Posts

TANZIA: Aliyewahi kuwa mkuu wa mikoa mbalimbali nchini, Abass Kandoro afariki dunia Hospitali ya Taifa Muhimbili

Image
TANZIA: Aliyewahi kuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Abbas Kandoro afariki dunia usiku huu Kandoro amefariki katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili alikolazwa kwa matibabu

Historia Imeandikwa......Rais Kim Jong-Un Avuka Mpaka na Kuingia Korea Kusini

Image
Rais Kim Jong-Un wa Korea Kaskazini amekuwa kiongozi wa kwanza wa taifa hilo kuvuka mpaka wa kijeshi uliowekwa kuzitenganisha nchi hizo mbili baada ya vita ya mataifa hayo mawili mwaka 1953. Akiwa ni mwenye tabasamu rais Korea kusini Moon Jae-in amempokea mgeni wake katika eneo la mpakani. Ni miaka 65 hadi sasa kwa kiongozi wa Korea Kaskazini kuwahi kuvuka mpaka wa kijeshi uliowekwa kuzitenganisha Korea Kaskazini na Korea Kusini tangu kumalizika kwa vita vya mataifa hayo mawili mwaka 1953. Eneo la mpaka huo aliouvuka Kim Jong Un wakati akielekea Korea kusini ni lenye kilomita 250 na upana wa kilomita nne,ambapo mara baada ya kuuvuka tu watu walipiga makofi kwa kuandikwa kwa historia. Mkutano huo wa tatu baada ya mkutano wa mwaka 2000 na 2007 ni matokeo ya jitihada zilizofanyika miezi kadhaa kuimarisha mahusiano kati ya Korea hizi mbili na kufungua milango ya mkutano kati ya Kim na Rais wa Marekani Donald Trump. Kim alitangaza juma lililopita kuwa angesitisha zoezi ...

KOCHA WA SIMBA ANAONDOKA

Image
Taarifa zinaeleza kuwa Kocha Mkuu wa Simba, Pierre Lechantre, amekuwa miongoni mwa Makocha 77 waliotuma maombi ya kazi nchini Cameroon. Lechantre ambaye amejiunga na Simba kuchukua mikoba ya Mcameroon Joseph Omog, ametuma maombi ya kuomba nafasi ya kuifundisha timu ya taifa ya Cameroon huku akikumbana na mchuano mkali. Cameroon ipo katika msako wa kocha mpya ili kuchukua nafasi ya Hugo Broos aliyefungashiwa virago mwishoni mwa mwaka jana. Inaelezwa pia Mcameroon wa zamani wa Simba, Joseph Omog, ni moja ya Makocha waliotuma maombi ya kukinoa kikosi hicho cha Cameroon, maarufu kama Indomitable Lions. Kocha wa zamani wa Yanga, Tom Saintfiet naye ametuma maombi ya kupata kibarua cha kuifundisha timu hiyo. Uwepo wa Makocha hao unafanya mchuano wa kupata kazi ya kuinoa Cameroon kuwa mgumu kwa Lechantre, kutokana na asilimia ya wengi kuwa na CV's nzuri. Mfaransa wa Simba ametuma maombi hayo akiwa anakiandaa kikosi chake kuelekea mechi dhidi ya watani wa jadi...

SIMBA YA ONYWA

Image
Katibu Mkuu wa zamani wa Yanga, Dokt. Jonas Tiboroha, amewasihi Simba kutoibeza Yanga kuelekea mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi yao, utakaopigwa Uwanja wa Taifa, Jumapili ya wiki hii. Simba na Yanga zitakutana katika mechi hiyo inayosubiriwa na umati lukuki wa mashabiki wa soka la Tanzania nchini. Tiboroa ameeleza kuwa msimu huu Yanga haijafanya vizuri kama Simba ambayo imeonekana kuwa ina kikosi kipana. Katibu huyo wa zamani wa Yanga ameeleza pia uzuri wa Simba usiwafanye wajiamini zaidi kuelekea mechi hiyo ambayo huwa si rahisi kutabirika pindi vigogo hawa wanapokutana. "Unajua timu hizi zinapokutana si rahisi kutabirika, Simba wapo vizuri msimu huu, wana kikosi kipana, lakini hawapaswi kuibeza Yanga kwa maana yeyote yule anaweza akapata matokeo.

IKUFIKIE HII MWANA SIMBA

Image
Vinara wa Ligi Kuu Bara, Simba wamerejea jijini Dar es Salaam leo wakitokea Morogoro. Simba wamerejea jijini Dar es Salaam wakitokea Morogoro, hali ambayo imewashangaza wengi. BASI LA SIMBA LIKIONDOKA MJINI MOROGORO LEO KUREJEA DAR ES SALAAM Kawaida huondoka siku moja kabla ya mechi, lakini Simba wameamua kurejea Dar es Salaam siku mbili kabla. Simba ilikuwa Morogoro kujiandaa na mechi dhidi ya watani wake Yanga kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, Jumapili. Yanga pia wameweka kambi mjini Morogoro kujiandaa na mechi hiyo inayosubiriwa kwa hamu na mashabiki wa soka nchini.

UMESIKIA KILICHO IKUTA SIMBA ?

Image
KLABU ya Simba SC imepigwa faini ya Sh. 500,000 kwa kuonyesha vitendo vinavyoashiria ushirikina katika mechi namba 171 dhidi ya wenyeji Njombe FC Aprili 3, 2018 kwenye Uwanja wa Saba Saba mjini Njombe. Taarifa ya Kamati ya Usimamizi na Uendeshaji wa Ligi, maarufu kama Kamati ya Saa 72 ya Bodi ya Ligi katika kikao chake kilichopita kupitia taarifa na matukio mbalimbali na kufanya uamuzi ufuatao imesema vitendo hivyo ni pamoja na shabiki mmoja wa timu hiyo kuingia uwanjani na kuchukua taulo la kipa wa Njombe Mji lililokuwa golini.  Taarifa hiyo imesema kwamba adhabu hiyo imetolewa kwa kuzingatia Kanuni ya 42(1) ya Ligi Kuu kuhusu Udhibiti wa Klabu. Simba SC pia imepigwa faini ya Sh. 500,000 kutokana na mashabiki wake kuingia uwanjani baada ya filimbi ya mwisho kwenye mechi namba 165 dhidi ya Mtibwa Sugar Aprili 9, 2018 kwenye Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro. Kitendo hicho cha washabiki wa Simba iliyokuwa ikicheza ugenini ni ukiukaji wa Kanuni ya 14(11) ya Ligi Kuu kuhusu Taratib...

WATU 9 WAKAMATWA WAKIANDAMANA POSTA , DAR ES SALAAM

Image
Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa amethibitisha kukamatwa kwa watu 9 waliokuwa wakiandamana eneo la Samora Avenue, Posta. Watu hao wamekamatwa baada ya Jeshi la Polisi kuonya kuwa litawachukulia hatua kali wale wote watakaokaidi agizo la kutoandamana kama walivyoagiza. Watu hao walikuwa wakiandamana kufuatia maandamano yaliyohamasishwa  kupitia mitandao ya kijamii yeye lengo la kupinga baadhi ya mambo yanayofanywa na serikali. Mbali na watu hao, baadhi ya maeneo mengine ya Jiji la Dar es Salaam leo yamekuwa na watu wachache sana tofauti na siku nyingine za mapumziko, ambapo watu wengi wamekuwa na hofu ya kutoka, kutokana na tetesi za kuwapo kwa maandamano. Hapa chini ni baadhi ya picha za muonekano wa Jiji la Dar es Salaam; Picha zote na Sammy Awami.