Rafat na uongozi chipukizi taifa

 

Mtoto Rafat Ally Simba ambaye hivi karibuni alitikisa vyombo mbalimbali vya habari nchini baada kuandika na kuzindua kitabu chake cha The First Female President, yaani Rais wa Kwanza Mwanamke sasa ameibukia Chama Cha Mapinduzi CCM na safari hii akiwania nafasi za Mjumbe wa Kamati ya Uendeshaji Chipukizi Taifa Bara na Mjumbe wa Baraza Kuu la UVCCM Taifa.
Kwa mujibu wa UVCCM, jina la Rafat mwenye miaka 11 ambaye pia mjumbe wa Kamati ya Uendeshaji ya Chipukizi Tawi la Boko limerudi likiwa nafasi ya pili jambo linalomuhamasisha Mwanachipukizi huyo ambaye pia  ni msemaji wa hadhara, yaani motivational public speaker, kutumia uwezo wake katika kuhamasisha watoto na vijana wenzake kujitambua, kujiamini na kupigania ndoto zao.

 

Kwa sasa Rafat Ally Simba ni mwanafunzi wa Darasa la sita katika shule ya Msingi Turkish Maarif iliyopo wilaya ya Kinondoni, Mkoani Dar es salaam akihudumu kama kiongozi mkuu wa wanafunzi shuleni hapo.
Kariba ya kiungozi  kwa mtoto Rafat ipo kwa damu ambapo mbali na masomo Binti huyo ni mwana mazingira, ambaye anaamini kuwa maisha ya usoni hasa kwa watoto yatategemea sana ni jinsi gani mazingira yanatunzwa kwa sasa.
 

Comments

Popular posts from this blog

HIZI HAPA SMS TAMU ZA KUMTAKIA USIKU MWEMA MPENZI WAKO

SMS na MESEJI 900+ za mapenzi

MIAKA 22 SASA TANGU KUZAMA KWA MELI KUBWA YA MV BUKOBA, TANZANI TUMEJIFUNZA NINI?