TAMISEMI : TANGAZO LA MAJINA YA WALIOITWA KAZINI AWAMU YA PILI

 



TANGAZO LA KUITWA KAZINI

Ofisi ya Rais – Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR-TAMISEMI) inapenda 

kuwataarifu waombaji kazi wa nafasi mbalimbali za kada za afya waliowasilisha 

maombi katika kipindi cha mwezi wa April, 2023 kuwa mchakato wa kuwapangia 

vituo vya kazi umekamilika kwa awamu ya pili. Awamu hii ni kwa ajili ya kujaza nafasi 

wazi za Watumishi waliokosekana wakati wa uchambuzi wa maombi ya awali.

Mwezi Aprili, 2023; Ofisi ya Rais – TAMISEMI ilipata kibali cha ajira ya watumishi 8,070 wa 

Kada mbalimbali za Afya. Baada ya mchakato wa ajira kukamilika, jumla ya waombaji wa 

ajira wenye sifa wa kada za afya 5319 walipangiwa vituo vya kazi. Aidha, jumla ya nafasi 

2,751 za kada ya afya zilikosa waombaji wenye sifa. Kada hizo ni Daktari Bingwa, Daktari 

Msaidizi, Daktari wa Meno, Daktari wa Meno Msaidizi, Dobi, Fiziotherapia, Fundi Sanifu 

Vifaa Tiba, Mteknolojia Macho, Mteknolojia Mionzi, Mteknolojia meno, Mteknolojia Msaidizi 

Macho, Mteknolojia Msaidizi Meno, Muuguzi ngazi ya cheti na Tabibu Msaidizi.

Tarehe 31 Mei, 2023, kwa barua yanye Kumb Na. CCD.129/215/01/61 Ofisi ya Rais –

TAMISEMI iliomba kubadili nafasi pamoja na kibali cha kuongezewa muda wa miezi miwili 

kuajiri watumishi kwa nafasi 77 za kada za Fundi Sanifu Vifaa Tiba na Fiziotherapia

zilizokosekana mwanzo na kubadili nafasi 2,674 ili kuajiri watumishi 1,796 kulingana na 

ukomo wa mishahara uliotengwa.

Waombaji wote walio pata nafasi wanatakiwa kuzingatia maelekezo yafuatayo:-

i) Kuripoti katika vituo vya kazi walivyopangiwa katika muda wa siku kumi na nne 

(14) kuanzia tarehe ya tangazo hili. Aidha, waombaji watakaoshindwa kuripoti 

kwenye vituo vya kazi ndani ya siku kumi na nne (14) nafasi zao zitajazwa na 

waombaji wengine haraka iwezekanavyo.

ii) Kuwasilisha Vyeti Halisi (Original Certificates) vya Kidato cha Nne, Sita, 

Chuo Kikuu, NACTE na vyeti halisi vya usajili wa mabaraza ya kitaaluma kwa 

ajili ya kuhakikiwa na mwajiri kabla ya kupewa barua ya ajira. 

iii) Waombaji waliopata nafasi za ajira watakaoripoti bila ya kuwa na Vyeti Halisi 

(Original Certificates) vya Kidato cha Nne, Kidato Sita, Chuo Kikuu, NACTE 

na vyeti halisi vya usajili wa mabaraza ya kitaaluma hawatapokelewa.

iv) Waombaji waliopata nafasi za ajira wanajulishwa kuwa hakutakuwa na nafasi 

ya kubadilisha vituo vya kazi walivyopangiwa.

Waombaji wote ambao majina yao hayakuonekana katika tangazo hili, watambue 

kuwa hawakupata nafasi hivyo wasisite kuomba kwa mara nyingine nafasi za kazi 

zitakapotangazwa.

Wakurugenzi wote wa Mamlaka za Serikali za Mitaa wanaelekezwa kuwapokea, 

kuhakiki vyeti na kuwafanyia mafunzo elekezi (Induction Course) kabla ya 

kuwapangia vituo vya kazi.

Orodha ya majina ya waombaji waliopangiwa vituo vya kazi inapatikana kupitia tovuti 

ya OR-TAMISEMI www.tamisemi.go.tz. 

Limetolewa na:

Katibu Mkuu,

Ofisi ya Rais - TAMISEMI,

Mji wa Serikali – Mtumba,

S.L.P. 1923, 

DODOMA.

30 Agosti, 2023

BOFYA >>HAPA>> KUPAKUA MAJINA


Comments

Popular posts from this blog

HIZI HAPA SMS TAMU ZA KUMTAKIA USIKU MWEMA MPENZI WAKO

SMS na MESEJI 900+ za mapenzi

MIAKA 22 SASA TANGU KUZAMA KWA MELI KUBWA YA MV BUKOBA, TANZANI TUMEJIFUNZA NINI?