MBABANE LAZIMA AFE LEO


Ofisa habari wa timu ya Simba, Haji Manara amesema kuwa mashabiki na watanzania wote kwa ujumla waungane leo kuishangilia timu ya Simba itakapocheza na Mbabane Swallows kwenye mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika.

Manara amesema wamejipanga kuhakikisha wana wapa furaha watanzania na mashabiki na kocha ameahidi kufanya makubwa pamoja na wachezaji na kitashushwa kikosi makini.


"Tunajua kazi kubwa ambayo tunatakiwa kufanya na tutasimamia kwa vitendo hasa mashindano haya ya kimataifa, mashabiki watupe sapoti na tuweze kupeperusha bendera ya taifa.


"Mbinu ambazo kocha mkuu Patrick Aussems amezipanga ni kubwa na ameahidi ushindi nyumbani ili tuweze kupenya hatua ijayo, wachezaji wana morali kubwa watafanya kweli," alisema.

Popular posts from this blog

HIZI HAPA SMS TAMU ZA KUMTAKIA USIKU MWEMA MPENZI WAKO

SMS na MESEJI 900+ za mapenzi

MIAKA 22 SASA TANGU KUZAMA KWA MELI KUBWA YA MV BUKOBA, TANZANI TUMEJIFUNZA NINI?