6 wafariki baada ya kudumbukia kwenye shimo muda mchache kabla ya harusi

 

Takriban watu sita waliokuwa wakipanga kuhuduria harusi wamefariki baada ya kuanguka ndani ya shimo la maji wakati walipokuwa wakicheza densi.

Ajali hiyo imetokea katika Kihunguro, Kaunti Ndogo ya Ruiru viungani mwa mji mkuu Nairobi, Kenya wakati watu hao walipokuwa wakidensi juu ya mwamba wa zege unaofunika kisima cha maji ambao uliporomoka na kuanguka nao ndani ya shimo la maji, vimeripoti vyombo vya habari nchini humo.

Kulingana na Msemaji wa Polisi wa Kiambu, kundi hilo la watu walikuwa wamesimama katika nyumba ya rafiki yao Jumamosi ili kujiburudisha wakati takriban 11 kati yao walikufa maji baada ya zege hilo la mfuniko wa shimo la maji kuporomoka.

Polisi wanasema lazima kisima hicho kilibomoka kutokana na uzito wa watu waliokuwa wamesimama juu yake.

Shughuli ya uokoaji ikiongozwa na kikosi cha zima moto na maafisa kutoka kituo cha polisi cha Kihunguro ilianza baadaye na watu 6 walipatikana wakiwemo wakiwa wamefariki akiwemo mtoto mmoja.

Hata hivyo, polisi wamethibitisha kuwa mmoja wa watoto hao, msichana alithibitishwa kufariki.

Comments

Popular posts from this blog

HIZI HAPA SMS TAMU ZA KUMTAKIA USIKU MWEMA MPENZI WAKO

SMS na MESEJI 900+ za mapenzi

MIAKA 22 SASA TANGU KUZAMA KWA MELI KUBWA YA MV BUKOBA, TANZANI TUMEJIFUNZA NINI?