Mvua kubwa yaja tena, TMA yatoa tahadhari ya siku mbili
Mvua hiyo kubwa inaratajia kunyesha katika mikoa ya Dar es Salaam, Pwani, Tanga, visiwa vya Unguja na Pemba.- Mvua hiyo inatarajia kunyesha Oktoba 17 hadi 18, 2019
- Changamoto zinazoweza kutokea ni pamoja na changamoto za usafiri na kusimama kwa baadhi ya shughuli za watu hasa za kiuchumi.
Dar es Salaam. Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imetoa angalizo la mvua kubwa inayoweza kunyeshja katika baadhi ya maeneo ya mikoa ya ukanda wa pwani ya kaskazini ikiwemo Dar es Salaam kwa siku mbili kuanzia kesho Oktoba 17
Angalizo hilo linahusisha mikoa ya Tanga, Dar es Salaam, Pwani, visiwa vya Unguja na Pemba pamoja na kaskazini mwa mkoa wa Morogoro ambapo mvua kubwa za muda mfupi zinatarajiwa kunyesha.
Katika taarifa yake iliyotolewa jana (Oktoba 15, 2019), TMA imesema uwezekano wa kutokea kwa mvua hizo ni wa wastani na hata kiwango cha athari zinazoweza kutokea ni cha wastani pia.
Mamlaka hiyo imeeleza baadhi ya changamoto zinazoweza kutokea ni pamoja na changamoto za usafiri na kusimama kwa baadhi ya shughuli za watu hasa za kiuchumi.
“Baadhi ya makazi kuzungukwa na maji, ucheleweshwaji wa usafiri, kusimama kwa muda kwa baadhi ya shughuli za kiuchumi na kijamii,” inasomeka sehemu ya taarifa hiyo.
Mvua hizo kubwa za vipindi vifupi zinatarajiwa kunyesha kesho Oktaba 17 na 19.
Hata hivyo, wananchi wanashauriwa kuendelea kufuatilia taarifa za utabiri kutoka TMA na kuzingatia tahadhari zilizotolewa na marejeo yake pamoja na kupata na kuzingatia ushauri na miongozo ya wataalam katika sekta husika ili kupunguza athari zinazoweza kujitokez
a
a
Comments
Post a Comment