Posts

Bodi ya mikopo mchana huu

Image
Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu haitozi riba – Mwaisobwa  8:00 AM     ELIMU, KITAIFA    Mkurugenzi Msaidizi wa Habari, Elimu na Mawasiliano kutoka Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu, Cosmas Mwaisobwa amesema Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu pamoja na kwamba inatoa mikopo kwa wanafunzi haitozi riba katika marejesho ya mkopo huo. Akizungumza Jijini Dar es salaam katika Kipengele kinachoitwa KIKAANGONI cha EATV , Mwaisobwa amesema kwamba Bodi ya Mikopo inachokifanya kwa walipaji ni kutoza tozo ya kulinga thamani ya mkopo ambao mnufaika alichukua. 'Tunatoza kiwango cha asilimia 6% ya tozo ya kulinda thamani ya mkopo kiwango ambacho ni tofauti kabisa na riba, ukiangalia benki kwa sasa hivi kuna ambazo zinatoza zinatoza zaidi ya asilimia 20 hivyo sisi kazi yetu tunasaidia kutoa elimu na siyo kunufaika zaidi” Amesema Mwaisobwa. Aidha Mwaisobwa amesesitiza kwamba kwa wote ambao walichukua mikopo na wanajificha kukwepa kulipa, watalipa tuu kwa kuwa uhakiki kwa sasa huivi unafanyika ...

KWANINI YANGA HAWATOSALIMIKA KWA SIMBA?

Image
Kwanini Yanga hawatasalimika mbele ya Simba, hizi hapa sababu kadhaa kutoka kwa Omog Kwa mwendo iliyonao Simba ya sasa, ni wazi kwamba usitie mguu maana utavunjika tu! Hii ni kutokana na kasi ya ajabu iliyoanza nayo msimu huu, ikiwa ndiyo timu pekee iliyokusanya pointi nyingi zaidi katika mechi tano za mwanzo. Simba iko kileleni na pointi 13, ikiwa imedondosha pointi mbili tu huku Azam FC na Yanga zikifuatia kwa pointi 10 kila moja, lakini Yanga ina mchezo mkononi. Hata hivyo, Simba imefichua sababu kuu nne ambazo zimeifikisha hapo, ambazo inasema ndizo hizohizo zitakazoiua Yanga wiki ijayo kama ilivyokuwa kwa Azam wikiendi iliyopita walipoichapa bao 1-0. Kabla ya hapo, tayari walikuwa wameshinda mechi dhidi ya Ndanda, Ruvu Shooting na Mtibwa Sugar huku wakitoa suluhu na maafande wa JKT Ruvu. Kocha msaidizi wa Simba, Jackson Mayanja ‘Mia Mia’ ametamba kasi yao ni hiyohiyo kwa mechi zinazokuja ikiwemo ya Oktoba Mosi mwaka huu dhidi ya watani wao wa jadi, Yanga kwenye Uwanja wa T...

UJUE MKANDA WA JESHI

Image
By Dk Emanuel : MKANDA WA JESHI NI NINI ?     Mkanda wa jeshi (shingles) ni jina linalotumika mitaani kuutaja ugonjwa unaoshambulia ngozi na kujenga tabaka la vijipele vikubwa venye majimaji ambavyo mara nyingi hukamata upande mmoja wa mwili . Ingawa vijipele vya mkanada wa jeshi vinaweza kutokea sehemu yo yote ya mwili , mara nyingi hupenda kuota kifuani , shingoni , usoni , mgongoni na mikononi . Vijipele hivi hukaa juu ya ngozi kwa muda wa wastani wa wiki mbili hadi sita kisha hupotea . Vipele vya mkanda wa jeshi huambatana na maumivu makali na kusikia ngozi kuwaka moto. Aghalab ugonjwa huu humrudia mtu zaidi ya mara moja . Mkanda wa jeshi huwapata zaidi watu wenye umri mkubwa , zaidi ya miaka 50, utafiti ukionyesha kuwa zaid ya nusu ya watu wenye umri wa zaidi ya miaka 80 hupatwa na mkanda wa jeshi . Vilevile huwapata zaidi watu waliopatwa na magonjwa yanayopungu...

NGOMA MPYA YA DIAMOND( salome)

ingia hapa kupakua ngoma mpya ya salome , ( traditional) aliyo imba diamond platinum, nime kuwekea hapa mtu wangu wa muhimu ,  click here ku downlodge >>> > https :// mkito .com /s ong/13465   pia tangaza nasi  piga 0766605392

TAMBUA SIKU ZA HATARI

Image
By docta EM ANUEL : ZITAMBUE SIKU ZA HATARI ZA KUSHIKA MIMBA{ NAJIBU MASWALI YA WENGI NA MMOJA WA MDAU WANGU KUTOKA KATIKA POST ILIYOPITA NAONA WENGI HAWAKUELEWA VYEMA ILA KWA SASA NIMEFAFANUA VYEMA KABISA} Nimeamua kuandika makala hii ili kujibu swali la moja wa mdau wa Wangu mmoja ambaye ameuliza kwamba, anahitaji kushika mimba na je, kwa mfano mwezi huu alianza period yake tarehe 17 Juni, ni zipi siku zake za kushika mimba? Ndugu mdau kwanza kabisa nachukua nafasi hii kukuomba samahani kwa kuchelewa kujibu swali lako. Pengine ninapoandika makala hii utakuwa tayari umeshashika mimba, basi kama ni hivyo hakuna tabu bali natumaini swali lako litakuwa limewasaidia wengine ambao pengine wana tatizo kama halo. Pia umeualiza je, ukitaka mtoto wa kike ufanyeje? Nachukua nafasi hii kwanza kujibu swali lako la kwanza kabla sijaenda kwenye swali lako la pili. Kwani kuelewa vyema swali la kwanza kutasaidia kuelewa swali la pili pia. Inafaa tufahamu kuwa ili kuweza kujua ni siku zipi za mwezi mw...

MASHELE BLOG: MPYA:HII HAPA LIST YA VYUO VILIVYOTOA SELECTION YA...

MASHELE  BLOG: MPYA:HII HAPA LIST YA VYUO VILIVYOTOA SELECTION YA... : Habari yako , Masshele blog , tumedhamiria kuwapa vitu roho inapenda hap tembelea blog hii mara kwa mara upate habari za uhakika

STAA TANZANIA AKIRI SIMBA IPO VIZURI

Image
Kiungo wa Azam FC, Himid Mao, amekubali yaishe baada ya kusema kuwa kikosi cha Simba msimu huu kipo vizuri ukilinganisha na msimu uliopita. Mao aliyasema hayo baada ya juzi Jumamosi Simba kuitembezea kichapo cha bao 1-0 Azam FC katika mchezo wa Ligi Kuu Bara kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam. Akizungumza na Championi Jumatatu, Mao alisema kuwa msimu huu kikosi cha Simba kipo vizuri na hiyo ni kutokana na usajili waliofanya. “Tulipambana sana uwanjani lakini mwisho wa siku Simba ndiyo walioibuka na ushindi, nawapongeza kwa hilo lakini pia nimegundua kuwa kikosi chao safari hii kipo vizuri. “Hata hivyo tumekipokea kipigo hicho kwa mikono miwili, upungufu wote uliojitokeza katika mchezo huo, najua kocha atakuwa ameuona na ataufanyia kazi ili kuhakikisha tunafanya vizuri katika mechi zetu nyingine kwa sababu kupoteza mchezo huo siyo kwamba ligi imeisha, tunatakiwa kushinda michezo yetu mingine iliyobakia,” alisema Mao.