Vyakula vinavyoongoza kwa kuongeza akili kwenye ubongo

Katika mwili wa mwanadamu hakuna kitu chenye umuhimu mkubwa kama ubongo, ubongo ndio ambao humsaidia mwanadamu katika kufanya mambo mbalimbali, hata hivyo inaelezwa ya kwamba ubongo wa mwanadamu ndio humfanya mwanadamu kuonekana hivyo alivyo. Hivyo inaelezwa ya kwamba ili mwanadamu aweze kuongeza akili, katika kufikiri na kutenda mambo mbalimbali anatakiwa kula vyakula vifuatavyo: 1. Mafuta ya samaki. Mafuta ya samaki ni muhimu kwa ubongo na mfumo wa fahamu. Ulaji wa samaki wenye minofu kama sangara na dagaa, utaweza kupata faida hizo kwa sababu aina hii ya samaki ina kiasi kingi cha mafuta ya Omega 3 ambayo huimarisha utendaji kazi na mawasiliano kati ya ubongo na seli za mwili moja kwa moja. 2. Ulaji wa mbegu za maboga. Mbegu za maboga zina kiwango kingi cha madini ya ‘Zinc’ ambayo husadia kuongeza kumbukumbu (memory). Kuna njia nyingi za kula mbegu za maboga, moja wapo ni kuzikaanga na kula kama karanga, ukila kiasi cha kiganja kimoja kwa siku, huweza kusaidia kuweza kuon...