TATIZO LA KUKOSA HEDHI (AMENORRHEA)
K WA kawaida, mtoto wa kike akishafikia umri wa kuvunja ungo, anaanza kuona siku zake za hedhi. Huendelea kuona siku zake kwa kipindi chote cha maisha yake, mpaka anapofikia umri wa ukomo wa hedhi. Siku pekee ambazo mwanamke hatakuwa akiona siku zake, ni pale anapokuwa mjamzito mpaka miezi kadhaa baada ya kujifungua. Hata hivyo, wapo ambao licha ya kufikisha umri wa kuvunja hedhi, huwa hawazioni siku zao na tatizo hili huweza kuendelea kwa kipindi kirefu na kumsababishia mhusika matatizo mengi, ikiwa ni pamoja na kukosa uwezo wa kunasa ujauzito. Tatizo hili kitaalamu huitwa Amenorrhea. Tatizo hili limekuwa likiwaletea usumbufu mwingi wa kisaikolojia wanawake wengi waliowahi kukumbana nalo. Tatizo hili limegawanyika katika makundi mawili: primary amenorrhea na seconday amenorrhea. PRIMARY AMENORRHEA Hii ni hali ya kukosa hedhi inayoweza kumtokea msichana aliye katika umri wa kuvunja ungo na ambayo huweza kuendana na hali ya kukosa mabadiliko ya kuv...