Amteka mpenzi wake akitaka arudishiwe hela alizo honga, amuua

Jeshi la Polisi Mkoani Geita linamshikilia mwanaume mmoja mwenye umri wa miaka 30 kwa tuhuma za kumuua mpenzi wake aitwaye Esta John (28) mkazi wa Ibamba Wilaya Bukombe Mkoani humo ambaye kabla ya kifo chake alitekwa nyara na mpenzi wake. Katika taarifa ya Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Geita Henry Mwaibambe aliyoitoa kwa waandishi wa habari inasema kwamba mwanamke huyo aliondoka nyumbani kwake juni 13 mwaka huu akiwa na mtu aliyesemekana ni mpenzi wake. Baada ya kutoweka kwa muda mwanaume huyo ambaye jeshi la polisi halijamtaja kwa majina yake, alianza kuwapigia simu wazazi wa mwanamke akihitaji kulipwa pesa alizokuwa akimuhudumia kwa ahadi ya kumuoa na kwamba mtuhumiwa alibaini kuwa sio mwaminifu . Kamanda Mwaibambe amesema baada ya taarifa kufika katika vyombo vya usalama upelelezi ulianza mara moja na kufankiwa kumkamata mtuhumiwa huyo akiwa na mali za marehemu ambaye alimteka nyara. “Katika mahojiano alikiri kumteka nyara mwanamke huyo akishinikiza kulipwa gharama alizotumia k...