IDARA YA UHARIRI KATIKA KAMPUNI YA UCHAPISHAJI



Idara ya uhariri ni idara nyeti sana katika katika kampuni ya uchapaji. Mhariri analo jukumu kubwa kwa mwandishi na kwa kampuni yake ya uchapaji. Mhariri ndiye anayehusika na kuhakikisha mswada Unakuwa Kitabu kwa namna inayofaa kwa kushirikiana na mwandishi. Kazi kubwa ya mhariri katika mswada ni kunyoosha lugha na kuhaikisha mawazo hayapingani. Mhariri pia analo jukumu la kumshauri mwandishi kuhusu mswada wake. Pia mahariri anayo majukumu kadhaa katika kampuni ya uchapishaji ikiwemo, kutafuta mswada, kupokea mswada, kupanga bajeti ya uchapaji, kutafiti soko na majukumu mengineo.  Kama mhariri hasa mhariri wa matini hata kuwa makini kazi iliypchapwa huweza kutoka na makosa mengi , ambayo huweza kuishushia hadhi kampuni ya uchapaji. Hivyo mhariri hana budi kuwa makini na kazi yake.

Pamoja na hayo wapo waandishi ambao huchapa kazi zao wenyewe Bila kupita katika mikono ya kampuni ya uchapaji ambako ndipo idara ya uhariri ilipo, hii ni kutoka na na maendeleo ya sayansi na teknolojia ambayo kwa kiasi kikubwa yamepunguza majukumu ya mhariri na majukumu ya kampuni ya uchapaji kwani mwandishi huweza kujichapia kazi yake mwenyewe.

Hata hivyo sio vyema sana kwani kazi iliyochapwa Bila kupita katika mikono ya mhariri huweza kuwa na makosa lukuki. 

Comments

Popular posts from this blog

HIZI HAPA SMS TAMU ZA KUMTAKIA USIKU MWEMA MPENZI WAKO

SMS na MESEJI 900+ za mapenzi

MIAKA 22 SASA TANGU KUZAMA KWA MELI KUBWA YA MV BUKOBA, TANZANI TUMEJIFUNZA NINI?