Hii ndio timu mpya ya Okwi kwa sasa
Mshambuliaji Emmanuel Arnold Okwi amejiunga na klabu yake ya zamani ya SC Villa ya nchini kwao Uganda baada ya kuachana na klabu ya Denmark SønderjyskE.
Mshambuliaji huyo aliyeanza kucheza soka katika klabu hiyo ya Villa anarudi kwa mkataba mfupi ambapo atacheza kwenye klabu hiyo maarufu kama Jogoos mpaka mwisho wa msimu.
“Ni dili ambalo limeshakamilika”, Alisema Mkurugenzi Mkuu wa klabu hiyo ya Villa, Ivan Kakembo
Okwi ambaye aliachana na Villa kujiunga na Simba mwaka 2010 ataungana na wachezaji wengine wapya klabuni hapo ambao ni Sulaiman Luzige, Arthur Arakaza na Farouk Musisi.
Emanuel Okwi
Comments
Post a Comment