Masshele Kiswahili

-Asili ya kiswahili
Asili ni chimbuko au namna kitu kinavuoanza. Kwa hiyo Asili ya kiswahili ni namna kiswahili kilivyoanza.

Katika kuangalia historia hii kunanadharia mbalimbali zinazoelezea chimbukoa na asili ya lugha hii.

-Kiswahili ni kiarabu
Wapo wataalamu wanaodai lugha hii asili yake ni kiarabu. Na mkazo wao upo kuwa kiswahili kinayo maneno mengi ya kiarabu. Vile vile asili ya neno kiswahili linatokana na neno la kiarabu sahil lenye maana ya pwani. Hata hivyo hoja hii haina nguvu kutokana na kuwa kiswahili hakina maneno ya kiarabu pekeyake na kuwa ni tabia ya lugha kuazima maneno kutoka katika lugha nyingine. Chunguza etimolojia ya maneno  yafuatayo,
Shule, bibo, skuli, na chai.


2. Kiswahili ni lugha chotara (pijini na kreoli)

Mtazamo huu unaona kuwa kiswahili kimetokana na muunganiko wa waarabu na wabantu. Kwa mujibu wa profesa Noor Sharif, katika makala kiswahili kinawenyewe alitetea ukrioli wa kiswahili. Aisha somo hili litajadiliwa kwa mapana katika ukurasa wake.


3. Kiswahili ni kibantu
Huu ni mtazamo unaopata mashiko kwa wataalam mbalimbali toka zamani.

Hoja zifuatazo zinaonesha ubantu wa kiswahili.

Hoja za kihistoria

1. Ugunduzi wa Al-Idris
Ulifanyika huko Sicily kati ya mwaka 1100-1166 B.K kwenyevmahakama ya Mfalme Roger II. Katika ugunduzi huo, aligundua kwamba Kiswahili kilipata kuandikwa kabla ya Marne ya 10 BK. 

Al- Idris pia alikuwa mtu wakwanza kugundua jina la zamani la Zanzibar kuwa Ungudya, ambalo sasa ni unguja
Vilevile alitaja majina ya aina za ndizi zilizokuwa zinapatikana Zanzibari kama vile sukari, muriani, mkono wa tembo ambayo wataalamu wanaoshadadia ushahidi huu wanadai ni yakibantu.

Maswali yakujiuliza
-Je kiswahili kinamaandishi yake?

Hoja ya msingi  kiswahili kilianza kuandikwa kwa kiarabu na baadaye kilatini soma historia ya Ushahiri andishi wa kiswahili.


2. Ushahiri wa Marco polo
Huyu alikuwa mwanageografia wa kizungu aliyeweza kusafiri sehemu nyingi duniani. Katika baadhi ya maandishi yake anarhibitisha hivi, " Zanzibar ni kisiwa kizuri ambacho kina mkubwa wa mzunguko wa maili 200. Watu wrote wanaabudu Mungu wanamfalme wao na wanatumia lugha yao  na hawalipi kodi kwa mtu.
Niwazi kuwa maelezo ya Marco polo yanathinitisha kuwa kiswahili kilikuwepo hususani alipotajabmajina ya ndizi ambayo ni ya asili ya kibantu, hivyo kuthibitisha kuwa kiswahili asili yake ni Kibantu

Pamoja na hayo maandishi hayo hayoneshi ukiwa kulikuwa na mwingiliano wa hao watu wa Zanzibar na watu wengine kama waarabu.
Shahidi nyingine ni

Ushahidi wa Al- massoud (915- B.k)

Kitabu cha Peryplus

Ushahidi wa Ibn Batuta

Ushahiri wa kiswahili
Na utafiti wa Dakta Alper

Tutaendelea kwajili ya ushahidi za kimsamiati

Niwajibu wako kuendeleza mjadala katika sehemu ya komment