The wedding year”: Filamu ya mapenzi iliyojaa visa vya kuchekesha


  • Inazungumzia mahusiano ya ndoa na  jinsi ya kuishi na mpenzi wako.
  • Imeja visa vingi ambavyo vitakufundisha nini maana ya ndoa. 

Dar es Salaam. Wiki hii, unahitaji kusahau visu, bunduki na kuachana na michezo ya kareti na kurusha mateke. 
Badala yake, andaa kitambaa kwa ajili ya kujiziba mdomo pale unapocheka na kufuta machozi wakati filamu ya The wedding year itakapokuwa inaonyeshwa katika kumbi mbalimbali kuanzia ijumaa ya leo Oktoba 25.
Filamu hii huenda ikawafaa walio na wanaotarajia kuingia kwenye ndoa,kwa sababu ina visa vingi vitakavyokupa funzo lililotukuka.
Sarah Hayland (Modern Family) hana mpango wa kuingia kwenye ndoa. Na wala hajioni kama msichana aliye tayari kutulizana kwenye mahusiano. Anapompata kijana  Jake Riddick (let it shine) ambaye yuko tayari kuipanda milima na hata kuvuka bahari kwa mbizi kwa ajili yake, mambo yanaanza kutindinganyika.



    Mialiko 15 ya kuhudhuria harusi za jamaa zake ndani ya mwaka mmoja, hotuba kwenye harusi za marafiki na dada zake ni vionjo tu ambavyo utakutana navyo kwenye filamu hiyo lakini angalia usiondolewe kwenye kumbi kwa kushindwa kujizuia kucheka.
    Tembelea Mlimani City, Aura mall na Mkuki house kujionea filamu hii iliyoongozwa na Robert Luketic ambaye pia ni kichwa nyuma ya kazi kama Monster in Law na Legally Blonde
    .

    Comments

    Popular posts from this blog

    HIZI HAPA SMS TAMU ZA KUMTAKIA USIKU MWEMA MPENZI WAKO

    SMS na MESEJI 900+ za mapenzi

    MIAKA 22 SASA TANGU KUZAMA KWA MELI KUBWA YA MV BUKOBA, TANZANI TUMEJIFUNZA NINI?