Posts

Showing posts from January, 2022

TANESCO Yatangaza Mgao wa Umeme Siku 10

Image
SHIRIKA la Umeme nchini (Tanesco) limetangaza rasmi kuanza mgao wa umeme wa siku 10 nchi nzima kuruhusu matengenezi ya mitambo ya kufua umeme kote nchini. Mkurugenzi Mkuu wa Tanesco Maharage Chande ametanganza leo Ijumaa Januari 28, 2022 kuwa mgao huo utaanza hadi Februari Mosi hadi Februari 10 mwaka huu. Taarifa na ratiba ya mgao huo itatolewa kuruhusu watanzania na taasisi kupanga ratiba zao. Kwa mujibu wa Tanesco maboresho katika mtambo wa kufua umeme wa Kinyerezi I na Ubungo III yataongeza uzalishaji kutoka megawati 150 hadi megawati 335

AJIRA 6000 ZA WAALIMU

Image
Rais Samia Suluhu Hassan  amesema  Serikali  ina mpango wa kuajiri walimu  6,000  ili kuwezesha shule zote nchini kuondokana na changamoto ya walimu.   Rais  ameyasema hayo katika siku yake ya kuzaliwa alipokuwa akizungumza kwa njia ya simu na walimu pamoja na wanafunzi wa  Shule ya Sekondari Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam.   “Kwa ujumla mambo ndani ya sekta ya elimu ni mengi mno, kuna ujenzi wa miundombinu, kuna kutoa vifaa vya kusomeshea, kuna kujenga mazingira ya uwezeshaji kwa ujumla, lakini baada ya kujenga madarasa na kuyawekea ‘furniture’ [samani], kinachofuata ni kuongeza ajira ya walimu, nitaongeza walimu 6,000 au 7,000 hivi tutawaongeza na kuwasambaza ili waendane na ujengaji wa madarasa,”  amesema Rais Samia.   Ameongeza kuwa anafahamu kuwa changamoto ipo katika shule za msingi, hivyo ataendelea kuboresha miundombinu ya shule za msingi ikiwemo kuongeza madarasa na samani.   “Changamoto ipo kwenye shule za msingi...

Breaking: Ajali Yaua Wawili na Kujeruhi 8 Kimara Suka

Image
 wawili wamefariki dunia papo hapo na wengine wanane kujeruhiwa kufuatia ajali ya lori lililovamia kituo cha daladala cha Kimara Suka jijini Dar es Salaam leo Januari 28, 2022.   Kamishna Msaidizi wa Jeshi la Polisi Usalama wa Barabarani Taifa, ACP Abdi Isango amefika eneo la tukio, lakini amesema hawezi kutoa taarifa mpaka atembelee hospitali zote ili ajuwe idadi ya majeruhi na waliopoteza maisha.   Mashuhuda wa ajali hiyo wameeleza kuwa chanzo cha ajali hiyo gari hilo lilionekana kupoteza mwelekeo baada ya kufeli breki na kuwapitia watembea kwa miguu waliokuwa eneo hilo hivyo kusababisha vifo vyao na majeruhi. “Mimi nimesimama pembeni naona gari linanifuata na lilikuwa katika spidi kubwa sana niliruka mtaroni ndicho kilichonisaidia bila hivyo sijui,” amesema John Kelvin aliyekuwa amepaki boda boda yake pembeni. “Rafiki yangu mshtuko alikimbia mbio limemkuta huko huko nikamuona anaingia chini ya lori ndio wamemtoa ameshakufa jamani,” amesema. Mmoja wa ndugu wa majeruhi a...

Askari afariki akiwa na mrembo Gesti

Image
  Polisi wameanzisha uchunguzi katika kisa ambapo mwanaume mmoja amefariki katika chumba cha hoteli mjini Ndhiwa Kaunti ya Homa Bay nchini Kenya baada ya kufurahia burudani kati yake na mwanamke mmoja. Kamanda wa polisi katika Kaunti Ndogo ya Ndhiwa Paul Rioba alisema kuwa kisa hicho kilitokea usiku wa Ijumaa, Januari 21, na mwanaume ambaye jina lake haliwezi kutajwa alikuwa afisa wa polisi.  Mwanaume huyo anaripotiwa kuzimia na kufariki wakati wa kushiriki tendo la ndoa na mwanamke ambaye polisi wamethibitisha kuwa na umri wa miaka 25. Kwa mujibu wa polisi, mwanaume huyo alikuwa na umri wa miaka 55. “Mwanaume huyo alifariki akiwa chumbani na mwanamke huyo. Kwa mujibu wa mwanamke huyo ambaye tunamzuilia, mwanaume huyo alizimia na kuaga dunia wakati wa tendo la ndoa,” Rioba alisema. Mwanaume huyo anasemekana kuwasili wa kwanza na kulipia chumba chao cha hoteli huku mwanamke huyo akijiunga naye baadaye.  Katika taarifa aliyoandikisha na polisi, mwanamke huyo alisema kuwa mw...

Watu 200000 wanaoishi na maambukizi bila kujua kusakwa nchi nzima

Image
  MCHAKATO wa kuwapata watu 200,000 waishio na virusi vya Ukimwi bila kujua ni mbinu mojawapo ambayo Wizara ya Afya imesema itaitumia ili kupunguza maambukizi mapya na kufikia malengo ya milenia mwaka 2030. Pamoja na hayo Wizara imesema inakusudia kupunguza idadi ya watoto wachanga wanaozaliwa na maambukizi ya Virusi vya Ukimwi (VVU) kutoka 6000 wanaozaliwa kila mwaka kwa kuhakikisha inamfikia kila mwanamke mwenye ujauzito. Hayo yamesemwa jana Alhamisi Januari 20, 2022 na Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu wakati alipokuwa akizindua mpango mkakati wa miaka mitano ya tafiti na mafunzo katika masuala ya afya ya jamii na lishe. “Nchini Tanzania inakadiriwa watu milioni 1.7 wanaoishi na Virusi vya Ukimwi lakini wanaotambua hali zao za afya ni milioni 1.5 pekee, hii ni changamoto kwetu lazima tuwatafute hawa 200,000 kwani ndiyo wanaochangia maambukizi mapya bila kujua. “Tutawapata hawa kwa kuwashauri na kuhamasisha ili wapime kupitia mtaa kwa mtaa, kata kwa kata, halmashauri kwa halmashauri l...

Mgonjwa Mahututi Aamka Baada Kupewe Dawa ya Kuongeza Hisia za Ngono

Image
KATIKA kile kimetajwa kama hatua kubwa kwenye tasnia ya utabibu, muuguzi mmoja kutoka nchini  Uingereza  ambaye alikuwa akipigania maisha yake hospitalini, aliamka baada ya kupoteza fahamu kwa siku 28.   Mwanamke huyo aliamka baada ya kupewa dozi moja ya dawa ya kuongeza hisia za kingono zijulikanazo kama ( viagra ).   Kulingana na vyombo vya habari vya Uingereza, Monica Almeida, (37), alilazwa hospitalini Novemba 9, 2021, baada ya kuambukizwa virusi vya COVID-19 mnamo Oktoba 19, 2021, licha ya kuchanjwa kikamilifu dhidi ya virusi hivyo.   Hata hivyo, baada ya kulazwa hospitalini, alipoteza hisia ya ladha na kunusa kwa siku nne kisha alianza kukohoa damu na viwango vyake vya oksijeni kushuka huku hali yake ikiendelea kudhoofika, na kupelekwa katika chumba cha wagonjwa mahututi(ICU) cha Hospitali ya Lincoln County ambapo aliingia katika hali ya kutokuwa na fahamu mnamo November 6, 2021.   Akiwa amebakiwa na saa 72 tu kabla ya mashine yake ya kumsaidia kupumu...

CCM YAMPITISHA DKT TULIA KUWANIA USPIKA

Image
  Kamati Kuu ya Chama cha Mapinduzi (CCM), leo Alhamisi Januari 20, 2022 imempitisha Naibu Spika wa Bunge, Dk. Tulia Ackson kuwania nafasi ya uspika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kurithi nafasi ya Job Ndugai aliyejiuzulu. Kikao cha Kamati Kuu ya CCM kimeketi leo katika Ukumbi wa White House jijini Dodoma na kuongozwa na Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan ambapo Dk. Tulia ameibuka kinara kati ya wagombea 70 waliojitokeza. Akizungumza jijini Dodoma katibu wa NEC Itikadi na Uenezi CCM Shaka Hamdu Shaka baada ya kikao hicho amesema hatua inayofuata ni jina hilo kupigiwa kura na Caucas ya wabunge wa chama hicho. Kikao hicho cha kamati kuu, kimekuwa na jukumu zito la kuwafyeka wagombea 69 kati ya 70 waliojitosa kwenye kinyanyany’iro hicho na kubaki na jina moja la Tulia ambalo litapelekwa katika kamati ya wabunge wa CCM ili kudhibitishwa. Kamati ya wabunge wa CCM, itakuwa na jukumu la kumchagua na atakwenda kukiwakilisha chama ...

NECTA MATOKEO YA MTIHANI KIDATO CHA NNE MLAMBAI SECONDARY

        Fungua >> hapa >> kuona matokeo ya kidato cha nne 2021 , shule ya sekondary mlambai

MWANAFUNZI BORA MATOKEO KIDATO CHA NNE 2021 ATAJA SIRI YA USHINDI

Image
  Dar es Salaam. Mwaka umeanza vizuri kwa binti Consolata Prosper baada ya kutangazwa kuwa mwanafunzi bora wa mtihani wa kidato cha nne mwaka 2021 kutoka Shule ya Sekondari ya St Francis Girls iliyopo mkoani Mbeya.  Katika matokeo ya mtihani huo yaliyotangazwa leo Januari 15, 2022 na Baraza la Mitihani la Taifa (Necta) Prosper ndiyo mwanafunzi aliyefaulu vizuri zaidi kati ya wanafunzi 483,820 waliofanya mtihani huo mwishoni mwa mwaka jana.  Binti huyo mwenye miaka 16  ameuambia mtandao huu kuwa moja ya silaha zilizomwezesha kuwa bora zaidi ni maombi.  Wakati matokeo hayo yanatangazwa binti huyo alikuwa akisikiliza nyimbo za injili huko  nyumbani kwao Salasala jijini Dar es Salaam.  “Sikutarajia. Nilikuwa na uhakika kuwa sitofeli lakini sikutarajia kama nitaogoza pia,” Consolata ameiambia Nukta Habari baada ya kuulizwa amepokeaje matokeo hayo.  Mwaka umeanza vizuri kwa binti Consolata Prosper baada ya kutangazwa kuwa mwanafunzi bora ...

SHULE KUMI BORA MATOKEO KIDATO CHA NNE

Image
  Dar es Salaam. Baraza la Mitihani la Taifa (Necta) limetangaza matokeo ya mtihani wa kidato nne mwaka 2021 na kuzitaja shule 10 zilizofanya vizuri huku Shule ya Sekondari ya  Kemebos  ya mkoani Kagera ikishika nafasi ya kwanza kitaifa. Kemebos imepanda kutoka nafasi ya nne iliyoshika katika matokeo ya mwaka juzi na kuishusha Shule ya Sekondari ya St Francis ya mkoani Mbeya hadi katika nafasi ya pili. Katika matokeo hayo yaliyotangazwa  leo (Januari 15, 2022) na Katibu Mtendaji wa Necta, Dk Charles Msonde amezitaja shule nyingine nane  zilizofanya vizuri zaidi katika matokeo hayo kuwa ni Waja Boys ya mkoani Geita iliyoshika nafasi ya tatu. Shule ya Sekondari Bright Future Girls ya Dar es Salaam imepenya katika nafasi ya nne,  Bethel Girls (Iringa) katika nafasi ya tano na Maua Seminary mkoani Kilimanjaro ikishikilia nafasi ya sita. Feza Boys ya jijini Dar es Salaam yenyewe imepigana vikali na kujitwaliwa Nafasi ya saba, Precious Blood (Arus...

HAYA HAPA MATOKEO YA KIDATO CHA NNE SHULE ZOTE

Image
  Matokeo ya kidato cha NNE 2021 yametangazwa Leo. Kuona matokeo ya kidato cha NNE 2021 mikoa yote Na shule zote BOFYA >> HAPA >>

HAYA HAPA MATOKEO YA KIDATO CHA PILI 2021

Image
  MATOKEO YA KIDATO CHA PILI WALIOFANYA MTIHANI MWAKA 2021 YANATANGAZWA LEO BOFYA >> HAPA >> KUFUNGUA MAJINA YOTE

MATOKEO YA DARASA LA NNE 2021

Image
  Matokeo ya Darasa la nne 2021 kutoka hivi karibuni Matokeo ya DARASA la NNE 2021 Yametangazwa Leo yatapatikana >> HAPA >> Kuanzia saa nne.  MATOKEO YA DARASA LA NNE MIKOA YOTE TANZANIA BOFYA >> HAPA >>

MATOKEO YA MTIHANI WA FORM 2 2021

Image
  Matokeo ya form two <script type="text/javascript"> atOptions = { 'key' : 'f646ce43109225b1e65e198de120b569', 'format' : 'iframe', 'height' : 50, 'width' : 320, 'params' : {} }; document.write('<scr' + 'ipt type="text/javascript" src="http' + (location.protocol === 'https:' ? 's' : '') + '://observationtable.com/f646ce43109225b1e65e198de120b569/invoke.js"></scr' + 'ipt>'); </script> <script type="text/javascript"> atOptions = { 'key' : 'f646ce43109225b1e65e198de120b569', 'format' : 'iframe', 'height' : 50, 'width' : 320, 'params' : {} }; document.write('<scr' + 'ipt type="text/javascript" src="http' + (location.protocol === 'https:' ? 's' : '') + '://observationta...

MHADHIRI ANAYEFAULISHA WANAFUNZI WAKIKE KWA NGONO ATUPWA JELA

Image
  Picha Mhadhiri wa Chuo Kikuu kimoja nchini Morocco aliyekuwa anatuhumiwa kufaulisha wanafunzi wa kike kwa kufanya nao ngono amehukumiwa kifungo cha jela miaka miwili. Hukumu hiyo ni ya kwanza kutolewa nchini Morocco kwa mtumishi mwandamizi wa kada hiyo kwenye vyuo vikuu vya Morocco. Mhadhiri huyo wa uchumi katika Chuo Kikuu cha Hassan, kilichopo karibu na Casablanca, alitiwa hatiani kwa tabia chafu pamoja na makosa mengine. Wahadhiri wengine wanne wanafikisha mahakamani hii leo kuhusiana na kashfa hiyo ya ufaulu kwa kutoa ngono. Kesi hiyo iliibuliwa na chombo cha habari cha Morocco mwaka jana baada ya waandishi wake kunasa meseji za mapenzi baina ya wanafunzi na wahadhiri.

RAIS SAMIA AKUTANA ANA KWA ANA NA NDUGAI LEO

Image
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, amekutana na kuzungumza na aliyekuwa Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Job Ndugai (Mb) aliyefika Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma.

MWANAFUNZI UDSM AFARIKI KWA KUJIRUSHA GHOROFANI

Image
  Mwanafunzi mmoja aitwaye Manawa Samson Horera (22) ambaye ni Mwanafunzi wa mwaka wa pili kitivo cha shahada ya uhasibu katika Chuo Kikuu cha Dar es salaam (UDSM) amefariki baada ya kuruka kutoka ghorofa ya pili. “Mwanafunzi huyo aliingia kwenye chumba cha Mwanafunzi mwenzake aitwaye Hamza Abdulhaman na kuiba laptop aina ya HP ambapo Hamza na Wanafunzi wengine wakamuona na alipobaini ameonekana na Wanafunzi wenzake aliamua kuruka kupitia dirishani” “Jeshi la Polisi linawataka Wanafunzi kuacha kujihusisha na uhalifu kwani maeneo hayo ya hosteli yamekuwa na malalamiko ya Wanafunzi laptop zao kuibiwa na Watu wanaodhaniwa ni Wanafunzi wenzao suala ambalo linaweza kukatisha masomo yao ikibainika ni Wahalifu” ——— Muliro Jumanne, Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya DSM

POLISI WAELEZA A TO Z BINTI ALIVYOMUUA MAMA YAKE

Image
  SILAHA ya jadi aina ya panga, ni moja ya vifaa vilivyokutwa katika shimo alilofukiwa mtu anayedhaniwa alikuwa muuguzi wa Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya KCMC, Patricia Ibrock (66), anayedaiwa kuuawa na watu watatu akiwemo mwanae wa kumzaa mwaka jana.   Taarifa za awali kutoka Jeshi la Polisi mkoani Kilimanjaro zimedai kuwa, binti huyo alishirikiana kufanya mauaji hayo akiwa na waganga wawili wa jadi kutoka Dar es Salaam na Tanga, huku mmoja wao akidaiwa kuwa na uhusiano wa kimapenzi na binti huyo.   Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro, Simon Maigwa alisema jana kuwa, tukio la mauaji ya mama huyo lilitokea Februari, 2021 nyumbani kwake Kijiji cha Rau Mrukuti, Kata ya Uru Kusini, wilayani Moshi na kwamba jeshi hilo linawashikilia watu watatu akiwemo binti huyo.   “Wakati timu ya uchunguzi inafukua eneo lililofukiwa mwili wa mama huyo tulikuta mabaki ya mwili unaodhaniwa wa Patricia uliokuwa umefungwa na blanketi, vitu vya aina mbalimbali ikiwamo panga amba...