TAMISEMI : TANGAZO LA MAJINA YA WALIOITWA KAZINI AWAMU YA PILI
.jpeg)
TANGAZO LA KUITWA KAZINI Ofisi ya Rais – Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR-TAMISEMI) inapenda kuwataarifu waombaji kazi wa nafasi mbalimbali za kada za afya waliowasilisha maombi katika kipindi cha mwezi wa April, 2023 kuwa mchakato wa kuwapangia vituo vya kazi umekamilika kwa awamu ya pili. Awamu hii ni kwa ajili ya kujaza nafasi wazi za Watumishi waliokosekana wakati wa uchambuzi wa maombi ya awali. Mwezi Aprili, 2023; Ofisi ya Rais – TAMISEMI ilipata kibali cha ajira ya watumishi 8,070 wa Kada mbalimbali za Afya. Baada ya mchakato wa ajira kukamilika, jumla ya waombaji wa ajira wenye sifa wa kada za afya 5319 walipangiwa vituo vya kazi. Aidha, jumla ya nafasi 2,751 za kada ya afya zilikosa waombaji wenye sifa. Kada hizo ni Daktari Bingwa, Daktari Msaidizi, Daktari wa Meno, Daktari wa Meno Msaidizi, Dobi, Fiziotherapia, Fundi Sanifu Vifaa Tiba, Mteknolojia Macho, Mteknolojia Mionzi, Mteknolojia meno, Mteknolojia Msaid...