WATU 9 WAKAMATWA WAKIANDAMANA POSTA , DAR ES SALAAM



Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa amethibitisha kukamatwa kwa watu 9 waliokuwa wakiandamana eneo la Samora Avenue, Posta.

Watu hao wamekamatwa baada ya Jeshi la Polisi kuonya kuwa litawachukulia hatua kali wale wote watakaokaidi agizo la kutoandamana kama walivyoagiza.

Watu hao walikuwa wakiandamana kufuatia maandamano yaliyohamasishwa  kupitia mitandao ya kijamii yeye lengo la kupinga baadhi ya mambo yanayofanywa na serikali.

Mbali na watu hao, baadhi ya maeneo mengine ya Jiji la Dar es Salaam leo yamekuwa na watu wachache sana tofauti na siku nyingine za mapumziko, ambapo watu wengi wamekuwa na hofu ya kutoka, kutokana na tetesi za kuwapo kwa maandamano.

Hapa chini ni baadhi ya picha za muonekano wa Jiji la Dar es Salaam;
Picha zote na Sammy Awami.

Popular posts from this blog

HIZI HAPA SMS TAMU ZA KUMTAKIA USIKU MWEMA MPENZI WAKO

SMS na MESEJI 900+ za mapenzi

MIAKA 22 SASA TANGU KUZAMA KWA MELI KUBWA YA MV BUKOBA, TANZANI TUMEJIFUNZA NINI?