SIMBA YAUA 3-1 KAGERE HAKAMATIKI AWEKA MBILI

MABINGWA watetezi, Simba SC wameanza vyema msimu mpya wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara baada ya ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya JKT Tanzania jioni ya leo Uwanja wa Uhuru mjini Dar es Salaam. Mshambuliaji wa kimataifa wa Rwanda, Meddi Kagere alikaribia kufunga hat trick katika mechi ya kwanza baada ya kufunga mabao mawili, huku lingine likifungwa na Miraj Athumani ‘Madenge’ aliyerejeshwa kikosini msimu huu. Kocha Mbelgiji, Patrick Aussems leo aliwaanzisha wachezaji wapta, Wabrazil Tairone Santos na Gerson Fraga kucheza pamoja safu ya ulinzi kwa mara ya kwanza tangu wasajiliwe Julai na wakafanya vizuri. Kagere aliye katika msimu wake wa pili Msimbazi tangu asajiliwe kutoka Gor Mahia ya Kenya, alifunga bao la kwanza sekunde ya 20 ya dakika ya kwanza akimalizia pasi ya kiungo Hassan Dilunga kabla ya kufunga la pili dakika ya 59 akimalizia pasi ya kiungo mwingine mzawa, Muzamil Yassin. Kagere alikaribia kukamilisha hat trick dakika ya 65 kama si shuti lake kugonga mwamba – lakini d...