Posts

HIKI HAPA KIKOSI CHA SIMBA MICHUANO YA SPORTPESA

Image
MICHUANO ya SportPesa Super Cup inatarajiwa kuanza Juni 3 jijini Nairobi na mabingwa wa Tanzania Bara Simba SC wanatarajiwa kuondoka saa 12 asubuhi ya leo Alhamisi na kikosi kamili kwenda kusaka tiketi ya kucheza na Everton nchini Uingereza Ukimuondoa Haruna Niyonzima, Simba itawakosa nyota wake wengine wote wa kigeni pamoja na nahodha John Bocco huku akijumuishwa mshambuliaji mpya aliyesajiliwa kutoka Majimaji ya Songea, Marcel Kaheza. Taarifa zinadai Adam Salamba anatarajiwa kuungana na wenzake Jumamosi hii.

SIMBA , AZAM HAWANA HURUMA , WAMEAMUA KUISAMBARATISHA YANGA KABISA , NYOTA HAWA WANATUA SIMBA , AZAM

Image
Obrey Chirwa. LICHA ya ku­maliza msimu kwenye nafasi ya tatu ambayo ni mbaya zaidi kuwahi ku­watokea katika miaka ya hivi karibuni, Yanga im­ekumbana na kasheshe jingine ambalo limefan­ya mambo yao kuwa ma­baya zaidi. Simba na Azam zimea­mua kuanzia vurugu zake za usajili katika kikosi cha Yanga ambapo zote mbili zimeikomalia kwelikweli huku mastaa wakubwa wa Jangwani wakionekana kupagawa na mafungu waliyowekewa mezani. Usajili rasmi unaanza Juni 15 lakini Simba na Azam zimeanza kuvuna Jangwani. Kwanza Yanga walikuwa wanamtaka Adam Salamba kutoka Lipuli, lakini juzi jioni ali­washangaza wengi baada ya kutua Simba kwa kile kilichodaiwa kuwa Yanga walishindwa kufikia dau linalotakiwa. Simba wamempa Salamba Sh40milioni taslimu na jana Jumanne walimkabidhi gari ya kutembelea aina ya Crown mpya yenye thamani ya zaidi ya Sh15milioni. Championi Jumatano,  ambalo ndilo gazeti la Kiswahili linaloongoza kwa mauzo Tanzania, linafahamu kuwa wache­zaji muhimu wa Yanga wa...

REYE’S SYNDROME TATIZO LINALOWEZA KUSABABISHWA NA MATUMIZI YA ASPIRINE

Image
Reye’s syndrome ni hali inayojitokeza kwa nadra lakini ni tatizo endapo itatokea ambalo husababisha kuvimba kwa ini na ubongo. Tatizo hili mara nyingi huathiri watoto wa rika dogo ambao wanapona kutoka kwenye maambukizi ya virusi mara nyingi mafua ama tetekuwanga. Dalili na viashiria kama kuchanganyikiwa, degedege na kupoteza fahamu huhitaji matibabu ya haraka.  Kugunduliwa mapema na kupata matibabu huweza kuokoa maisha ya mtoto. Dawa ya aspirini imekuwa ikihusishwa na tatizo la reyes syndrome, kwa hivo chukua tahadhali unapokuwa unampa mtoto ama kijana wako dawa hii. Ingawa dawa ya aspirini inashauriwa kuanza kutumika kwa watoto walio na miaka kuanzia miwili(2), watoto wanaopona kutoka kwenye maambukizi ya mafua na tetekuwanga hawatakiwi kutumia dawa hii kabisa. Ongea na daktari wako endapo  unataka ufafanuzi zaidi Dalili Mtoto mwenye tatizo la reyes mara nyingi kiwango cha sukari wmilini hushuka wakati kiwango cha kemikali za ammonia na hali ya as...

MBWANA SAMATTA AFANYA ZIARA MAKKA

Image
Nahodha wa timu ya taifa ya Tanzania, na mchezaji wa timu ya Genk ya Ubelgiji, Mbwana Samatta (kulia) akiwa msikitini Makka. …Akiwa na mchezaji mwenzake wa timu ya Genk,  Omar Colley. Nahodha wa timu ya soka ya taifa ya Tanzania, Mbwana Samatta,  anayekipiga katika timu ya Genk ya nchini Ubelgiji baada ya kumaliza msimu wa ligi kuu nchini humo,  ameelekea nchini Saudia Arabia kwa ajili ya kufanya ziara ya kidini huko Makka. Samatta anatarajiwa kurudi Tanzania mwishoni mwa wiki hii kujiandaa na mchezo wa hisani kati yake na mwanamuziki Alikiba katika mchezo wa soka utakaofanyika Juni 9 mwaka huu kwenye Uwanja wa taifa kati ya Timu Alikiba dhidi ya Timu Samatta.

AUDIO | Kala Jeremiah Ft Walter Chilambo - NATABIRI | Download

Image
DOWNLOAD

KIJANA ALIYEMWOKOA MTOTO, AJIUNGA NA JESHI UFARANSA – PICHAZ

Image
KIJANA shujaa mhamiaji kutoka nchini Mali, Mamoudou Gassama aliyemwokoa mtoto aliyekuwa amening’inia kwenye kibaraza cha ghorofa ya nne katika jengo refu jijini Paris, Ufaransa tayari amejiunga na Jeshi la Zima Moto na Uokoaji la Ufaransa, baada ya kupewa ajira hiyo na Rais wa Ufaransa, Emmanuel Macron Mamoudou alipanda jengo hilo refu bila kutumia vifaa vyovyote huku akishangiliwa na watu waliokuwa wamekusanyika nje ya jengo hilo, hadi kufanikisha kumfikia mtoto huyo wa kiume mwenye umri wa miaka minne na kumuokoa. Rais wa Ufaransa, Emmanuel Macron alimualika kijana huyo Ikulu na kuzungumza naye, kisha akampa cheti maalum cha kutambua ushujaa wake na kuamuru apewe uraia wa Ufaransa baada ya kusikia jinsi alivyohangaika kuingia nchini humo. Pia, Rais Macron alimpatia kazi Mamoudou katika Jeshi la Zima moto la Ufaransa, pia amemtunukia medali ya kipekee ya ushujaa kijana huyo na kuwataka raia wote kuiga mfano wake. Aidha, Rais wa Mali,  Ibrahim Boubacar Keïta ...

MHADHIRI UDSM ACHAGULIWA KUWA KATIBU MKUU CCM KUCHUKUA NAFASI YA KINANA

Image
Chama cha Mapinduzi (CCM) kimemteua Dk Bashiru Ali kuwa katibu mkuu wa chama hicho. Taarifa kwa vyombo vya habari iliyotolewa Mei 29,2018 na Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Humphrey Polepole imesema Dk Bashiru ambaye ni mhadhiri wa masuala ya Sayansi ya Siasa wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) ndiye mrithi wa Abdulrahman Kinana aliyestaafu jana. Mwenyekiti wa CCM, Rais John Magufuli aliridhia ombi la Kinana kujiuzulu jana. Dk Bashiru ndiye aliongoza tume ya kuchunguza mali za CCM. Taarifa ya CCM imesema, Raymond Mangwala ameteuliwa kuwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana (UVCCM) na Queen Mlozi, kuwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Wanawake (UWT). Erasto Sima ameteuliwa kuwa Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Wazazi ya CCM.