PICHA: MAFUNZO YA TAASISI YA HELPTOHELP YAFANA


Wadau wakifuatilia kwa makini mafunzo ya kompyuta ya helptohelp na kufanya kwa vitendo.


Na mwandishi wetu,
Dar es salaam, Leo january 26 ilikuwa siku ya mwisho ya programu yamafunzo iliyoendeshwa kwa siku mbili mfululizo katika chuo kikuu cha Kampala tawi la Dar es salaam, mafunzo hayo yalilenga zaidi kufundisha stadi za kompyuta pamoja na mijadala kuhusu masuala ya usawa wa kijinsia. Aidha warsha hiyo ya siku mbili iliwakutanisha wadau mbalimbali zaidi ya 60 ambapo wamenufaika kwa kupata ujuzi mbalimbali wa masuala ya TEHAMA , pamoja na masuala ya kijinsia.  Baada ya mafunzo hayo wadau mbalimbali waliohudhuria ambapo wengi ni Wahitimu pamoja na wanafunzi wa vyuo mbalimbali vya Dar es salaam walikiri kunufaika na mafunzo hayo.

Miongoni mwa malengo muhimu ya taasisi isiyo ya kiserikali ya Help to help ni pamoja na kuwaelimisha watu wanaoweza kuielimisha jamii pia na kuleta fikra chanya na mabadiliko katika jamii. Pia taasisi hii inatoa fursa za ufadhili wa kimasomo ndani ya nchi kwa wahitaji wanaokidhi vigezo (tembelea katika tovuti yao) >>>https://helptohelp.se/our-mission

Mdau akiendelea kujifunza huku mwongozaji akifuatilia kwa makini na kutoa maelekezo kwa karibu.

Wadau wakimsikiliza kwa makini mkufunzi.

Mfundishaji wa masuala ya Tehama akifundisha huku wadau wakimsikiliza kwa makini.

Picha zaidi





















































Mwisho, unaweza kuwa follow help to help katika mtandao ya kijamii ili usipitwe na tukio lolote linaloandaliwa na taasisi hii, pia tembelea katika tovuti yao kwaajili ya kupata masomo mbalimbali na kuielewa taasisi hii kiundani >>>https://helptohelp.se/

Comments

Popular posts from this blog

HIZI HAPA SMS TAMU ZA KUMTAKIA USIKU MWEMA MPENZI WAKO

SMS na MESEJI 900+ za mapenzi

MIAKA 22 SASA TANGU KUZAMA KWA MELI KUBWA YA MV BUKOBA, TANZANI TUMEJIFUNZA NINI?