MOTIFU YA SAFARI ,
MOTIFU YA SAFARI By Glory mushy MOTIFU YA SAFARI NA MSAKO KAMA MWEGA MKUU WA DHAMIRA KATIKA “MARIMBA YA MAJALIWA” “Marimba ya Majaliwa ni hadithi iloyoandikwa na Edwini Semzaba mwaka (2008) ambayo inaelezea kuhusiana na marimba ya Majaliwa iliyopotea. Mwandishi ameonyesha jinsi Majaliwa alivyokuwa anatafuta marimba yake mpaka akaipata. Majaliwa alisafiri kwa kutumia njia mbalimbali kama vile ungo, fagio, na maumbo ya samaki akizunguka Tanzania nzima akisaka marimba ya nyuzi ishirini (20). Alianza Mafia, akaenda Zanzibar, Tanga, Moshi na Arusha, Iringa, Mwanza, Kigoma, na miji mingine mingi. Na Kongoti bingwa wa Taifa wa Marimba akimchenga kila mara huku akinga’nga’nia Marimba ya Majaliwa ili amzuie kushinda na ashinde yeye na bila Marimba yenye nyuzi ishirini (20) hakuna ushindi. Katika mada hii tutaanza kuelezea maana ya fasihi, fasihi ya watoto, na maana ya motifu, na maaana ya dhamira. Kisha katika kiini cha swali letu tutachambua motifu mbalimbali...