Posts

Showing posts from December, 2023

Dalili za mwanamke asiyekupenda

Image
  Unapokuwa  kwenye mahusiano ya kimapenzi  mwanamke ambaye hakupendi kwa dhati basi utamgundua kwa dalili zifuatazo; 1. Hataki kuambata na wewe katika matembezi na ikitokea anakuwa mtu wa masharti mara akuambie tangulia nakuja au pengine kutembea nawe kwa umbali. 2. Anapata kigugumizi kukutambulisha kwa rafiki zake na ndugu na inapotokea amebanwa hafikishi ujumbe kwa kiwango timilifu. 3. Haoneshi kubana matumizi kwa ajili ya maendeleao, kwake ni kufuja mali na anapokosa kupewa pesa ni mwepesi kulalamika na wakati mwingine kununa kabisa. 4. Anaahilisha mara kwa mara kukutana na wewe tena bila kukueleza sababu za msingi Au kukutungia uongo wa dhahili na kuusisitiza bila kuona aibu. 5. Anapokuwa akitoa maelezo ya mwanaume amtakaye sifa zake zinakuwa hayalingani na wewe. Anaweza kukuambia napenda kuishi na mwanaume mwenye gari au mwenye mwili mkubwa, sifa ambazo wewe huna! 6. Hacheki kwa furaha hata kama ukimchekesha haoneshi furaha ya moyoni. Tena mara nyingine anakuwa mkim...

FAIDA KULA MACHUNGWA KIAFYA

Image
  Utangulizi Chungwa ni tunda la mchungwa. Ni kati ya matunda yanayovunwa sana duniani. Jina la kisayansi ni Citrus aurantium L. var. sinensis L. au Citrus sinensis (L.) Osbeck. Ni jamii ya matunda aina ya citrus. Jamii hii ya matunda inajumuisha machungwa, machenza, tangerine, clementine n.k. Tunda lenyewe ni kijani na rangi inabadilika kuelekea njano ikiiva. Pamoja na limau, danzi, balungi na ndimu ni mojawapo kati ya matunda chungwa. na yanapatikana kwa wingi na urahisi sehemu mbalimbali hapa nchini. Machungwa ni matunda maarufu sana sehemu mbalimbali duniani ikiwemo Tanzania. Asili yake ni katika Asia ya Kusini-Mashariki ambako lilioteshwa na wakulima. Kuna aina mbili yanayotofautiana kwa ladha ama chungu au tamu. Aina yenye ladha chungu iliwahi kusambaa duniani hivyo jina la Kiswahili limetunza ladha hii hata kama matunda mengi yanayopandwa siku hizi ni aina tamu. Chungwa tamu lilisambaa kote duniani baada ya Wareno kuchukua machipuko yake na kuyapanda k...

USAJILI SIMBA :SIMBA NIKAMA WAMESHINDWA KWA ASANTE KWASI YAJULIKANA ANAMKATABA NALIPULI

Image
Simba inaonekana kama imekwama kumsajili beki Asante Kwasi. Taarifa zinasema, Simba imegundua Kwasi ana mkataba wa miezi saba na Lipuli ya Iringa, jambo ambalo limewakatisha tamaa. Simba ilikuwa imemficha Kwasi jijini Dar es Salaam kusubiri kumalizana naye baada ya wakala wake kusema hakuwa na mkataba na Lipuli. Lakini baada ya kufanya uchunguzi wa kina kupitia kamati yake ya usajili, iliamua kufunga breki ili kutafakari kwanza kuangalia kama inawezekana kujadiliana na Lipuli au kuachana naye. Dirisha dogo la usajili linatarajiwa kufungwa saa sita na dakika moja, na inaonekana umebaki muda mchache Simba kumaliza na Lipuli ingawa ilielezwa kuna juhudi zilikuwa zinafanywa. KUJIUNGA NA KAMPUNI ZA KUBETI Pmbet tanzania app  jisajili  na upakue >> HAPA >> Betway tanzania app  jisajili na upakue >> HAPA >> Gal sport  jisasajili na upakue kwakubofya >>  HAPA >>

Faida 5 Kuu za Kiafya za Kitunguu saumu

Image
  Chanzo cha picha, Getty Images Kitunguu saumu ni kiungo muhimu katika kaya nyingi kwenye mapishi. Pia kinajulikana kwa sifa zake za dawa. Mtaalamu wa Lishe Kerry Torrens anaeleza kwa nini? Kitunguu saumu ni nini? Kitunguu saumu ni moja ya mimea ya zamani zaidi duniani na ni mmea mgumu wa kudumu wa familia ya Liliaceae. Mimea mingine ya familia hii ni pamoja na kitunguu maji na kitunguu cha majani. Wanatofautishwa na harufu ya kupendeza na ladha maalum. Tembe zake zenye mfanano wa weupe hivi ndizo zinazotumika. Umuhimu wa tembe ya kitunguu saumu • 4Kcal / 16KJ • 0.3g protini • 0.0g mafuta • 0.7g wanga • 0.2g fiber • 25mg potasiamu Chanzo cha picha, Getty Images Faida 5 za kitunguu saumu 1.   Ina misombo yenye sifa za dawa. Umaarufu mwingi wa matibabu ya vitunguu ni kutokana na sifa ya allicin iliyomo ndani yake. Madini haya ya salfa huipa kitunguu saumu harufu yake kali na ladha ya kipekee. Kwa bahati nzuri kwa sisi wapishi, hatua ya kukata au kusaga huchochea uzalishaji...

USAJILI TANZANIA: Azam yakamilisha usajili wa mchezaji huyu

Image
  Klabu ya Azam FC imetangaza kukamilisha usajili wa mshambuliaji, Franklin Navarro (24) kutoka kwa vigogo wa Colombia. Navarro anakuwa Mcolombia wa kwanza kucheza kwenye Ligi Kuu ya NBC Tanzania bara.

Pacome akabidhiwa tuzo ya mchezaji Bora wa mwezi

Image
  Shirika la Bima la Taifa (NIC) leo Desemba 18, 2023 limekabidhi mfano wa hundi ya malipo kwa mchezaji bora wa mwezi Novemba 2023 kwa klabu ya Yanga, Pacome Zouzoua yenye thamani ya Tsh 4,000,000/=. Hundi hiyo imekabidhiwa na Mkurugenzi Mtendaji wa NIC Ndg Kaimu Abdi Mkeyenge. NIC ndio wadhamini wa tuzo ya mchezaji bora wa mwezi wa klabu hiyo (NIC Player Month

Rafat na uongozi chipukizi taifa

Image
  Mtoto Rafat Ally Simba ambaye hivi karibuni alitikisa vyombo mbalimbali vya habari nchini baada kuandika na kuzindua kitabu chake cha The First Female President, yaani Rais wa Kwanza Mwanamke sasa ameibukia Chama Cha Mapinduzi CCM na safari hii akiwania nafasi za Mjumbe wa Kamati ya Uendeshaji Chipukizi Taifa Bara na Mjumbe wa Baraza Kuu la UVCCM Taifa. Kwa mujibu wa UVCCM, jina la Rafat mwenye miaka 11 ambaye pia mjumbe wa Kamati ya Uendeshaji ya Chipukizi Tawi la Boko limerudi likiwa nafasi ya pili jambo linalomuhamasisha Mwanachipukizi huyo ambaye pia  ni msemaji wa hadhara, yaani motivational public speaker, kutumia uwezo wake katika kuhamasisha watoto na vijana wenzake kujitambua, kujiamini na kupigania ndoto zao.   Kwa sasa Rafat Ally Simba ni mwanafunzi wa Darasa la sita katika shule ya Msingi Turkish Maarif iliyopo wilaya ya Kinondoni, Mkoani Dar es salaam akihudumu kama kiongozi mkuu wa wanafunzi shuleni hapo. Kariba ya kiungozi  kwa mtoto Rafat ipo kwa da...

Wahanga Hanang wazidi kupokea misaada

Image
  Meneja Uhusianoo wa Umma wa Amsons Gruop Bhoke Rioba(kulia) akikabidhi hundi ya Sh.milioni 100 kwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge na Uratibu, Jenista Mhagama (wa pili kushoto)kwa ajili ya mfuko wa maafa kusaidia waathirika wa mafuriko ya matope yaliyotokea Hanang mkoani Manyara. Kushoto ni Naibu Waziri wa Afya Dk. Mollel. KAMPUNI ya Amsons Group kupitia kampuni zake za Camel Oil na Camel Cement zimekabidhi hundi ya Sh.milioni 100 kwa Serikali kwa ajili ya kusaidia waathirika wa mafuriko ya matope yaliyotokea Hanang mkoani Manyara. Pamoja na pesa hizo Kampuni ya Camel Oil imetoa misaada mbalimbali kama magodoro, maji na mablanketi kwa ajili ya waathirika hao na hiyo ni sehemu ya kampuni kurejesha tabasamu kwa wananchi waliokumbwa na mafuriko hayo yaliyosababisha vifo, majeruhi na uharibifu wa mali. Akizungumza baada ya kukabidhiwa hundi ya milioni 100 pamoja na mahitaji hayo, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge na Uratibu Jenista Mhagama ameishukur...

Ukimapata Mchumba mwenye sifa hizi usimwache aende

Image
  Mahusiano yoyote mazuri yanatengenezwa. Yana hatua za kupita. Hauamki tu asubuhi ukawa na uhusiano mzuri, ni lazima ukubali kujifunza na kufanya maamuzi sahihi ili uweze kufikia malengo yako katika muda muafaka. Wengi wamejikuta wakipoteza muda kwa kushindwa kufanya maamuzi sahihi. Wamejikuta wakiingia kwenye uhusiano bila kujua wanataka nini na matokeo yake kujikuta wakipoteza muda na uhusiano wao unakuwa hauna malengo. Tunafahamu kwa pamoja kwamba, ili ufikie kwenye hatua ya ndoa ni lazima upitie hatua mbalimbali. Urafiki, uchumba na hatimaye muingie kwenye hatua ya ndoa. Ukikosea kwenye moja ya hatua hizo lazima upate madhara mbele ya safari. Mchumba mzuri ana sifa gani? Utamjuaje? Hili ndiyo darasa la leo na hapa chini utakwenda kupata elimu, twende sambamba. Mchumba mzuri ni yule ambaye tangu awali anaonesha kujitambua, anajua nini anapaswa kufanya kwa wakati muafaka. Aina au mfumo wa maisha yake unauona kabisa tangu mwanzoni kwamba huyu amekomaa kiakili, anayatamani maisha ...

Simba kufa kupona Uarabuni Leo

Image
  MASTAA wa Simba wameapa kupigana kufa na kupona ili kuhakikisha timu yao inapata matokeo mazuri katika mchezo wao wa ugenini dhidi ya Wydad Casablanca ya nchini Morocco. Simba leo Jumamosi watakuwa na kibarua cha kucheza na Wydad Casablanca ambao hawajapata matokeo katika mchezo wowote wa makundi ya michuano hiyo. Akizungumza na Championi Ijumaa, Nahodha wa Simba, Mohamed Hussein ‘Tshabalala’ alisema kuwa, wanatambua ugumu wa mchezo huo kutokana na matokeo mabaya ya mpinzani wao lakini hata kwa upande wao hawajapata matokeo mazuri jambo ambalo linawasukuma na wao kupambana ili kuipa timu ushindi. “Tunafahamu kuwa wapinzani wetu wapo katika hali mbaya kwa kuwa hawajapata matokeo yoyote ya ushindi kwenye hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa hivyo lazima mechi iwe ngumu. “Hata sisi kwa upande wetu hatujapata matokeo ambayo tuliyataka hivyo lazima tuhakikishe kuwa tunapata matokeo ili tuweze kufika mbali, malengo yetu sio kupoteza mchezo wowote bali ni kushinda,” alisema Tshabalala. ...

Maswali ya interview Na majibu yake

  INTERVIEW QUESTIONS & ANSWERS . Question 1. Tell us more about yourself? : Answer: I am hard worker, passionate, consistent and disciplined. . . Question 2. Why do you think you are the best candidate for the job? . Answer: I am a very committed worker, I love challenges and I have the will to succeed. I am a motivated person. I have the ability to learn fast which will facilitate the training period. . . Question 3. Why do you apply for this position? . Answer: Because I am looking for a job. I want to advance my career / experience in a position that allows me to grow as person and employee. . . Question 4. What are your strengths? . Answer: I can work under a lot of pressure. I am an amazing problem solver. I am a persistence person and I don’t give up very easily. My dependability. I can make a decision under a lot of pressure (good decision maker) I can be able to work with little/no supervision, willing to learn new things, easy to adapt, friendly, reliable, expressive ...

Serikali kugharamia mazishi waliofariki kwa mafuriko Hanang

Image
  Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akipita katika moja ya maeneo yaliyoathiriwa na mafuriko katika kijiji cha Gendabi, Katesh mkoani Manyara. Majaliwa yupo mkoani humo kujionea hali ya athari iliyosababishwa na mafuriko. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amemuelekeza Waziri Mkuu, Mhe. Kassim Majaliwa kuwa serikali igharamie mazishi ya wote waliopoteza maisha kutokana na mvua kubwa iliyotokea na mafuriko katika Halmashauri ya Wilaya ya Hanang. Rais Samia pia ametaka majeruhi wote ambao wapo kwenye hospitali mbalimbali wapate matibabu yote yanayostahili kwa gharama za Serikali, huku vyombo vya ulinzi na usalama vikiendelea kutoa msaada wa dharura na uokoaji. Taarifa ya Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Zuhura Yunus imebainisha kuwa Rais Samia ameelekeza Serikali ya Mkoa na Kitengo cha Maafa cha Ofisi ya Waziri Mkuu kuhakikisha wananchi wote ambao makazi yao yamesombwa na maji wapate makazi ya muda kwa ajili ya kuwastiri wananchi hao Maafa haya yameathiri mji wa...