Posts

NECTA: Matokeo ya Kidato cha Nne 2017 kwa Waliokuwa Wamekata Rufaa

Image
KUONA MATOKEO BONYEZA HAPA

PICHA : WABUNGE, MADIWANI WAANDAMANA OFISI, UMOJA WA ULAYA

Image
Wabunge na Madiwani wa Chadema, leo mchana Machi 29, 2018 wameandamana kwenda ofisi za Umoja wa Ulaya (EU). Wabunge hao wamekwenda katika ofisi hizo kulalamikia kile wanachofanyiwa viongozi sita wa chama hicho akiwamo mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe waliopo mahabusu. Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema amesema, “Tuko EU (Umoja wa Ulaya). Tupo wabunge wote tumeandamana kuja hapa kuleta kilio chetu.”   Miongoni mwa Viongozi waliofika katika ubalozi huo ni Mbunge wa Arusha Mjini Godbless Lema, Meya wa Ubungo Bonface Jacob ambapo wametahadhalisha usalama wa Viongozi hao pamoja wafuasi wa chama hicho.

MTWARA : MWANAFUNZI KIDATO CHAPILI AJINYONGA

Image
Binti Salma Abdalah ambaye ni mwanafunzi wa kidato cha pili mkoani Mtwara aliyekuwa akiishi Mbawala Chini, amefariki dunia kwa kujinyonga, baada ya kukutwa na simu ambayo alipewa na mpenzi wake. Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo, Kamanda wa Polisi mkoa wa Mtwara Lucas Mkondya, amesema tukio hilo limetokea mwanzoni mwa wiki hii baada ya wazazi wa binti huyo kuamua kumfukuza nyumbani na kumtaka kwenda kuishi kwa bibi yake kutokana na utovu wa nidhamu, na ndipo akaamua kujitoa uhai wake. Kamanda Mkondya ameendelea kwa kueleza kwamba wazazi wake waligundua kuwa binti yao alikuwa akimiliki simu ambayo hawajamnunulia, na walipomuuliza hakuwa na jibu sahihi, ndipo baba mtu ambaye ni baba wa kufikia aliamua kumfukuza nyumbani kutokana na kuchoshwa na tabia zake za utovu wa nidhamu, na kuelekea sokoni kwenye biashara zake kumtafutia nauli, huku mama yake akielekea shambani kwenye shughuli zake za kilimo, “Ni binti ambaye alikuwa ni mwanafunzi wa kidato cha pili, sasa asubuhi ...

MTEULE KUTOKA JAMII YA OROMO AWA WAZIRI MKUU ETHIOPIA

Image
Ahmed anatoka katika kabila kubwa zaidi nchini Ethiopia la Oromo ambalo limekuwa likifanya maandamano ya kuipinga serikali tangu mwaka 2015. Daktari  Abiy Ahmed Ali , anayetoka jamii ya Oromo yenye watu wengi Ethiopia, amechaguliwa kuwa mwenyekiti wa muungano unaotawala EPRDF, hatua itakayomfanya kuwa Waziri Mkuu mteule wa nchi hiyo.  Ahmed  alichaguliwa kwa zaidi ya asilimia 60 ya kura zilizopigwa kwa mujibu wa vyombo vya habari vya serikali na atachukua wadhifa huo kutoka kwa  Hailemariam Desalegn  aliyetangaza ghafla kujiuzulu mwezi uliopita. Taifa hilo kwa sasa liko katika hali ya dharura iliyotangazwa kwa ajili ya kumaliza maandamano ya takriban miaka mitatu dhidi ya serikali. Dkt  Ahmed , 42, anatazamwa na wengi kama mwenye kuzungumza kwa uwazi, mwenye ujuzi na uzoefu, na mwenye kukumbatia uongozi wa kuwashirikisha wote. Anaaminika kuwa na ufuasi mkubwa miongoni mwa vijana wa Kioromo na pia katika jamii nyingine. Wakosoaji wa...

MH Mbowe na Viongozi Wengine wa CHADEMA Wafikishwa Tena Mahakamani

Image
Viongozi sita wa Chadema wamefikishwa leo saa 2 asubuhi katika Mahakama ya Kisutu kwa ajili ya kusikiliza uamuzi wa dhamana yao, huku ulinzi ukiimarishwa katika eneo hilo. Kesi hiyo inatajwa leo Machi 29, ambapo Hakimu Mkazi Mkuu Wilbard, Mashauri atatoa uamuzi kama washtakiwa hao watapata dhamana au hawatapata. Wakati viongozi hao wakifikishwa mahakamani, Jeshi la Polisi limeimarisha ulinzi kuzunguka viunga vya mahakama ya Kisutu. Katika lango kuu la kuingia mahakamani hapo, polisi waliovalia kiraia walifanya ukaguzi kwa kila anayeingia na kutoka na kuwazuia baadhi.

Mwigulu Awaponza Wanafunzi Sita Udsm, Walimwa Barua Ya Onyo

Image
Wanafunzi sita wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), wamelimwa barua za onyo kwa kuhamasisha maandamano kinyume cha sheria. Wanafunzi hao wanadaiwa kuhamasisha maandamano kutaka Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba ajiuzulu kutokana na kifo cha mwanafunzi wa Chuo cha Usafirishaji (NIT), Aquilina Akwilini, aliyeuawa kwa risasi Februari mwaka huu. Katika barua yake ambayo imesainiwa na Makamu Mkuu wa Chuo (Taaluma), Profesa David Mfinanga, kwenda kwa wanafunzi hao ambao wamekataa majina yao yasitajwe, imesema onyo hilo ni la mwisho na endapo wataendelea kujihusisha na vitendo hivyo watasimamishwa masomo mara moja kulingana na kipengele 14(xi) wakati mashtaka dhidi yake yakiandaliwa na kushughulikiwa. “Uongozi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, umepata taarifa kuwa wewe ni miongoni mwa wanafunzi wanaojihusisha na vitendo kinyume cha sheria ndogo ndogo za wanafunzi wa Chuo Kikuu ya mwaka 2011, hususan makosa yaliyoainishwa kwenye vipengele 4.2(vxiii), 4.2(xix) n...

Mwanamke Aliyemwaga Machozi Mbele ya Rais Magufuli Afungwa Jela Miezi Mitatu

Image
Mahakama ya Mwanzo Usambara mkoani Tanga imemhukumu kwenda jela miezi mitatu Swabaha Shosi ambae alishawahi kushika headlines kwa kulia mbele ya Rais Magufuli wakati wa maadhimisho ya siku ya sheria February 2, 2017. Hakimu wa Mahakama hiyo Khadija Kitogo amemtia hatiani kwa kuingia eneo lisiloruhusiwa kisheria. Swahaba alifikishwa Mahakamani hapo August 9, 2017 akikabiliwa na shtaka la kuingia Chongoleani ambako hakuruhusiwi Raia kuingia. Mahakama ilielezwa kuwa aliingia katika eneo lililokuwa limetengwa kwa ajili ya ujio Rais Magufuli na Yoweri Museveni walipokwenda kuzindua mradi wa bomba la mafuta kutoka Uganda mpaka Hoima. Swahaba alikana mashtaka hayo na kujitetea kuwa alikanyaga eneo wakati akiandaa eneo kwa ajili ya kuwauzia chakula waliodhuria uzinduzi huo na kwamba hakuwa peke yake walikuwa wengi. Hakimu Kitogo akitoa hukumu hiyo amesema baada ya kusikiliza ushahidi wa pande zote mahakama imemkuta na hatia ya kuvunja sheria ya Makosa...