Bibi Titi Mohamed Historia ya Bibi titi mohamed -mwanamke shujaa na mwanaharakati wa ukombozi wa Tanganyika BIBI Titi Mohammed alizaliwa juni mwaka 1926 ,Dar es salaam, katika harakati zake za kuwakomboa wanawake ,Bibi Titi alikaririwa siku moja akisema; " Dhumuni langu kubwa ni kuhakikisha naamsha akili za wanawake waliolala na kubadilisha fikra na mitazamo yao na kuwaaminisha kwamba Uhuru wa Tanganyika utapatikana kama wanawake watajitambua". Kumbukumbu pekee tulinayo ya Mwanaharakati huyu katika taifa letu ni mtaa na Barabara ya Bibi Titi iliyopo Dar es salaam, Kihistoria Bibi Titi Mohammed aliingia katika siasa kwa kushawishiwa na Schneider Plantan ,akapewa kadi namba 16 ,na mumewe bwana Boi Selemani alipewa kadi namba 15.( Bibi Titi Mohammed aliolewa akiwa na umri wa miaka 13) Alikuwa muasisi wa Umoja wa wanawake Tanganyika (UWT) uliokuja kuundwa rasmi Mwaka 1963, wakati wa harakati za kupigania Uhuru alisimamia vikundi vya muziki kama vile " ...