KUKOJOA KITANDANI/NOCTURNAL ENURESIS

Kukojoa kitandani ni moja ya matatizo yanayowakumba watoto wengi ambao wamefikia umri wa kuweza kudhibiti haja ndogo. Tatizo hili pia liko miongoni mwa watu wazima wachache. Kukojoa kitandani ni moja kati ya mambo ambayo yanaweza kumfanya mtoto asifanye vizuri kimasomo na kukosa kujiamini mbele ya wenzake. Kwa wazazi wenye watoto wenye tatizo hili ambao umri wao ni chini ya miaka saba wasiumize kichwa kwani watoto wanakuwa bado wanajifunza kudhibiti haja ndogo. Kukojoa kitandani kunawapata sana watoto wa kiume kuliko wa kike. Kwa watu wazima tatizo la kukojoa kitandani linasababisha matatizo kwenye jamii ikiwemo wachumba kuachana na baadhi ya ndoa kuvunjika kwa ajili ya kukosa uvumilivu na uelewa kuwa tatizo hili si makusudi ya muhusika na kuwa anahitaji kutiwa moyo na kusaidiwa. Kama tatizo litaendelea baada ya miaka saba basi mzazi anaweza kuanza kutafuta tiba ya tatizo. Tiba ni pamoja na kubadili mfumo wa maisha, kumfundisha mtoto namna ya kudhibiti haja ndog...