KITENDO CHA KUFUKUZWA KWA MWANAFUNZI HUYU WA CHUO KIKUU CHA DAR ES SALAAM CHAENDELEA KULAANIWA KILA KONA
Alphonce Lusako kwaheri mpambanaji. Ulifukuzwa mwaka 2011 ukiwa mwaka wa 3, Kwa kutambua umuhimu wa elimu ukaamua kurudi chuo kuendelea na masomo yako kwa kuanza mwaka wa kwanza sheria 2016, lakini leo baada ya kutoka kwenye mtihani umekutana na barua ikikutaka uondoke chuo haraka kwa sababu kuwa ulisajiliwa kimakosa. Inauma sana lakini ndio gharama halisi ya harakati za kujitoa kwajili ya wengine. ALUTA CONTINUA

BY Malisa GJ
Nimesikitika kupata habari za Ndugu.Alphonce Lusako mwanafunzi wa UDSM aliyefukuzwa mara mbili chuoni hapo. Mwaka 2011 akiwa mwaka wa 3, (ambao ni mwaka wa mwisho wa masomo) alifukuzwa chuoni hapo kwa madai ya kuchochea mgomo. Kwa maelezo niliyopata ni kuwa hoja zake zilikua mbili. Mosi TCU inadahili wanafunzi hewa, pili Bodu ya mikopo inafanya ubadhirifu wa pesa za wanafunzi. Madai haya yakaonekana ni uchochezi na akafukuzwa chuo akiwa mwaka wa mwisho.
Akakaa mtaani miaka 6, bila kupewa barua ya kumuita tena chuoni. Mwaka jana akaamua kuomba tena nafasi ya kusoma kupitia TCU, wakampanga tena UDSM, kozi ya sheria. Akaamua kuanza mwaka wa kwanza. Sasa amesoma semester moja hatimaye jana akitoka kwenye chumba cha mtihani akapewa barua ya kufukuzwa tena chuoni. Sio kwamba amefanya kosa ila UDSM wamefukua makaburi ya mwaka 2011. Wamemfukuza tena wakidai walimdahili kimakosa alipoomba nafasi mara ya pili.
#MyTake:
1. Je UDSM walimfungia Lusako kusoma chuoni hapo milele?
2. Kwanini UDSM hawakumkataa alipoomba admission mara ya pili, badala yake wamemdahili na kusubiri apoteze muda kusoma semester moja ndio wamfukuze?
3. Hoja za Lusako kuhusu TCU na HESLB, zinafanana na hoja za Rais JPM kuhusu taasisi hizo. JPM amesema TCU ilikua ikidahili wanafunzi wasio na sifa na Bodi ilikua ikitoa mikopo kwa wanafunzi hewa. Hali hii ilipelekea JPM kufanya mabadiliko ya management kwenye taasisi hizo. Sasa ikiwa ndivyo, kwanini Lusako aendelee kuonekana na hatia?
Anyway, binafsi nimejisikia vby kuona taasisi za elimu zinatumia nguvu kubwa kulazimisha watu kuwa wajinga badala ya kupunguza ujinga. Taasisi za elimu zinapaswa kuwa na mazingira rafiki kwa kila mtu mwenye sifa na uwezo wa kusoma aweze kusoma.
Kama ni adhabu Lusako ameshatumikia vya kutosha. Kwanza kupoteza degree yake aliyokua amalize mwaka 2011 ni adhabu kali sana maana miaka yote mitatu alifanya kazi bure. Pili kukaa mtaani miaka 6 kwa kukosa fursa ya kusoma ni adhabu kubwa zaidi. Adhabu hizi mbili zilimtosha kabisa Lusako na kama ni kujifunza ameshajifunza vya kutosha.
Kwahiyo sioni kama kulikua na sababu ya kumfukuza tena mtu wa aina hii. Labda kama UDSM walidhamiria kumkomoa. Lakini kama ni adhabu iliyolenga kumfundisha nina hakika Lusako amejifunza vya kutosha, na UDSM haikua na sababu ya kumfukuza tena mara ya pili.
Tujenge taasisi za elimu zenye mazingira rafiki kwa wote. Zilenge kutatua changamoto za jamii, sio kuongeza changamoto kwa jamii. Nina imani Management ya UDSM ina fursa ya kupitia upya maamuzi yake kuhusu hatma ya kijana huyu na ikafanya maamuzi ya busara zaidi kuliko haya. Pole sana Lusako.!!

By Tito Daudi Lyanga
This is more than sheet to be torelated!
Narudia tena! Huu ni zaidi ya upuuzi unaoweza kuvumiliwa!
Haiwezekani katika taifa hilihili wawepo miungu watu wa kuamua hatma za maisha ya watanzania wengine na wakaachwa waendelee kumea na kutekeleza maamuzi yao ovu kila wakati wanapoamua wao.
Wakaachwa waendelee kupoteza muda na nyakati za yeyote wanayemuamulia,
Wakaachwa waendelee kupoteza rasilimali za yeyote Yule wanayemualia kwa wakati wanaoutaka wao.
Wakaachwa watekeleze umungu wao katika hatma za maisha ya wengine kwa visingizio mfu vya kulinda kanuni, taratibu, na sheria za taasisi husika ama za nchi. Kuacha miungu ya Aina hii inayoweza kujipa majukumu ya kufifisha malengo ya watu, ndoto za watu iendelee kutekeleza malengo yake ni kufuga maadui katika Taifa, Ni kufuga ujinga ambao hauna sababu katika Taifa hili.
Kaka yangu Alphonce Lusako natambua ugumu wa ngozi yako na nimaombi yangu uzidi kuwa na ujasiri wa kuyakabili haya.
Lakini ni matumaini yangu pia Kama Taifa. Haya si mapambano ya wanafunzi wa vyuo vikuu tu, si ya wafanyabiashara tu, Si ya wanasiasa tu. Kulinda haki ya mtaifa mwenzetu yeyote Yule ni jukumu la kila mmoja wetu. Tafakuri zinazoendana na matendo zinahitaji kulinusuru Taifa na maamuzi kandamizi Kama haya.
Mwisho.
Ni imani yangu kesho tarehe 31/1/2017, Mapema Sana natarajia kuona waliofanya hiyo iliyoitwa #Irregularadmission# (Kisingizio mfu) wakiwajibika ama kuwajibishwa ipasavyo.
Alammsik!

By Kabenga Yisega Jangala
ALPHONCE LUSAKO IPO SIKU YAKO TU
nimesikitishwa na kuvunjwa moyo juu ya taarifa za kutenguliwa kwa usajili wa mwanaharakati huyu ktk chuo kikuu cha dare salaam(UDSM) kwa kile kilichotajwa kama usajili wa kimakosa! kamanda huyu inasemekana amepewa barua wkt akitoka kwenye mtihan wke wa kumaliza semister ya kwanza
kamanda huyu ni mmoja wa wanaharakati walikuwa mstari wa mbele kupgania haki za wtoto wa walalahoi na hatimaye kufukuzwa 2011,pmoja na hilo kumekuwa na figusu nyng za kuhakikixha hawarud chuon! ingawa sijajua bdo sbbu za chuo kufikia uamuzi huo kuna maswali ya kujiuliza
1.ilikuwaje akadahiliwa na tcu na hatimaye udsm kama bdo alikuwa na kasoro?
2.ilikuwaje akasajiliwa na kuruhusiwa kulipa gharama zote bila kuambiwa?
3.ilikuwaje akae semister nzima kama kuna makosa ktk usajili wake?
4.ilikuwajd akaruhusiwa kubadilisha koz kwenda koz ya sheria ambayo hakuchaguliwa hpo awal?
any way ipo siku yko mkuu daima nimezidi kujifunza kutoka kwko# Alphonce Lusako(emekha)
By Oscar Kimaro
Naifahamu adha ya kufukuzwa au kusimamishwa chuo kwa kutetea maslahi ya walio wengi. Pole Alphonce Lusako
By Anthon Mwangake
POLE COMRADE
Mwaka 2010 nilipojiunga na chuo kikuu cha Dar es salaam , kampasi kuu maarufu kama "MLIMANI" Nilipata fursa ya kukutana, kufahamiana na kujenga URAFIKI na MARAFIKI wenye ndoto RAFIKI nami......
Alphonce Lusako si tu kwamba alikuwa mwanamapambano mwenzangu bali alikuwa na aina ya maisha ambayo nilitamani kuyaishi pia
Alphonce Lusako ni kati ya watu walionishauri juu ya uamuazi wangu juu ya ama niendelee kuandika makala kupitia kijarida maarufu kama "MLIMANLEO" au la!
Mambo makuu matatu ambayo mimi na Lusako tumepitia
1.Sote tulipata kupitia CHASO , wakati fulani mimi nilikuwa kwenye kikosi kazi maalumu baada ya uongozi uliokuwepo kuondoka enzi hizi tukiwa na ndugu yangu Hatari Chacha, Andrew G. Kadege ,Mwalusanya Wilfred Aswile Legan
2.Sote tulishiriki kuasisi Rungwe Natives University Students Association (RUNUSA)
3.Sote tulipigwa mabomu ya machozi wakati wa kudai ongezeko la pesa ya kujikimu
IKUMBUKWE KUWA Mnamo mwaka 2011 Alphonce Lusako ni kati ya rafiki zangu wa karibu waliosimamishwa masomo na kutishiwa kutodahiliwa tena ndani ya vyuo vikuu vya Tanzania ...
Baada ya kukaa uraiani miaka kadhaa , rafiki yangu aliweza kupata nafasi nyingine ya kusoma chuo hicho kwa udahiri wa kitivo cha sheria
Jana nimepata taarifa kuwa udahiri huo umefutwa na leo nikampigia simu amekili hilo swala kutokea
"Never underestimate the power within you"
-OBEY IT, FOR GOD DECIDED TO GIVE YOU-
"Every human came to the health with something humanity needs"
-SHARE IT-
"There is a room for everyone at the top"
-ONE DAY YES-
"Never follow and Live for what you are not willing to die for"
-LIVE YOUR DREAM -
"The value of all creation is in its contribution to others"
-KEEP IT UP-
"The greatness is measured by how much of yourself you lose in service to the others"
-GOD WILL DIRECT AND CROWN YOU-
By Mwl Razaq Mtele Malil
Nimesikitishwa sana juu ya taarifa ya kutenguliwa kwa usajiri wake kaka yangu, rafiki yangu na kiongozi wangu Alphonce Lusako katika chuo kikuu cha Dar Es Salaam.
Ikumbukwe Lusako alifukuzwa Chuo hapa UDSM 2011 katika harakati za kupinga ufisadi uliokuwa unafanyika TCU na HESLB ambapo baada ya kuingia Rais Magufuli ilibainika ni kweli Taasisi hizo za UMMA zilikuwa zikijihusisha na ufisadi mkubwa ikiwemo mikopo hewa na kubainika kuwa wanafunzi hewa na TCU kudaili wanavyuo wasio na vigezo.
Kwa kutambua umuhimu wa elimu ndugu Lusako akaomba upya kusoma sheria UDSM na akachaguliwa na kusajiriwa lakini leo akitokea kwenye mtihani wa kumaliza semesta ya kwanza ndugu Lusako anapewa barua ya kutenguliwa usajiri wake katika chuo hiki.
Imeniuma sana kupata taarifa hii na kujiuliza kwa nini chuo kilimsajiri na kumuacha akilipa gharama ikiwemo ada na vinginevyo huku wakijua sheria za chuo haziruhusu.
Ndugu yangu Lusako nakuomba cool down mungu ana mipango yake hizi ni changamoto za dunia japo natambua ulikuwa na malengo makubwa sana ila still kama ipo ipo hakuna binadamu wa kuzui riziki ya mtu.

BY Gibson Johnson Eliaform Mdakama
Not Yet Uhuru.
Bado naitafakari siku ya jana. Ila mkuu wangu mpambanaji mwenzangu bado taifa linatuhitaji. Never give up.
Mawimbi ya baharini hayachagui aina ya mvuvi lakini changamoto mara kwa mara humkumba mpambanaji. Kumbuka hatua ya changamoto hiyo ni maono ya hatua ijayo na hutathimini juhudi za malengo yako kuona ni nani hapendi hatua hiyo na kwa kiwango gani ulichotarajia, si kila TIMU inaruhusu sifa zozote za mchezaji bali kigezo kilichowekwa kifuatwe ili kukidhi mahitaji ya kocha, basi unapoona timu hiyo huendani nayo hunabudi kijiunga na timu inayoruhusu kiwango chako.
BY Emanuel Didas
Pole sana Bro Alphonce Lusako Kwa mateso yote haya. Kufukuzwa Chuo Mara mbili Kwa Sababu ya kutetea haki ya waliowengi sio kitu ambacho watu tulio wengi tunaweza shindana nacho, *Ila kumbuka Wewe ni kiongozi bora ajaye (Hata Sasa UPO);* Na utapaswa kutenda HAKI kwa watu wote hata Kama watoto Na wajukuu wawaliozuia HAKI Yako Leo watakuwa mstari wa mbele kudai haki hiyo.
#Nb; Pamoja Na kujua kuwa mambo Kama haya yanaweza kuwa njia ya KUPATA ukomavu Na uvumilivu; tunapaswa kubadilisha sheria Na taratibu kandamizi katika Sekta ya Elimu ili kuweka Usawa katika vyuo vya Umma Na Binafsi katika Taifa LETU.
Mpende Jirani Yako Kama Nafsi Yako🇹🇿
By Confitemin Kashaija
Safari ya ukombozi kwa mtu binafsi na jamii ya wanaopewa cheo cha unyonge wakafrahi si nyepesi hata kidogo. Inakuwa ngumu zaidi pale wale wanaojitoa kuwatetea wanapominywa mbavu kutokea kila upande, watetezi hawa watanyimwa fursa na haki zao kikatiba kama wanadamu. Miungu watu wanajivua ubinadam na kusahau kuwa kwa kawaida wapumuapo pumzi yao yaelekea chini pengine kuzimu wakisubiriwa wao kuifata kama sote tutakavyofanya. Mabwana hao tuwaache maana mwisho wao ushapangwa na aliyewaumba.
Kwa maskitiko makubwa nmepokea taarifa za kufutiwa udahili chuo kikuu UDSM rafiki yangu comred ALPHONCE LUSAKO mwanafunzi wa mwaka wa kwanza( BA,LAWS) eti kwa vile aliwahi kufukuzwa mwaka 2011 chuon hapo. Yapo mengi ya kujiuliza ila machache ni kama yafatayo, Mifumo ya udahili ni dhaifu kias gan mpaka apate udahili TCU na apite kwenye vetting ya chuo hadi apate registration no? ktk hilo nani anapaswa kuwajibika kama si vyombo vya udahili badala ya mdahiliwa? Je sheria hiyo ilotumika kumfutia udahili iliambatanishwa ktk barua yake ya november 2011 kama masharti ambata ya kufukuzwa kwake? Je, ipo ktk university charter?
hata hivo, naamini comred Lusako bado yuko imara kama ilivyo ada yetu tokea 2011. Nakumbuka msemo mmoja tuliutumia sana wakati huo REVOLUTION SQUARE, "Kama ipo ipo na si lazima UDSM" Mifano ipo mingi. Rafiki yako Kashaija kahitim UDOM, Ndunguru kahitim mzumbe, Mwambapa Makerere UGANDA, Aaliyekuwa mwalishi wa conas yupo Algeria anamalizia shahada ya udaktar na wengine wengi nmetaja wachache tu. Vyovyote iwavyo haki ya mtu iko palepale na ole wao waicheleweshao haki ya mtu. NIRUDIE KUKUPA POLE ILA ZAIDI NIKUPONGEZE KWANI UMEPATA FURSA YA PEKEE PENGINE ZAIDI YA MWANAUDSM YEYOTE WA ENZI HIZI. NIKUKUMBUSHE KUWA,"SUCCESS IS WALKING FROM FAILURE TO FAILURE WITHOUT LOOSING ENTHUSIASM THAT AT LAST U WILL IRRUPT IN VICTORY.
By Dennis Wilson
Usife Moyo Kaka Alphonce Lusako
Ni rafiki yangu niliyeachana naye chuo wakati huo yuko mwaka wa tatu nami nikiwa namalizia mwaka wa kwanza wa masomo mwaka 2011. Ni Kijana jasiri katika kusimamia Yale anayoyaamini. Alikuwa mstari wa mbele kuhoji uhalali wa mtoto wa maskini kunyimwa fedha za kujikimu na wengine kupewa fedha "kiduchu" kwa ajili ya masomo ya elimu ya juu. Ni mengi alikuwa mstari wa mbele kusimamia lakini hili la mtoto wa maskini kunyimwa fedha ndicho hasa siwezi kusahau kwa ndugu yangu huyu na alifanya kwa weledi Mkubwa kama msomi anayejielewa.
Misimamo yake ilitokea kutuvutia wengi na alikubalika kwa namna ya kipekee. Hakuwa anahoji au kuhimiza kuvunja majengo ya chuo, kuvuta bangi, kutumia madawa ya kulevya , uasherati na mengine mabaya, La hasha! Alikuwa anahoji mambo ya kumnufaisha mtoto wa maskini, na taifa kwa ujumla. Hakupenda vijana tuwe watu wa "NDIYO MZEE" bila kutumia akili zetu tulizojaliwa na MUNGU wakati tunaona mambo yanazidi kuharibika.
Aliondolewa masomoni kwa kile kilichodaiwa kuandaa migomo na kuhimiza machafuko na hivyo kutimuliwa kabisa masomo na baraza la chuo kwa maelekezo kutoka juu.
Kutokana na kupenda elimu aliendelea kupambana ili kuona naye anapata elimu kama watoto wengine wa walala hoi walio na bidii. Na mwaka Jana 2016 alifanya taratibu zote za udahili na akapata nafasi tena ya kujiunga na masomo katika chuo kikuu cha Dar es Salaam katika kitivo cha Sheria , amehudhuria vipindi vyote vya masomo kwa wiki 15 kama ilivyo utaratibu na umewadia wakati wa mitihani(UNIVERSITY EXAMINATION) ameingia kufanya mitihani, Ile ametoka tu kwenye mtihani anakuta kuna barua ya kumwondosha tena masomoni.
Inaumiza sana lakini ni matumaini yangu kwamba kaka yangu huyu ndoto alizo nazo na mategemeo mazuri kwa taifa hili atayaona. Yale ambayo ameyapigania kwa muda mrefu ipo siku atayaona kwa macho. Nichukue nafasi hii kumtia moyo , asikate tamaa maana Mtetezi wetu yu HAI.
WE SHALL OVERCOME Brother Alphonce Lusako (EMEKA)! Don't give up! Stay Strong !!
#Righteousness_Justice_and_Freedom
Dennis Wilson
By Ivon Ng'umbi
One scholar on the Earth once said "you can't teach old dogs new tricks"..I thought we are in the new era,the period where even the then administrators are thinking differently.Surprisingly, time changes but no change in the minds of the administrators. What is happening to Alphonce Lusako who is a great admirer to change is celebrated by the old dogs whose ideas are old- fashioned.Keep on fighting brother!
By Respicius Francis
Nimesikitishwa sana juu ya taarifa ya kutenguliwa kwa usajiri wake kaka yangu, rafiki yangu na kiongozi wangu Alphonce Lusako katiika chuo kikuu cha Dar Es Salaam.
Ikumbukwe Lusako alifukuzwa Chuo hapa UDSM 2011 katika harakati za kupinga ufisadi uliokuwa unafanyika TCU na HESLB ambapo baada ya kuingia Rais Magufuli ilibainika ni kweli Taasisi hizo za UMMA zilikuwa zikijihusisha na ufisadi mkubwa ikiwemo mikopo hewa na kubainika kuwa wanafunzi hewa na TCU kudaili wanavyuo wasio na vigezo.
Kwa kutambua umuhimu wa elimu ndugu Lusako akaomba upya kusoma sheria UDSM na akachaguliwa na kusajiriwa lakini leo akitokea kwenye mtihani wa kumaliza semesta ya kwanza ndugu Lusako anapewa barua ya kutenguliwa usajiri wake katika chuo hiki.
Imeniuma sana kupata taarifa hii na kujiuliza kwa nini chuo kilimsajiri na kumuacha akilipa gharama ikiwemo ada na vinginevyo huku wakijua sheria za chuo haziruhusu.
Ndugu yangu Lusako nakuomba cool down mungu ana mipango yake hizi ni changamoto za dunia japo natambua ulikuwa na malengo makubwa sana ila still kama ipo ipo hakuna binadamu wa kuzui riziki ya mtu.
Alphonce Lusako kwaheri mpambanaji. Ulifukuzwa mwaka 2011 ukiwa mwaka wa 3, Kwa kutambua umuhimu wa elimu ukaamua kurudi chuo kuendelea na masomo yako kwa kuanza mwaka wa kwanza sheria 2016, lakini leo baada ya kutoka kwenye mtihani umekutana na barua ikikutaka uondoke chuo haraka kwa sababu kuwa ulisajiliwa kimakosa. Inauma sana lakini ndio gharama halisi ya harakati za kujitoa kwajili
Comments
Post a Comment