MHADHIRI UDSM ACHAGULIWA KUWA KATIBU MKUU CCM KUCHUKUA NAFASI YA KINANA



Chama cha Mapinduzi (CCM) kimemteua Dk Bashiru Ali kuwa katibu mkuu wa chama hicho.

Taarifa kwa vyombo vya habari iliyotolewa Mei 29,2018 na Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Humphrey Polepole imesema Dk Bashiru ambaye ni mhadhiri wa masuala ya Sayansi ya Siasa wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) ndiye mrithi wa Abdulrahman Kinana aliyestaafu jana.

Mwenyekiti wa CCM, Rais John Magufuli aliridhia ombi la Kinana kujiuzulu jana.

Dk Bashiru ndiye aliongoza tume ya kuchunguza mali za CCM.

Taarifa ya CCM imesema, Raymond Mangwala ameteuliwa kuwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana (UVCCM) na Queen Mlozi, kuwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Wanawake (UWT).

Erasto Sima ameteuliwa kuwa Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Wazazi ya CCM.

Popular posts from this blog

HIZI HAPA SMS TAMU ZA KUMTAKIA USIKU MWEMA MPENZI WAKO

SMS na MESEJI 900+ za mapenzi

MIAKA 22 SASA TANGU KUZAMA KWA MELI KUBWA YA MV BUKOBA, TANZANI TUMEJIFUNZA NINI?