Posts

Showing posts from October, 2019

AUDIO | Jux Ft. Diamond Platnumz – Sugua | Download

Image
Tanzanian singer,  Jux  has unlocked a new single titled “ Sugua ” featuring WCB Wasafi Records Boss,  Diamond Platnumz . The song, “ Sugua ” serves as the lead single off his new body of work, ‘ The Love ‘ album which houses 18 tracks. In conclusion, Jux new project, ‘ The Love ‘ album features the likes of Diamond Platnumz, Vanessa Mdee, Nyashinski, GNako, Tommy Flavour, Singah, Q Chief, Joh Makini and Ruby. DOWNLOAD

| HEKAYA ZA LOLIONDO | Babu asisitiza dawa ilifanya kazi [Part 2]

Image

| HEKAYA ZA LOLIONDO | Tiba ya Babu wa Loliondo [Part 1]

Image

ISSUING OF GRADUATION GOWNS

Image
       University of Dar es salaam logo   ISSUING OF GRADUATION GOWNS   Attachment :  20191030_025259_UDSM_ISSUING OF GRADUATION GOWNS.pdf

Maajabu ya kioo kiroho jinsi unavyoweza mtumia mtu ndoto za ajabu

Image

The wedding year”: Filamu ya mapenzi iliyojaa visa vya kuchekesha

Image
Inazungumzia mahusiano ya ndoa na  jinsi ya kuishi na mpenzi wako. Imeja visa vingi ambavyo vitakufundisha nini maana ya ndoa.  Dar es Salaam.  Wiki hii, unahitaji kusahau visu, bunduki na kuachana na michezo ya kareti na kurusha mateke.  Badala yake, andaa kitambaa kwa ajili ya kujiziba mdomo pale unapocheka na kufuta machozi wakati filamu ya  The wedding year  itakapokuwa inaonyeshwa katika kumbi mbalimbali kuanzia ijumaa ya leo Oktoba 25. Filamu hii huenda ikawafaa walio na wanaotarajia kuingia kwenye ndoa,kwa sababu ina visa vingi vitakavyokupa funzo lililotukuka. Sarah Hayland (Modern Family) hana mpango wa kuingia kwenye ndoa. Na wala hajioni kama msichana aliye tayari kutulizana kwenye mahusiano. Anapompata kijana  Jake Riddick (let it shine) ambaye yuko tayari kuipanda milima na hata kuvuka bahari kwa mbizi kwa ajili yake, mambo yanaanza kutindinganyika. Mialiko 15 ya kuhudhuria harusi za jamaa zake ndani ya mwaka mmo...

ANNUNAK HAWAKUFA KATIKA GHARIKA LA NUHU

Image

Mfahamu kwa ufupi malkiaTiye

Image

MAJINA YA WATAALAM WA KISWAHILI KUSAMBAZWA OFISI ZA UBALOZI

Image
Da es Salaam. Kama ulipuuzia kujiorodhesha kwenye kanzidata, hii ni habari njema kwa watalaamu wa lugha ya Kiswahili nchini ambao walitii wito huo. Serikali imesema itayasambaza kwenye ofisi mbalimbali za ubalozi majina yaliyoorodheshwa kwenye kanzidata ya Baraza la Kiswahili la Taifa (Bakita). Akizungumza hivi karibu wakati akizindua Mpango wa Kutahmini Uwezo wa Wakalimani katika ukumbi wa Bakita, Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Dk Harrison Mwakyembe alisema tayari kuna wataalamu wa Kiswahili zaidi ya 1,000 ambao Bakita imewatambua kwenye kanzidata yake. Pia,ameliagiza Baraza hilo lianze kuwaingiza kwenye kanzi data wakalimani ambao watakidhi vigezo kwenye kanzidata ya taifa ili watumike watakapohitajika na ikibidi waendelezwe zaidi. Alisema suala la kuwapeleka walimu wa Kiswahili kwenye nchi ambazo zimeomba wataalamu linafanyiwa kazi kwa umakini na shughuli hiyo inakwenda vyema. Alisisitiza kwamba Watanzania watambue kwamba sio rahisi kama watu wengi wana...

Baba aeleza mauaji ya mwanaye yalivyokatisha ndoto kuwa muuguzi

Image
  Songea.  Christopher Kafuru ambaye nibaba wa Beata Kafuru anayedaiwa kuuawa na mpenzi wake amesema mwanaye amekatishwa ndoto ya kuwa muuguzi. Amesema haki inatakiwa kutendeka ili ukweli kuhusu kifo hicho ujulikane na mhusika kuchukuliwa hatua. Kwa mujibu wa kamanda wa polisi mkoani Ruvuma, Simon Maigwa, mtuhumiwa alichukua uamuzi huo baada ya kumtuhumu Beata kuwa na uhusiano wa mapenzi na mtu mwingine. Beata anadaiwa kuuawa na James Paul ambaye ni ofisa wa Takukuru Oktoba 20, 2019 wilayani Tunduru kwa kinachodaiwa ni wivu wa mapenzi. Katika ufafanuzi wake Kamanda Maigwa amesema  mtuhumiwa alikiri kufanya mauaji hayo kwa lengo la kulipiza kisasi na alitumia bastola aina ya Browning na kumpiga  Beata risasi tatu za kichwani ambaye alikufa hapo hapo. Akizungumza na Mwananchi, Kafuru amesema, “hadi sasa nakosa cha kuzungumza, Beata ni mtoto wangu wa pili kati ya watoto wangu wanne. Ningejua kama anakwenda kukatishwa uhai ningemzuia asiru...

Ukweli kuhusu jini mahaba

Image

CHUO KIKUU CHA DAR ES SALAAM (UDSM) KUTOA MITIHANI YA KISWAHILI KIMATAIFA

Image
Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Dk.Leonard Akwilapo akizungumza jijini Dodoma leo na Wandishi wa habari wakati akitoa taarifa ya kuanzishwa kwa mitihani ya Kimataifa ya Ujuzi wa Lugha ya Kiswahili na Chuo kikuu cha Dar es Salaam kuanzia Januari,mwaka  2020 katikati ni Mkurugenzi wa Taasisi ya Confucius, Prof.Aldin Kai Mutembei Mkurugenzi wa Taasisi ya Confucius Prof.Aldin Kai Mutembei,akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dodoma kuhusiana na kuanzishwa kwa mitihani ya Kimataifa ya Ujuzi wa Lugha ya Kiswahili na Chuo kikuu cha Dar es Salaam kuanzia Januari,mwaka  2020 Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Bi.Sylvia Lupembe,akifafanua jambo kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) mara baada ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Dk.Leonard Akwilapo,kutangaza kwa Chuo Kikuu cha Dar Es Salaam kuanzisha mitihani ya Kimataifa ya Ujuzi wa Lugha ya Kiswahili inayotarajia kuanza Januari,mwaka  2020 Katibu...

TANGAZO MUHIMU KWA WANAFUNZI WA MWAKA WA KWANZA 2019-2020

Image
  TANGAZO MUHIMU KWA WANAFUNZI WA MWAKA WA KWANZA 2019/2020 Angalia kiambatanisho kupata taarifa kamili   Attachment :  20191021_024818_UDSM_TANGAZO MUHIMU KWA WANAFUNZI WA MWAKA WA KWANZA 2019-2020.pdf

Tanzania yapendekeza Kiswahili kuwa lugha rasmi ya UN

Image
Iwe miongoni mwa lugha rasmi za chombo hicho chenye wanachama 193. Kama Kiswahili kitakubaliwa, itakuwa ni lugha ya saba rasmi ya UN baada ya Kiarabu, Kichina, Kiengereza, Kirusi, Kifaransa na Kihispania. Kiswahili ni lugha rasmi kwenye Umoja wa Afrika (AU), Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) na Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC). Dar es Salaam.  Wakati vikao vya kamati ya nne ya Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa (UN) vikiendelekea nchini Marekani, Tanzania imeendelea kuipigia chapuo lugha ya Kiswahili iwe miongoni mwa lugha rasmi za chombo hicho chenye wanachama 193. Akihutubia kikao hicho jana (Oktoba 21, 2019), mwakilishi wa kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa,  Balozi Modest Mero amesema wito huo wa Taifa lake unazingatia ukweli kuwa Kiswahili hivi sasa ni lugha ya kiafrika inayozungumzwa na takribani watu milioni 500 kote duniani. “Na kama hiyo haitoshi tayari lugha ya Kiswahili ni lugha rasmi kwenye Umoja wa Afrika (AU), Jumuiya ...

VAN DIJK APAMBANISHWA NA MESSI NA RONALDO KUWANIA BALLON D'OR

Image
NYOTA Cristiano Ronaldo, Lionel Messi, Mohamed Salah, Sadio Mane NA Virgil van Dijk wameingia kwenye orodha ya wachezaji 30 wanaowania tuzo ya Mwanasoka Bora wa Dunia, Ballon d'Or iliyotangazwa Ufaransa jana.   Mane na Van Dijk ni miongoni mwa wachezaji saba wa Liverpool katika orodha hiyo ambao wanaungana na nyota wengine wa Ligi Kuu ya England, Sergio Aguero, Bernardo Silva na Pierre-Emerick Aubameyang.  Wachezaji wengine wa Liverpool ni Salah, Roberto Firmino, Alisson, Georginio Wijnaldum na Trent Alexander-Arnold ambao wote walikuwemo kwenye kikosi cha timu hiyo kilichotwaa taji la saba la Ligi ya Mabingwa.  Ronaldo na Messi wote watakuwa wakiwania tuzo ya sita ya Ballon d'Or, wawili hao wakitarajiwa kuchuana tena msimu huu, huku mshindi wa tuzo hiyo mwaka jana,  Luka Modric akikosekana kwenye orodha hiyo ya watu 30. Beki Virgil van Dijk wa Liverpool na Uholanzi ameteuliwa kuwania tuzo ya Ballon d'Or mwaka huu   NYOTA 30 WANAOWANIA BALLON D'OR...

Maajabu ya kulala chali na uhusiano wake na ulimwengu wa kiroho

Image

PETE YA MFALME SULEIMAN IPO MLIMA KILIMANJARO ALIYOICHUKUA MENELIK 1

Image

Ukweli kuhusu Rozari na sala yake

Image

Rhapta jiji lililozama baharini miaka 2000 iliyopita nchini Tanzania

Image

Vita ya waganga na wachawi

Image

Aina ya tahajudi na jinsi ya kufanya

Image

Jinsi ya kutoka nje ya mwili na jicho la tatu#hmglife new style

Image

Jinsi ya kufanya tahajudi ya mtoto wa ndani na nk

Image

Wageni kutoka sayari nyingine wanaoleta teknolojia na kutawala dunia

Image

kijiji kinachoongoza kwa uchawi duniani ni balaa

Image

Hisabati, Kiingereza bado pasua kichwa mitihani darasa la Saba Tanzania

Image
Ufaulu wa Hisabati washuka kidogo kwa asilimia moja ikilinganishwa na mwaka jana. Kiingereza ndiyo somo ambalo lina ufaulu mdogo zaidi huku wadau wakiomba juhudi zaidi kufanyika kuwaokoa watoto. Dar es Salaam.  Kwa mara nyingine Baraza la Mitihani la Taifa (Necta) limetangaza matokeo ya mtihani wa kumaliza elimu ya msingi (PLSE) au maarufu kama darasa la Saba huku yakionesha kuwa ufaulu umeongezeka kwa takriban asilimia 4 kutoka mwaka jana. Hata hivyo, Katibu Mtendaji wa Necta, Dk Charles Msonde aliwaambia wanahabari kuwa pamoja na matokeo hayo, ufaulu wa masomo ya Kiswahili, Maarifa ya Jamii, Kiingereza na Sayansi ulipanda kati ya asilimia 1.83 hadi asilimia 6.86. Wakati ufaulu wa masomo hayo ukipanda, Kiingereza na Hisabati yameendelea kuwa pasua kichwa. Safari hii ufaulu wa Hisabati umeshuka kidogo kwa asilimia moja ikilinganishwa na mwaka 2018. Katika matokeo yaliyotangazwa jana (Oktoba 15, 2019) Hisabati ina wastani wa ufaulu wa takriban asilimia 65 ikilinganis...

KISWAHILI CHAPENDEKEZWA KUTUMIKA KATIKA NCHI ZA UKANDA WA MAZIWA MAKUU

Image
Brazzaville, Katika jitihada za kukuza lugha ya Kiswahili barani Afrika, Tanzania imeziomba nchi wanachama wa ukanda wa maziwa makuu kuanza kutumia lugha ya Kiswahili kama lugha rasmi na lugha ya kazi Wito huo umetolewa katika mkutano wa mawaziri wa mambo ya nje wa nchi wanachama wa ukanda wa maziwa makuu, uliofanyika mjini Brazzaville leo na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dkt. Damas Ndumbaro   "Tumewaomba wenzetu wa maziwa makuu wakubali lugha ya Kiswahili kutumika kama lugha rasmi na lugha ya kazi katika nchi zote za maziwa makuu. Pia nchi sita ambazo zipo hapa na hazijaridhia mabadiliko ya mkataba wa Afrika kuruhusu Kiswahili kutumika kama lugha rasmi katika Afrika (AU) nchi hizo zimetuhakikishia kuwa zitaridhia mabadiliko hayo ili kuhakikisha kuwa Kiswahili kinaanza kutumika kama lugha rasmi ya kazi," Alisema Dkt. Ndumbaro Kwa mujibu wa Waziri Ndumbaro, matumizi ya lugha ya Kiswahili katika ukanda huo ni fursa ambayo it...

Mvua kubwa yaja tena, TMA yatoa tahadhari ya siku mbili

Image
Mvua hiyo kubwa inaratajia kunyesha katika mikoa ya Dar es Salaam, Pwani, Tanga, visiwa vya Unguja na Pemba. Mvua hiyo inatarajia kunyesha Oktoba 17 hadi 18, 2019 Changamoto zinazoweza kutokea ni pamoja na changamoto za usafiri na kusimama kwa baadhi ya shughuli za watu hasa za kiuchumi. Dar es Salaam.  Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imetoa angalizo la mvua kubwa inayoweza kunyeshja katika baadhi ya maeneo ya mikoa ya ukanda wa pwani ya kaskazini ikiwemo Dar es Salaam kwa siku mbili kuanzia kesho Oktoba 17 Angalizo hilo linahusisha mikoa ya Tanga, Dar es Salaam, Pwani, visiwa vya Unguja na Pemba pamoja na kaskazini mwa mkoa wa Morogoro ambapo mvua kubwa za muda mfupi zinatarajiwa kunyesha. K atika taarifa yake iliyotolewa jana (Oktoba 15, 2019), TMA imesema uwezekano wa kutokea kwa mvua hizo ni wa wastani na hata kiwango cha athari zinazoweza kutokea ni cha wastani pia. Mamlaka hiyo imeeleza baadhi ya changamoto zinazoweza kutokea ni pamoja na changamoto ...