Mbinu za ukalimani
Mjadala kuhusu mbinu za ukalimani. Ukalimani fululizi Ukalimani fuatizi Ukalimani nong’onezi Ukalimani changamani Ukalimani pokezi Ukalimani tazamishi MBINU ZA UKALIMANI Utangulizi Insha hii imegawanyika katika sehemu kuu nne ambazo ni; utangulizi, kiini, hitimisho na marejeleo. Sehemu ya utangulizi ni maelezo kuhusiana na mgawanyiko wa insha hii pamoja na fasili ya ukalimani, sehemu ya kiini ni mbinu za ukalimani, sehemu ya hitimisho ni mawazo ya jumla kuhusiana na insha kisha vyanzo mbalimbali vilivyotumika kusheheneza insha hii, vimewekwa katika sehemu ya marejeleo. Dhana ya Ukalimani Wanjala (2011:14) anaeleza kuwa ukalimani ni kitendo cha kuhawilisha ujumbe katika mazungumzo kutoka lugha chasili hadi lugha lengwa. Katika fasili hii, jambo la muhimu linalodokezwa ni kwamba, ukalimani unahusu uhawilishaji wa lugha ambayo ipo katika mazungumzo. Hata hivyo, kwa maoni yetu, kutokana na maendeleo ya sayansi na teknolojia fasili ya ukalimani inapevuka n...