KUVIMBA KWA MISHIPA YA DAMU WAKATI WA UJAUZITO (VARICOSE VEINS)

Kuvimba kwa mishipa ya damu(Varicose veins) hasa miguuni ni kitu kinachowatokea mama wajawazito walio wengi.Tatizo hili mara nyingi hutokea wakati mimba imekua kubwa kuanzia miezi 8 hadi 9 japo kwa baadhi ya watu hali hii huweza kutokea katika umri mdogo. Mishipa hii huvimba na inaweza kuonekana kwenye ngozi kama Mistari iliyovimba kwenye ngozi isiyoinyooka yenye rangi inaelekea kuwa kama blue. Watu wanopata ujauzito katika umri mkubwa ndio wanakua kwenye hatari kubwa ya kutokewa na hali hii,pia watu wenye uzito kupita kiasi (wanene sana) wanakua kwenye hatari ya kukumbwa na hali hiii. Hizi varicose veins zinatokea sana miguuni,ila zinaweza kutokea maeneo mengine kama kwenye uke na shingo ya kizazi,zinapotokea maeneo haya mama hutokwa na majimaji ukeni yaliyochanganyikana na damu. Varicose veins zinapotokea sehemu ya haja kubwa ndio tunaiita Bawasiri (Haemorrhoids) DALILI ZA TATIZO HILI Mistari myembamba yenye rangi ya blue inayoonekana kwenye ngozi Uvimbe kwenye ngozi ambao...