Man United kuikabili Man City bila Pogba, bila Zlatan, bila Rojo.

Man United kuikabili Man City bila Pogba, bila Zlatan, bila Rojo.

Sahau kuhusu majeraha ya Smalling na Phill Jones waliyoyapata wakati wa kambi ya timu ya taifa ya Uingereza lakini majeruhi ndani ya United wanazidi kumiminika.

Tayari Zlatan Ibrahimovich yuko nchini Marekani kwa ajili ya upasuaji baada ya kuumia katika mchezo wa ligi ya Europa dhidi ya klabu ya Ubelgiji ya Anderlchelt.

Marcos Rojo naye aliumia katika mchezo huo wa Europa lakini kuna jipya, Paul Pogba hatakuwepo katika mchezo mkubwa kwa Manchester dhidi ya majirani zao City.

Taarifa kutoka ndani ya klabu hiyo zinasema majeruhi aliyopata Pogba katika mchezo wa ligi kuu dhidi ya Burnley utamfanya asiwepo katika Manchester Derby.

Jose Mourinho amesema kutokuwepo kwa Pogba hakuwaumizi sana na wanaamini atarudi siku nyingine na kwa sababu hayupo inabidi wapambane na walichonacho.

Mechi kati ya United na City ni ngumu sana na inavuta hisia za wengi lakini pia klabu hizo mbili zinapigana vikumbo kuingia top four ya ligi na hii inaufanya mchezo huo kuwa mgumu zaidi

Comments

Popular posts from this blog

HIZI HAPA SMS TAMU ZA KUMTAKIA USIKU MWEMA MPENZI WAKO

SMS na MESEJI 900+ za mapenzi

MIAKA 22 SASA TANGU KUZAMA KWA MELI KUBWA YA MV BUKOBA, TANZANI TUMEJIFUNZA NINI?