Posts

Ajali ya boti yaua 59

Image
  Takriban wahamiaji 59, wakiwemo watoto 12, wamefariki dunia na makumi ya wengine wanahofiwa kutoweka baada ya boti yao kuzama kwenye bahari ya kusini mwa Italia. Boti hiyo ilizama ilipokuwa ikijaribu kutia nanga karibu na mji wa pwani wa Crotone katika eneo la Calabria. Walionusurika walisema angalau watu 150 walikuwa ndani. Wengi wao walikuwa wakikimbia hali ngumu, rais wa Italia alisema. Waziri wa Mambo ya Ndani Matteo Piantedosi, ambaye alitembelea eneo la tukio, alisema hadi watu 30 bado hawajulikani walipo. Mtoto anayedhaniwa kuwa na umri wa miezi michache tu alikuwa miongoni mwa waliofariki, kulingana na shirika la habari la Ansa la Italia. Miili iliopolewa kutoka ufukweni katika eneo la mapumziko lililo karibu la bahari. Walinzi wa pwani walisema watu 80 wamepatikana wakiwa hai, “ikiwa ni pamoja na wengine ambao walifanikiwa kufika ufukweni baada ya kuzama”. Idadi kamili ya watu waliokuwa kwenye boti hiyo ilipovunjika haijabainika – waokoaji waliliambia shirika la habari l...

UTEUZI: RAIS SAMIA AFANYA UTEUZI MUDA HUU, MWANA FA ATEULIWA

Image

Simba Yashinda dhidi ya Vipers huko Uganda

Image
  NA EMMANUEL MBATILO KLABU ya Simba imefanikiwa kuondoka na alama tatu ugenini baada ya kufanikiwa kuichapa Vipers ya nchini Uganda 1-0, na kufanikiwa kushika nafasi ya tatu kwenye kundi akiwa amecheza mechi tatu. Katika mchezo huo muhimu ambao Simba Sc alihitaji kupata ushindi ili aweze kupata matumaini katika kuwania nafasi mbili za juu na kuweza kutinga robo fainali kwenye michuano hiyo ya Klabu Bingwa Afrika inayoendelea. Simba Sc ilifanikiwa kupata bao la mapema kipindi cha kwanza kupitia kwa beki wao kisiki Inonga Baka na kuiwezesha timu yake kuibuka na ushindi wa bao 1-0.

MWANAFUNZI AMUUA MWALIMU KWA KUMCHOMA KISU

Image
Mwalimu mmoja ameuawa mikononi mwa mwanafunzi wake ambaye alimshamubulia kwa kisu katikati ya somo. Katika tukio hilo la Jumatano, Februari 22, lililotokea magharibi mwa Ufaransa, mwalimu huyo wa Kihispania mwenye umri wa miaka 52, alikuwa akifundisha darasani wakati mwanafunzi huyo mwenye umri wa miaka 16, alipomshambulia kwa kisu. Shirika la habari la AFP likinukuu ripoti ya gazeti la Sud Ouest, lilisema kuwa mvulana huyo aliingia darasani wakati wa somo la Kihispania la mwalimu huyo. Mwanafunzi huyo alifunga mlango wa darasa hilo kwa ndani na kumchoma kisu mwalimu kifuani mwake. Kisha mwalimu huyo wa kike alifanyiwa huduma ya kwanza lakini alifariki kutokana na majeraha aliyopata huku mwanafunzi huyo akikamatwa na kwa sasa anazuiliwa kwenye seli ya polisi. Vyombo vya habari nchini humo vilinukuu chanzo kikisema kuwa mvulana huyo alimwambia mwalimu mwingine kuwa sauti ilimwambia atekeleze kitendo hicho. Kufuatia tukio hilo katika Shule ya Saint-Thomas d'Aquin, ...

Umuhimu wa fasihi simulizi kwenye jamii

  i)  Kuburudisha Fasihi simulizi huweza kutumiwa kama burudani kwenye mkusanyiko wa jamii. Tanzu kama hadithi, ushairi, semi (methali, vitendawili, nk.) aghalabu hutumiwa ili kuwaburudisha waliokusanyika katika jamii. Kwa mfano, watoto wanapokusanyika kucheza, aghalabu hutegeana vitendawili kama njia ya kujiburudisha. Hadithi, ngano, hekaya au hata hurafa huweza pia kutambwa kama njia ya burudani. (ii) Kuelimisha    Kwa kutumia fasihi simulizi, wanajamii wanaweza kuzielimisha thamani za kijamii, historia yao, utamaduni na mtazamo wao kilimwengu kutoka kizazi kimoja hadi chengine. (iii)  Kuipa Jamii Muelekeo Kwa njia ya kuelimishana kimawazo yanayohusiana na tamaduni na desturi za jamii husika, wanajamii wanahakikisha kwamba jamii, kwa kutumia fasihi simulizi, inapata muelekeo utakaowabainisha wao mbali na wengine. (iv) Kuhifadhi Historia na Utamaduni Katika kuhifadhi amali muhimu za  kijamii, fasihi simulizi inakuwa nyezo muhimu. A...

NADHARIA YA SEMIOTIKI

  Neno semiotiki limetokana na mnyambuliko wa neno la Kigiriki ‘ semeion ’ lenye maana ya ishara na linalowakilisha vikundi vya wafuasi wa mielekeo fulani kulingana na maelezo ya John Selden. Yaliyomo 1. NADHARIA ya simiotiki  2. Marejeo ya nadharia ya semiotiki Kwa upande mwingine Wamitila anapambanua kwamba ‘semiotiki’ ni neno la lugha ya Kiyunani lenye maana ya ishara na ambalo linatumiwa kuelezea mielekeo ya makundi fulani ya Uhakiki. Wamitila anakubaliana na Selden kuhusu asili ya neno semiotiki kwa kuwarejelea wasomi Bailey, Matejk na Steiner walioeleza kuwa semiotiki ni mchakato ambapo vitu na matukio huja kutambuliwa kama ishara na kiumbe hai ambacho kinahisi. Kulingana na Selden, semiotiki ni taaluma ambayo hufanya kazi kwenye desturi pana za kiutamaduni zinazohusisha ishara violwa na ishara tajwa. Anapozungumzia semiotiki ya kisasa anasema kuwa inatumiwa kurejelea uwanja unaoendelea kubadilika wa elimu ya masomo ambayo huangaza fenomena ya maana katika j...

NADHARIA YA MWITIKO WA MSOMAJI

Yaliyomo NADHARIA YA MWITIKO WA MSOMAJI MAANA YA NADHARIA (Williady, 2013), Nadharia ni maelezo yakinifu kuhusu kitu, tajiriba, mahalifa au upumbavu na mafanikio au maangamizi yanayochomoza katika jamii. Hivyo nadharia hufungamana na mambo mbalimbali ya jamii kama vile mbinu, maarifa, tasinifu, mikabala na mienendo mbalimbali ya jamii. 1. NADHARIA YA UPOKEZI (MWITIKO WA MSOMAJI) Nadharia ya Upokezi (mwitiko wa msomaji) ambayo husisitiza nguvu ya msomaji. Nadharia ya Upokezi (Reception Theory) iliasisiwa na wahakiki wa waasisi wa Kijerumani mwishoni  mwa miaka ya 1960.Miongoni mwa waasisi wa nadharia hii ni Robert C. Holub,Hans Robert  Jauss na Wolfagang Isser.Katika kitabu chake Reception Theory (1984), Holub anaelezea nadharia ya Upokezi  kuwa ni Mabadiko ya jumla ya umakinikiaji kutoka kwa mwandishi na kazi yake kwenda kwa matini na msomaji” Nadharia ya upokezi inaakisi mabadiliko ya mbinu katika historia ya fasihi na ilizingatiwa ka...