifa.  Kupitia vifaa mbalimbali vya tehama kama vile, kompyuta, simu n.k mtumiaji huweza kufikia intanet.  Internet ni mfumo wa kompyuta ambao huunganisha kompyuta zote duniani kupitia kiungo cha webu(www) ili mtu aweze kutembelea mtandao nilazima apitie kiungo/link . Maendeleo ya TEHAMA na Mapinduzi mkubwa katika tasnia ya uandishi. Kupita tehama mwandishi huweza 1. Kuandika mswada, kufanya utafiti Huu ya wazo lake, 2. Kutafuta kampuni ya uchapishaji 3. Kuhariri mswada 4. Kuchapa 5. Kutafuta solo 6. Kuuza Haya hutokana na muunganiko wa tehama na vifaa vyake, bapo kabla ya ujio na maendeleo ya tehama haya yasingeweza kufanyika.

IDARA YA UHARIRI KATIKA KAMPUNI YA UCHAPISHAJI

Image
Idara ya uhariri ni idara nyeti sana katika katika kampuni ya uchapaji. Mhariri analo jukumu kubwa kwa mwandishi na kwa kampuni yake ya uchapaji. Mhariri ndiye anayehusika na kuhakikisha mswada Unakuwa Kitabu kwa namna inayofaa kwa kushirikiana na mwandishi. Kazi kubwa ya mhariri katika mswada ni kunyoosha lugha na kuhaikisha mawazo hayapingani. Mhariri pia analo jukumu la kumshauri mwandishi kuhusu mswada wake. Pia mahariri anayo majukumu kadhaa katika kampuni ya uchapishaji ikiwemo, kutafuta mswada, kupokea mswada, kupanga bajeti ya uchapaji, kutafiti soko na majukumu mengineo.  Kama mhariri hasa mhariri wa matini hata kuwa makini kazi iliypchapwa huweza kutoka na makosa mengi , ambayo huweza kuishushia hadhi kampuni ya uchapaji. Hivyo mhariri hana budi kuwa makini na kazi yake. Pamoja na hayo wapo waandishi ambao huchapa kazi zao wenyewe Bila kupita katika mikono ya kampuni ya uchapaji ambako ndipo idara ya uhariri ilipo, hii ni kutoka na na maendeleo ya sayansi na teknol...

Mbinu zitakazowasaidia wahitimu wa vyuo vikuu ‘kutoboa’ soko la ajira

Image
Wanahimizwa kutatmnini soko linataka nini kwa wakati huu. Kutengeneza mtandao na kujitolea katika shughuli mbalimbali kunaweza kuwatoa kimaisha.  Serikali, wadau wakumbushwa kuimarisha programu za maendeleo ya nguvukazi kwa vijana.  Dar es Salaam.  Ni ndoto ya kila muhitimu wa elimu ya juu, kuajiriwa au kujiajiri ili kutumia taaluma na kipaji chake kuwa sehemu ya kuchangia maendeleo ya jamii na kupata kipato cha kuboresha maisha yake.  Lakini ndoto hizo huyeyuka baada ya wahitimu kuingia mtaani na kujikuta waliyotarajia kuyapata hayapo, jambo linalowaweka katika utata wa kuzikabili changamoto za ajira na kujenga mustakabali mzuri wa maisha ya baadaye. Hata hivyo, vijana waliopo vyuoni na wale ambao wamehitimu miaka ya hivi karibuni, bado wana nafasi kubwa ya kufanikiwa katika ajira za kuajiriwa au kujiajiri wenyewe.  Yapo mambo mengi yanayoweza kuwasaidia vijana hasa waliopo vyuoni kufanikiwa mara baada ya kutoka vyuoni. Usisubiri umalize mas...

Ni kwa vipi utendaji katika fasihi simulizi huchukuliwa kuwa ndio uti wa mgongo wa fasihi simulizi

Utendaji na fasihi simuli, Swali: jibu Swali hili kwa mfumo wa makala kisha utume majibu yako katika barua pepe info.masshele@gmail.com Makala hii itakusaidi kujibu >>>> https://masshele.blogspot.com/2018/01/utendaji-ni-uti-wamgongo-wa-fasihi.html?m=1

PICHA: MAFUNZO YA TAASISI YA HELPTOHELP YAFANA

Image
Wadau wakifuatilia kwa makini mafunzo ya kompyuta ya helptohelp na kufanya kwa vitendo. Na mwandishi wetu, Dar es salaam, Leo january 26 ilikuwa siku ya mwisho ya programu yamafunzo iliyoendeshwa kwa siku mbili mfululizo katika chuo kikuu cha Kampala tawi la Dar es salaam, mafunzo hayo yalilenga zaidi kufundisha stadi za kompyuta pamoja na mijadala kuhusu masuala ya usawa wa kijinsia. Aidha warsha hiyo ya siku mbili iliwakutanisha wadau mbalimbali zaidi ya 60 ambapo wamenufaika kwa kupata ujuzi mbalimbali wa masuala ya TEHAMA , pamoja na masuala ya kijinsia.  Baada ya mafunzo hayo wadau mbalimbali waliohudhuria ambapo wengi ni Wahitimu pamoja na wanafunzi wa vyuo mbalimbali vya Dar es salaam walikiri kunufaika na mafunzo hayo. Miongoni mwa malengo muhimu ya taasisi isiyo ya kiserikali ya Help to help ni pamoja na kuwaelimisha watu wanaoweza kuielimisha jamii pia na kuleta fikra chanya na mabadiliko katika jamii. Pia taasisi hii inatoa fursa za ufadhili wa kimasomo ndani ...