PICHA : WABUNGE, MADIWANI WAANDAMANA OFISI, UMOJA WA ULAYA

Wabunge na Madiwani wa Chadema, leo mchana Machi 29, 2018 wameandamana kwenda ofisi za Umoja wa Ulaya (EU).

Wabunge hao wamekwenda katika ofisi hizo kulalamikia kile wanachofanyiwa viongozi sita wa chama hicho akiwamo mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe waliopo mahabusu.

Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema amesema, “Tuko EU (Umoja wa Ulaya). Tupo wabunge wote tumeandamana kuja hapa kuleta kilio chetu.”
 
Miongoni mwa Viongozi waliofika katika ubalozi huo ni Mbunge wa Arusha Mjini Godbless Lema, Meya wa Ubungo Bonface Jacob ambapo wametahadhalisha usalama wa Viongozi hao pamoja wafuasi wa chama hicho.

Popular posts from this blog

HIZI HAPA SMS TAMU ZA KUMTAKIA USIKU MWEMA MPENZI WAKO

SMS na MESEJI 900+ za mapenzi

MIAKA 22 SASA TANGU KUZAMA KWA MELI KUBWA YA MV BUKOBA, TANZANI TUMEJIFUNZA NINI?