MBWANA SAMATTA AFANYA ZIARA MAKKA


Nahodha wa timu ya taifa ya Tanzania, na mchezaji wa timu ya Genk ya Ubelgiji, Mbwana Samatta (kulia) akiwa msikitini Makka.
…Akiwa na mchezaji mwenzake wa timu ya Genk,  Omar Colley.
Nahodha wa timu ya soka ya taifa ya Tanzania, Mbwana Samatta,  anayekipiga katika timu ya Genk ya nchini Ubelgiji baada ya kumaliza msimu wa ligi kuu nchini humo,  ameelekea nchini Saudia Arabia kwa ajili ya kufanya ziara ya kidini huko Makka.
Samatta anatarajiwa kurudi Tanzania mwishoni mwa wiki hii kujiandaa na mchezo wa hisani kati yake na mwanamuziki Alikiba katika mchezo wa soka utakaofanyika Juni 9 mwaka huu kwenye Uwanja wa taifa kati ya Timu Alikiba dhidi ya Timu Samatta.

Popular posts from this blog

HIZI HAPA SMS TAMU ZA KUMTAKIA USIKU MWEMA MPENZI WAKO

SMS na MESEJI 900+ za mapenzi

MIAKA 22 SASA TANGU KUZAMA KWA MELI KUBWA YA MV BUKOBA, TANZANI TUMEJIFUNZA NINI?